Ntuzu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 17,418
- 10,877
mie nadhani hayo majani ni majani halisi.Nafahamu kuwa unabii huwa una viwakilishi lakini pia nikujuze mkuu kuwa kuna wakati unabii unasimama na literal meaning yake na pia kuna wakati unazungumza both kiuwakilishi na kiuhalisia(two fold kama unabii wa chukizo la uharibifu wenye maana halisi ya taifa la Israel kuvamiwa na Warumi na maana ya kinabii ya kanisa la Mungu kuvamiwa na roho ya mpinga kristo kwa pamoja) Kuhusu malaika,hawa ni wajumbe wa Mungu ktk hali zote,mazuri na mabaya kwa maana kwamba hata anapoleta balaa kama lile la Sodoma anatumia malaika.Hata hapa tulipo malaika wapo wanafanya kazi zao ndio maana tunaishi otherwise Hallel angekuwa katumaliza kabisa.Nadhani mkuu unafahamu kuna malaika wanailinda dunia hii dhidi ya uovu lakini hatuwaoni.Hivyo hata suala la hao wa revelation 8 ni hivyo hivyo,watu hawataona malaika,watashuhudia physical disasters toka mikononi mwa malaika hao waliotumwa na Mwenyezi Mungu kuiadhibu dunia kwa mapigo(deluge).Mtu wa kawaida hataelewa kinachoendelea lakini mwenye ufahamu wa Mungu kupitia neno lake atazisoma nyakati na kujua wale malaika wameanza kazi.
mkuu,naomba niwe specific kwenye ufunuo 8.Soma aya ya 1 hadi ya 5 uone scenario iliyotokea mbinguni baada ya muhuri ya saba kufunguliwa,kukawa kimya mbinguni..hii inaonyesha ubaya na uzito wa jambo linalokwenda kutendeka.Sidhani kama katika miaka ya kizazi chetu hivi karibuni kuna jambo kubwa la kiasi hiki limewahi kutokea.Sidhani kama hilo tukio la kuanguka nyota linalosemwa kwamba limeshawahi kutokea miaka ya karibuni lina-fit description ya ufunuo 8 mkuu.Hebu mkuu Ntuzu na wana jf wengine tujaribu kusoma ufunuo 8:7-12 halafu tujaribu kutafakari kwa kina hasa ukizingatia maelezo ya mwanzoni mwa sura hiyo "mbinguni kukawa kimya...uvumba na maombi ya watakatifu(maombi gani haya yaliyomsababisha Mungu kuiadhibu dunia hivi)" halafu connect dots,utagundua hili tukio ni kubwa sana, ni cataclysmic event ambayo haijatokea bado na event hii iko associated na maombi ya watakatifu,kwamba viumbe watakatifu(bila shaka malaika na binadamu) wanamlilia Mungu hadi anaamua kuitwanga dunia na ile zahma inayoelezewa kuanzia aya ya 5.Bila shaka,kitendo cha Mungu kuitwanga dunia kinaeleza ni nini watakatifu walimwomba.Bila shaka ni kukomesha dhambi na uovu uliokuwepo duniani ambao unawaumiza watakatifu hawa ama kwa kuushuhudia(malaika) au kwa baadhi yao na hasa watakatifu binadamu kuwemo katika dunia hiyo na kuathirika.Je,tumeshafika kipindi cha uovu huo?mkuu Ntuzu bila shaka wewe ni mojawapo ya hawa watakatifu,dunia imeshakuchosha kiasi hicho?kipindi cha "taabu ya Yakobo" kimeshapita au umeshakipitia?je,descriptions za hii sura zina-fit tukio lolote la hivi karibuni kweli ambalo limeshatokea?
Mkuu kwa hiyo ufunuo 8 yanayosemwa hapo bado hayajatukia!
Nakubaliana na wewe kua wakati mwingine unabii hua unatumia neno moja kwa moja na si viwakilishi! Lkn ktk hizi sura za ufunuo kumetumika maneno mengi ya viwakilishi ambayo Km tungeweza kujua maana ya hayo maneno Km majani ya kijani, Miti, Maji, nzige etc tungelahisisha kuelewa!
Kuna kitabu ntakipata hivi karibuni kinaelezea haya vizuri! Ntaleta comment zake tuchangie pamoja!