The average lifespan of a Tanzanian male is about 50 years of age, so in light of that Kikwete is NOT young.
...nakubali ya kuwa ni maamuzi magumu kwa JK kuachia ngazi, lakini haikuwa rahisi wa Nyerere kuachia ngazi either. Mi nadhani siyo uzito wa uamuzi bali it is the depth of character of the individual that counts
Uzuri ni kwamba hakuna anayekatazwa kuota mchana...endeleeni na ndoto zenu
Wastani wa maisha ya wanaume watanzania ni miaka 50.
Kikwete ataishi miaka 50
Hii ni Falacy mzee.Kwa maneno mengine hoja yako haina mantiki kwa sababu hauwezi kutumia general observation ili u conclude kwa individual case, ila unaweza kutumia individual cases to derive a general conclusion.
Uzuri ni kwamba hakuna anayekatazwa kuota mchana...endeleeni na ndoto zenu
Kibunango,
Nakubaliana na wewe kuwa pengine tunaota mchana.
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa Kikwete atagombea 2010 na labda 2015 ili ajilinde yeye na marafiki zake, ingawa kama angekuwa ndugu yangu ningemshauri aachie ngazi mapema, yaani 2010, ili kuiepusha angalau familia yake na hukumu ya jumuiya.
Kwa hiyo kwa kuachia ngazi angeweza kukwepa haya yote, lakini nikimnukuu raisi wa zamani wa Zambia, Chiluba, yeye alisema wazi kuwa;
- Akiondoka sasa hivi hatahitaji kuiba tena BOT ili abaki madarakani
- Hatahitaji kufyatulia mtu risasi ili abakie madarakani
- Hatahitaji kuvunja sheria yoyote ili abakie madarakani
- Hatahitajika kuwahukumu hivi sasa au hapo baadaye maBesti wake, Chenge, Lowassa, RA n.k. ili kutimiza masharti ya wafadhili.
"Hakujua kama kiti cha uraisi ni kitamu hivi".
Sasa tujiulize kuna viongozi wangapi Africa wasiosafi wanaoachia utamu kiurahisi?
Sidhani kama sasa swala ni nani apendekezwe kuwa Raisi swala la msingi la sasa ni kujua mahitaji ya Tanzania ni nini na tunahitaji raisi wa aina gani ambaye atatuvusha katika mkanganyiko tulionao. Kwakuwa raisi tunaye aliyechaguliwa kwa asilimi 80% - naheshimu sana kura za wananchi. Lakini ushindi huo unakuja na wajibu, hasa nyakati kama hizi. Nivyema tufikirie huyu raisi afanye nini, maana tunamlipa mshahara kuongoza hii nchi ati! NGuvu kazi ya watu inapungua kwa kukimbia kusoma magazeti, na taarifa za habari, bila mwongozo. Anapaswa kuongoza.Kuna msemo unaosema Nyani haoni nyuma kwake.
Mutuambie basi nani bora zaidi leo.
......
Nadhani Ili JK afikirie kuacha uraisi
a) Kwanza lazima achague mtu atakayechukua madaraka ya uraisi, anayemwamini na kuahidi atamlinda, hii inamaana upinzani hawatachukua ungozi kwa miaka 10 ijayo.
b) Pili, kuwe na mabadiliko ya agenda katika tanzania, swala la ufisadi liwekwe chini ya kapeti. Na agenda iwe kujenga nchi, na hata vita ya ufisadi vikiendelea, iwe kiini macho tu.
Swala Je taifa liko tayari kufumbia macho ufisadi ili kikwete aichie ngazi? Faida zake ni nini!
.
- Mkuu vipi tena huu ndio utamaduni wa Upinzani? Ngazi inaachiwa kwenye kupiga kura sasa tusubiri ipigwe kura ndio ango'olewe, mkuu heshimu demokrasia maana huyu rais amechaguliwa na 80% ya sisi wananchi wa Tanzania, sasa tuheshimu japo kidogo na choice yetu ya rais wa jamhuri.
Respect!
FMEs!
JK kama akifikia maamuzi ya kutogombea hatakuwa mdhaifu. Akiacha kugombea ataacha historia kubwa sana katika uongozi, na kuondoka kwake kutaleta mabadiliko ya msingi sana katika maadili ya uongozi wa Tanzania.
