Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Kama una uwezo paa linakuwa la zege la flat ambalo utaweza kutumia kupanda majani, kuanika nguo au kupumzika tu. Hata mti unaweza kupanda.
Amandla...
Amandla...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali lako linashangaza kidogo. Si inategemea na ukubwa wa ghorofa unayojenga?Wataalamu na mainjinia majibu tafadhali.
Ni kweli sheria kulingana na planning space standards inataka kuwepo na building setbacks(nafasi Kati ya mwisho wa kiwanja na mwanzo wa linapojengwa jengo)Inategemea unajengea wapi. Kama ni eneo la kupimwa, utatakiwa angalau kuacha mita 1.5 na nusu kila upande na hivyo utabaki na upana wa mita 5 za kujenga. Kwa mbele utatakiwa kuacha mita 3 na nyuma mita 1.5 hivyo utabaki na mita 10.5 za kujenga. Nafasi yako ya kujenga itakuwa mita 5 kwa 10.5. Hizi zinatosha kabisa kujenga ghorofa. Changamoto utakayokuwa nayo ni ujenzi wa septic tank na soak pit ambazo kwa kweli nafasi iliyobaki haitoshi. Unachoweza kufanya ni kuinyanyua yote kwa nguzu na kuanza kukata vyumba kuanzia ghorofa ya kwanza. Hiyo nafasi ya chini ya unaweza kuweka septic tank na soak pit yako. Na hata gari unaweza kupaki.
Amandla...
Inafanya kazi. Tatizo ni kuwa code zetu hazizungumzii kuhusu vitu vinavyo "cantilever" kwenye hizo setbacks. Kwa sababu hiyo wengi wanaweka balconies hivyo kubakiza nafasi ndogo sana. Kwa mfano, mtu akiweka balcony ya mita 1 anaacha sentimeta 50 tu kutoka kwenye mpaka wake. Wa upande wa pili nae akifanya hivyo utaona inabaki mita moja tu kati ya balcony ya nyumba na nyingine. Ukiwa na ghorofa nyingi ndio hiyo nasi inavyozidi kuonekana kiduchu na kuzuia mwanga kufika katika ghorofa za chini. Ukiangalia nchi nyingine wanaruhusu watu kujenga kwenye mpaka wa upande moja ( wengine pande zote) na hivyo kuruhusu setbacks ya mita 3 upande uliobaki. Hiyo inaruhusu mwanga kufika chini. Majengo ya katikati ya miji hayana sababu ya setback za pembeni.Ni kweli sheria kulingana na planning space standards inataka kuwepo na building setbacks(nafasi Kati ya mwisho wa kiwanja na mwanzo wa linapojengwa jengo)
Lakini naona hii hafanyi kazi kwa bongo yetu hii maana kariakoo hakuna setbacks popote na bado wameweza kupewa vibali na wamejenga na mambo yanaendelea kama kawaida
Bado haifanyi kazi, maghorofa mengi hasa kariakoo hayana balcony both sides, balcony zipo kwa mbele tu. Ukiangalia picha namba mbili utaona kuna ghorofa hapo hazina balcony left and right sides, balcony zipo mbele tuInafanya kazi. Tatizo ni kuwa code zetu hazizungumzii kuhusu vitu vinavyo "cantilever" kwenye hizo setbacks. Kwa sababu hiyo wengi wanaweka balconies hivyo kubakiza nafasi ndogo sana. Kwa mfano, mtu akiweka balcony ya mita 1 anaacha sentimeta 50 tu kutoka kwenye mpaka wake. Wa upande wa pili nae akifanya hivyo utaona inabaki mita moja tu kati ya balcony ya nyumba na nyingine. Ukiwa na ghorofa nyingi ndio hiyo nasi inavyozidi kuonekana kiduchu na kuzuia mwanga kufika katika ghorofa za chini. Ukiangalia nchi nyingine wanaruhusu watu kujenga kwenye mpaka wa upande moja ( wengine pande zote) na hivyo kuruhusu setbacks ya mita 3 upande uliobaki. Hiyo inaruhusu mwanga kufika chini. Majengo ya katikati ya miji hayana sababu ya setback za pembeni.
