Endapo Salum Kikeke atateuliwa na Rais, Diaspora tutaanza kuona njia ya Uraia Pacha ikifunguka

hakuna anayehoji kuhusu sheria za uraia Kwa Sababu anayeteua ndiye mwenye nchi.
stop that nonsense, nchi ni ya wananchi. Rais siyo mmiliki wa watanzania 60 or so millions. We are not objects of the president
 
Sijui kwa nini wanaogopa au kusuasa kutupa uraia pacha.
Mh Rais tunaomba hili ulikamilishe awamu yako
 

Tendawili:

"Kitambua chako au chenu kitakuwa hatarini kwa ujio wa mtu kama Chikeke."
 
Kama mtu anafanya jambo kwa manufaa ya nchi, hakuna haja ya kuzingatia uraia wake. Yeyote atayeleta tija kwenye nchi mpeni uongozi
Umesema kweli sana! Kwani hawa raia si ndio majizi makubwa! Maccm, mapuuzi Sana!
 
kikeke anakwenda azm media
 
Vyovyote itavyokuwa, akitokea kuukwaa uteuzi anapaswa kuwa makini asiikosee serikali; vinginevyo namuasa arejee yaliyomkuta Ali Nabwa kule Zanzibar. Tanbihi: Ali Nabwa alifikia kuwa msaidizi wa Rais lkn baadae akageuka akawa mkosoaji mkubwa wa serikali kupitia gazeti la Dira kule Zanzibar. Yaliyomkuta wengine tunakumbuka.
 
Sioni tatizo lolote juu ya uraia pacha.
Tena kwangu mimi sioni tatizo hata akiteuliwa asiye raia wa Tanzania alimradi awe ana-perform vizuri zaidi kuliko Watanzania.

Fikiria uwe na wanahabari kama Musiba, si afadhali ukamteua asiye raia?

Fikiria mashirika kama ATCL, hasara kila siku, akiteuliwa Mwingereza, kama ilivyokuwa kwa Emirates Airline, halafu shirika likaanza kufanya vizuri, kunakuwa na sababu gani ya kupiga kelele kuwa mkurugenzi siyo Mtanzania?

Unaweza ukawa na mtanzaia kwenye nafasi fulani ambaye performance ni zero, ufujaji na udokozi 100%, shirika halikui, haliingizi faida wala kuongeza ajira, linaendeshwa kwa ruzuku ya Serikali; wakati unaweza kuwa na mgeni mwenye performance safi, mshahara mkubwa lakini haibi wala kufuja hata shilingi moja, shirika likakua, likapanuka, likaongeza ajira, likatoa huduma bora, likaipa Serikali gawio, gjarama za usafiri zikashuka.

Kwa mashirika kama ATCL, ilistahili tumtafute aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Fastjet. Iliwezekana vipi Fastjet watoe huduma ya usafiri kwa gharama za chini kiasi kile, na halina ruzuku?
 
Mbona wahutu wengi tu ni viongozi hapa?
Kuna mmoja hata aliwahi kuwa mkurugenzi wa uhamiaji? Nasikia
Sijui mtawali
Kuwa mhutu sio hoja, Kama umemuelewa vizuri mtoa mada anazungumzia uraia. Huyo mhutu anaweza kuwa mhutu lakini Hana uraia wa huko Bali Ana uraia wa Tanzania
 
Kama mtu anafanya jambo kwa manufaa ya nchi, hakuna haja ya kuzingatia uraia wake. Yeyote atayeleta tija kwenye nchi mpeni uongozi
Anajisahaulisha kwa mbunge wa bukombe sio RAIA lakini ni waziri. Uraia ni maneno tuu ya kumfanya MTU asiye na manufaa apoteze fursa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…