Hayo umesema wewe. Tena ataonekana mdebwedo haswaa! Ni mangapi yanapita mbele yake anashindwa kuyakemea? Nakiri kusema hana cha kujivunia. Angefanya jambo moja tuone then aseme anajiuzulu, hapo angeheshimika.
Asie chie ngazi kabisa ,mwacheni aumwe na kichwa ,asipate usingizi ,lakini tunataka amalize ngwe yake ya miaka kumi,mwacheni amalize.
One day Yes tutapata kiongozi ambae atakuwa na ubavu wa kuwahoji hawa Maraisi wanaomaliza miaka kumi ,nini walikifanya na kwa nini hili na lile hawakulisemea wakati walikuwa na uwezo ,ndio maana yake asije mtu akasema mimi nilikuwa nilivalie njuga lakini sikupata miaka ya nyongeza ,ni kujitetea tu japo ni nonesense. Mwacheni Kikwete aendelee na mwengine lakini wakumbuke kama wababe hawatatokea upinzani na kuwaweka kiti moto basi humo humo CCM kutatokea mwenye usongo ambae atatumia hao viongozi waliopita kuwafurahisha wananchi na kujiwekeza zaidi kwa wananchi kuliko kwenye Chama na njia ya kujiwekeza huko ni kuwakamata mafisadi wote na kuwatia adabu ,ni very cheap political tactics to gain imani za wananchi just kwa kuwakamata watajwa wote wa ufisadi naamini ,atatokea kiongozi na kuitumia nafasi hii bila ya huruma na huyo ndie atakae kuwa hana ubia na wengine katika uongozi wake, unafikiri wananchi wakimpata kiongozi wa aina hiyo watakuwaje.Kama sikuona kuwa wamepata mkombozi ,ndio maana yake ,mwacheni amalize miaka yake mitano na mingine mitano ya bonus.
Petu Hapa: umeweza kunisoma vizuri na umempa maelezo mazuri Burn.
Mi naamini kile alichosema mchangiaji moja kuwa kuna haja ya kuwa na Reconciliation council kama ile ya Sauzi au Rwanda. Watu watoke watubu waliiba kidogo, waliiba mabilioni, wapewe adhabu inayolingana au wakatambike kimila whatever, lakini yaishe.
bm21
Kauli yangu ya kwamba JK ni kijana ndio propaganda iliyotumika mwaka 2005, wazee wapishe vijana waje. Alikuwa kijana kabisa! Leo kama tumezinduka tunasema sio kijana hayo ni maswala mengine. Kwangu naona ni mtu wa makamo ya kati, umri mzuri kabisa wa kuwa raisi kwa mtu yeyote.
Maandamano ya kupinga uamumizi, yatakuwa magumu kama wewe sio mwanachama wa ccm. Kwani mgombe uraisi anachaguliwa na chama chake. Labda nguvu uliyonayo ni katika kupiga kura! Je huwa unapiga kura!
Kibunango,
Nakubaliana na wewe kuwa pengine tunaota mchana.
Nakubaliana na wewe kabisa kuwa Kikwete atagombea 2010 na labda 2015 ili ajilinde yeye na marafiki zake, ingawa kama angekuwa ndugu yangu ningemshauri aachie ngazi mapema, yaani 2010, ili kuiepusha angalau familia yake na hukumu ya jumuiya.
Kwa hiyo kwa kuachia ngazi angeweza kukwepa haya yote, lakini nikimnukuu raisi wa zamani wa Zambia, Chiluba, yeye alisema wazi kuwa;
- Akiondoka sasa hivi hatahitaji kuiba tena BOT ili abaki madarakani
- Hatahitaji kufyatulia mtu risasi ili abakie madarakani
- Hatahitaji kuvunja sheria yoyote ili abakie madarakani
- Hatahitajika kuwahukumu hivi sasa au hapo baadaye maBesti wake, Chenge, Lowassa, RA n.k. ili kutimiza masharti ya wafadhili.
"Hakujua kama kiti cha uraisi ni kitamu hivi".
Sasa tujiulize kuna viongozi wangapi Africa wasiosafi wanaoachia utamu kiurahisi?