Nimeona mnajadiliana kuhusu ukubwa wa vyumba. Ni kweli inategemea sehemu unapojenga. Mara nyingi wanasema upande mmoja usipungue mita 2.4. Hiyo ya mita 3 inatokana na vyumba vya nyumba za NHC za vyumba 6 kuwa na ukubwa wa futi 10 ( mita 3.3) kwa futi kumi kutumika kama standard. Sisi kwetu tunapenda dari lisiwe chini ya mita 3 kwa sababu ya mahitaji ya mzunguko wa hewa na kuruhusu kufunga ceiling fan. Katika maeneo ya baridi mita 2.7 ( hata 2.4 kwa mbinde) inatosha ili kuhifadhi joto ndani ya chumba.
Amandla...
Bila kusahau Singapore, Singapore hata kiwanja Cha mita 5 kwa 10 watu wanatoa ghorofa moja Kali Sana, inajengwa cube ya maana sanaUkienda Japan au sehemu za India hiki ni kiwanja kikubwa tu.
Amandla...
Sheria za setbacks za mita 5 ni kwa ajili ya residential areas. Maeneo ya mjini hayapaswi kuwa na setback ya mbele kwa sababu maduka n.k. yanatakiwa yaingiwe moja kwa moja kutoka kwenye side walk. Hakuna mji wa maana wenye setbacks za mbele kwenye majengo ya biashara katikati ya mji. Kunatakiwa kuwa na continuity kutoka jengo moja kwenda lingine.Bado haifanyi kazi, maghorofa mengi hasa kariakoo hayana balcony both sides, balcony zipo kwa mbele tu. Ukiangalia picha namba mbili utaona kuna ghorofa hapo hazina balcony left and right sides, balcony zipo mbele tu
Lakini pia kwa floor ya chini huwezi kuona space ya mita tatu ipo wazi Kati ya ghorofa na ghotofa.
Kuendelea kuthibitisha hii sheria haifuatwi angalia pia front setbacks kwa kkoo, standard na sheria inataka kuwe na mita si chini ya 5. Je maghorofa ya kkoo yana space kwa mbele kwa mita 5 au zaidi?
Kwenye bedroom standard ulichosema ni kweli, japo hata sehemu zenye baridi wanazidisha urefu wa 2.7 hasa wale wenye A house design, au wale wanaojenga loft apartments, unakuta kutoka kwenye floor mpaka ceiling ni mita karibu 6😂
Bado zinaangukia kwenye general standards.Sheria za setbacks za mita 5 ni kwa ajili ya residential areas. Maeneo ya mjini hayapaswi kuwa na setback ya mbele kwa sababu maduka n.k. yanatakiwa yaingiwe moja kwa moja kutoka kwenye side walk. Hakuna mji wa maana wenye setbacks za mbele kwenye majengo ya biashara katikati ya mji. Kunatakiwa kuwa na continuity kutoka jengo moja kwenda lingine.
Ukiangalia picha ya kwanza, balconies za pembeni ziko wazi kabisa na nafasi kati ya kuta na kuta inawezekana kabisa kuwa mita 3.
Amandla...
