Hakuna sheria za mpira za wazanzibari na za FIFA, hiyo ego yenu pelekeni kwenu hapa zinafuatwa sheria, kanuni na taratibu za FIFA.Nataka nikufahamisheni kuhusu wa Zanzibari
Wazanzibari wakweli usiwachezee kwenye utu wawo.
Mfano kaja kuomba chakula ananjaa, kama utampa chakula na kumtupia chini sahani basi atakuwachia mwenyewe chakula chako na ataondoka na njaa yake hatokula.
Huwezi kumnyanyasa mzanzibari katika utu wake.
Feisal kadhalilishwa utu wake dio maana bora umaskini kuliko kurudi yanga ikiwa walomdhalilisha wapo bado.
Yanga hawamhitaji Feisal kwanini wanamzuwiya? wamefika Final bila ya feisal. Lakini chiyo sababu hawataki timu ingine imchukuwe akaja kuwapa taabu.
Pia hiyo siyo ndoa kwamba ukimchoka mume au mke unaamua kuomba talaka unaenda kwenye maisha mengine. Taratibu na sheria lazima zifuatwe.
Sheria za mpira hazipingwi na ubishi wa kizanzibari bali na kanuni za FIFA, ameitwa na kupewa option tatu, ipi aliyoitekeleza? Huo ushindani wenye chembechembe za uchawi.
Yanga haina cha kupoteza bali inalinda heshima na taswira ya taasisi, akiamua kukaa bila kucheza mpira anamkomoa nani? Kuna mzanzibari pale Mudathir, yuko Ibrahim Bacca, Farid Musa wao hawanyanyaswi? Mchangieni aende CAS