Nadhani unachanganya vitu. Hamna general standards. Kinachozungumzia setbacks ni development conditions. Pamoja na setbacks kunakuwa pia na miongozo ya kiasi gani cha kiwanja kinaweza kufunikwa ( coverage) na umla ya eneo linaloweza kujengwa katika kiwanja hicho ( Floor Area Ratio) na urefu wa jengo unaoruhusiwa. Hizi zote zinaongozwa na malengo ya Manispaa katika maeneo husika. Je wanataka nyumba moja moja, majengo yanayoweza kukaliwa na wengi, majengo yenye mchanganiko wa matumizi n.k. Hamna setbacks maalum kwa ajili ya hoteli au aina ya jengo lolote. Setbacks zinazowekwa ni minimum kwa hiyo kama unataka kuwa na garden kubwa mbele ya nyumba yako basi unaongeza setback. Hii ni tofauti katikati ya miji ambapo mara nyingi nia inakuwa majengo yawe katika msitari mmoja ( majengo yz zamani ya Acacia/Independence Avenue ambayo siku hizi inaitwa Samora Avenue). Majengo haya pia mara nyingi yanaruhusiwa kubanana ( sio hapa kwetu siku hizi) kwa kuwa na "party walls". Kuna miji mingine ilikuwa inadai hata ghorofa ziwe zinarudishwa nyuma ili kuruhusu mwanga kufika chini. Kwa kifupi setbacks n.k. hazina standards bali ni uamuzi wa mamlaka zinazohusika na mipango miji ya kila eneo. Mamlaka zetu kwenye hili eneo ziko nyuma sana ndio maana wanatumia miongozo ya maeneo ya makati katika maeneo ya biashara. Hilo ni kosa na litaharibu miji yetu.Bado zinaangukia kwenye general standards.
Lakini pia sio wote wenye ghorofa wameweka fremu, wapo walioweka chini offices na wengine hotel mwanzo mwisho lakini bado hakuna setbacks. Tena kwa standards za hotel setbacks ni kubwa
Naelewa wala sichanganyi, space standards zimewekwa kwenye sehemu specific na wakacategorize na yapo matumizi yanabaki na kuingia kwenye general standardsNadhani unachanganya vitu. Hamna general standards. Kinachozungumzia setbacks ni development conditions. Pamoja na setbacks kunakuwa pia na miongozo ya kiasi gani cha kiwanja kinaweza kufunikwa ( coverage) na umla ya eneo linaloweza kujengwa katika kiwanja hicho ( Floor Area Ratio) na urefu wa jengo unaoruhusiwa. Hizi zote zinaongozwa na malengo ya Manispaa katika maeneo husika. Je wanataka nyumba moja moja, majengo yanayoweza kukaliwa na wengi, majengo yenye mchanganiko wa matumizi n.k. Hamna setbacks maalum kwa ajili ya hoteli au aina ya jengo lolote. Setbacks zinazowekwa ni minimum kwa hiyo kama unataka kuwa na garden kubwa mbele ya nyumba yako basi unaongeza setback. Hii ni tofauti katikati ya miji ambapo mara nyingi nia inakuwa majengo yawe katika msitari mmoja ( majengo yz zamani ya Acacia/Independence Avenue ambayo siku hizi inaitwa Samora Avenue). Majengo haya pia mara nyingi yanaruhusiwa kubanana ( sio hapa kwetu siku hizi) kwa kuwa na "party walls". Kuna miji mingine ilikuwa inadai hata ghorofa ziwe zinarudishwa nyuma ili kuruhusu mwanga kufika chini. Kwa kifupi setbacks n.k. hazina standards bali ni uamuzi wa mamlaka zinazohusika na mipango miji ya kila eneo. Mamlaka zetu kwenye hili eneo ziko nyuma sana ndio maana wanatumia miongozo ya maeneo ya makati katika maeneo ya biashara. Hilo ni kosa na litaharibu miji yetu.
Amandla...
Space standards ni kwa ajili ya maeneo ya ndani ya majengo wakati hizo setbacks n.k. ni kwa ajili ya maeneo ya ujenzi na zinakuwa kwenye "Development conditions". Development conditions za Tanzania ni arbitrary ndio maana hata zinapozungumzia setbacks hazitoi ufafanuzi wa projections juu yake. Waraka wa ujenzi wa Manispaa kuhusu ujenzi katikati ya hauona miongozo yoyote ya maana maana una miongozo ya residential area. Ukiifuata hamna jengo litajengwa katikati ya mji. Kwa kuwa Kariakoo ilikuwa zamani sehemu ya makazi hakumaanishi development conditions zibaki zile zile kila wakitayarisha Master plan mpya. Masterplan iliyopo ya Oysterbay inaruhusu ujenzi wa mixed use buildings ( residential/commercial) pembezoni mwa barabara wakati eneo lote lilikuwa kwa ajili ya makazi ya viongozi wa serikali!Naelewa wala sichanganyi, space standards zimewekwa kwenye sehemu specific na wakacategorize na yapo matumizi yanabaki na kuingia kwenye general standards
So general standards zipo, rejea UPA Act iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2018
Kaangalie planning space standards utaona zinazokua regarded as general na zilizo specific
Halmshauri(mamlaka za miji) zinaweza kuandaa waraka kulingana na aina ya matumizi na ukawa Kama muongozo wa ujenzi kwenye hiyo halmashauri lakini bado wata-adhere na ile UPA act ya 2018
Setbacks maalum zipo kulingana na aina ya matumizi, hiko kilichowekwa ni minimum tu
Mfano halmashauri ya jiji ilala wanao waraka wa ujenzi kkoo, tafuta huo waraka uone kama unafatwa kwenye ujenzi. Au mfano rahisi vituo vya mafuta kaangalie standards zake na masharti yake alafu ingia mtaani kaangalie kinachoendelea
Ni kweli Kuna kosa kutumia standards za residential kwenye maeneo ambayo ni commercial kama kkoo, lakini kumbuka hao wengi kkoo walikua ni residential wala hawakua na plot za makazi biashara
Hapana planning space standards sio kwa ajili ya ndani ya majengo, ni nje na setbacks inaingia ndani ya space standards, rejea UPA act 2018. Uzuri sheria zetu zimetoa tafsiri vizuriSpace standards ni kwa ajili ya maeneo ya ndani ya majengo wakati hizo setbacks n.k. ni kwa ajili ya maeneo ya ujenzi na zinakuwa kwenye "Development conditions". Development conditions za Tanzania ni arbitrary ndio maana hata zinapozungumzia setbacks hazitoi ufafanuzi wa projections juu yake. Waraka wa ujenzi wa Manispaa kuhusu ujenzi katikati ya hauona miongozo yoyote ya maana maana una miongozo ya residential area. Ukiifuata hamna jengo litajengwa katikati ya mji. Kwa kuwa Kariakoo ilikuwa zamani sehemu ya makazi hakumaanishi development conditions zibaki zile zile kila wakitayarisha Master plan mpya. Masterplan iliyopo ya Oysterbay inaruhusu ujenzi wa mixed use buildings ( residential/commercial) pembezoni mwa barabara wakati eneo lote lilikuwa kwa ajili ya makazi ya viongozi wa serikali!
Suala la vituo vya mafuta linatakiwa kuwekwa kwenye Masterplan. Naamini utitiri wake ni kutokana na masterplan iliyopo kutoa mianya kibao ambayo wajanja wanatumia. Sidhani kama kuna miongozo yeyote rasmi kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta au aina yeyote ya majengo. Dar es Salaam kulikuwa na ghala za silaha za kivita katikati ya makazi sembuse vituo vya mafuta!!!?
Tatizo la mipango miji ni zaidi ya yanayo endelea Kariakoo.
Amandla....
Si kweli, inatoa muongozo vizuri tu na ndio kitu hata huyu waziri wa sasa anapambana nachoUkiangalia Urban Planning Act 2007 iliyoongezewa 2018 haitoi miongozo yeyote kuhusu petrol stations isopokuwa kuziweka kwenye User Group D inayohusu maduka. Hilo ni pungufu kubwa.
Amandla....
Unaweza kujenga Ndugu.Wataalamu na mainjinia majibu tafadhali.