Eng Hersi Said Simamia Misingi ya Kanuni na Sheria za Mpira. Mshauri Rais Samia asivuke Mipaka

Eng Hersi Said Simamia Misingi ya Kanuni na Sheria za Mpira. Mshauri Rais Samia asivuke Mipaka

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Habari wanajamvi.

Leo amesikika Rais wa Tanzania Akimdadavulia Rais wa Yanga SC Bw Eng Hersi Said kwa lengo la
kumuhimiza ahakikishe Mchezaji Feisal Salum anapata haki yake.

Ninacho fahamu kuwa Mama Samia hana ufahamu sahihi wa kinacho endelea baina ya mgogoro uliopo kati ya Yanga SC na Mchezaji husika. Hisia zake kama Mzanzibar ndizo zimempelekea kusukumwa kutoa mapendekezo yake pasi na kuhitaji kulifahamu zaidi swala hilo.

Ndugu Hersi Said, unapaswa kucheza karata zako makini mno kwenye hilo. Kumbuka Mama Samia ametumia gharama kiduchu sana kwenye kampeni ya zawadi za kila goli, Dinner la Ikulu pampja na usafiri wa ndege. Kumbuka hajafanya haya si kwa mapenzi ya dhati na masuala ya michezo, bali alilenga zaidi kuilaghai taasisi ya michezo ili iache kusimamia misingi ya kisheria na kikanuni ya michezo.

Kwa kawaida, ni muhimu kwa Rais wa nchi kuzingatia majukumu yake kikatiba na kutofautisha majukumu ya mamlaka nyingine za kiserikali na taasisi mbalimbali. Mgogoro kati ya klabu na mchezaji ni suala la kisheria ambalo linapaswa kusuluhishwa na mamlaka husika za sheria na kanuni za michezo.

Rais Samia Anahitaji Elimu zaidi.

Kwa hiyo Rais wa nchi kuingilia kati ktk mgogoro kama huo unaweza kusababisha mchanganyiko wa majukumu na kuingilia uhuru wa mamlaka nyingine. Ni muhimu kwamba kila mamlaka ifanye kazi yake. Kitendo cha Rais kuwapa Incentives mbalimbali basi isiwe sababu ya kuhalalisha kuingiliana ki mamlaka katika mihimili inayo jitegemea kiutendaji.

Rais Samia anahitaji mrejesho, Basi ni wasaa sahihi kuhakikisha anaandikiwa mrejesho wa kumuelimisha kuwa masuala ya migogoro ya kisoka/kimpira yana namna yake ya kutatuliwa. Muelewesheni kuwa zipo sababu za msingi kwanini hili suala linakawia kufikiwa tamati.

Ni vyema akafahamu kuwa uvunjwaji wa taratibu na mchezaji yeyote wa klabu ni lazima kuadhibiwe pasi na kujali kama huyu ni mchezaji wa kizanzibar, wa bara au wa kimataifa. Na hukumu kwa mchezaji wa namna hiyo hautotokwa kwa upendelea wa kibusara eti kwa kisingizio kuwa mchezaji ni mzawa au la.

Mshaurini Rais kuwa licha ya kuyafurahia mafanikio haya madogo ya klabu, kuna watu nyuma ya pazia ambao wanawekeza pesa zao na wasingependa kuona wanapata hasara ktk biashara ya mauzo ya wachezaji. Tukiruhusu kuingilia maamuzi ya taasisi huru ambazo zina sheria zake za usuluhishi basi tunajiweka katika nafasi ya kuwafukuza wawekezaji aina ya wakina GSM na Mo Dewji katika mpira wa Tanzania.

Kuna madhara makubwa sana endapo klabu kama klabu itashindwa kusimamia misingi ya taratibu zake na kusuluhisha migogoro na kesi za kimpira kwa kutumia tu mapendekezo ya wana siasa. Je Mama Samia anatoa ushauri kama nani? Je ni kama mtu mwenye ufahamu wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa mpira? au Kama
 
Mualiko wa ikulu umekua mchunguu, pilau limegeuka boko boko.

Sahivi ndo mnajua serikali haitakiwi kujihusisha na masuala ya soka? Alipokua anatoa ndege ya serikali buree? Na gharama zote zile? Mbna mlikua hamu muambii hilo??

Tulieni dawa iwaingie vizuriii, na ameshasema hivyoo, kinachotakiwa ni utekelezaji tyuuh.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] patamu hapoooo.
 
Hata nyie hamna ufahamu wowote wa mfuko gani uliotumika kutoa zile pesa la goli la Mama.

Feisali wiki hii ataachwa huru na vile vimidomo mlivyokuwa mnachonga kwa kujiona ma King Kong wa kufuata sheria now vitakata.
 
🤣🤣wakati akipokea ndege ya serikali bure hakuvuka mipaka?wakti akipokea mil 20,ilhal walofungwa nyumban hakuvuka mipaka?puliiizzzz,sikuzote masikini hana sauti,imeisha hiyooo
Kwani nani alimuomba atupatie ndege?
Kwani nani alimuomba incentives za magoli?

Hawezi kulaghai taasisi kwa dinner ya Milioni 200.
 
Kanuni zinaeleza mikataba isivunjike mpaka huko CAS.

Fei hana faida yoyote Yanga kama hachezi. Mwambieni awalipe muachane naye. Hakuna maslahi yoyote kwa club mkiamua kumng'ag'ania. Raisi yupo sahihi. Yanga ni kubwa, Fei ni mdogo kumkomoa hakuna malsahi yoyote kwa club.
Hakuna anaye mngangania.

Ameambiwa aje mezani ili wajadiri masilahi ya pande zote kwakuwa hawezi kuondoka iili hali bado yuko kwenye mkataba wake..
 
Gharama za Algeria na kurudi = 200,000,000
+
Ndege hadi Mbeya 30,000,000
+
Ubwabwa wa Ikulu = 20,000,000
+
Goli la Fainali kwa Mkapa = 20,000,000

Jumla = 270,000,000

Gharama za kumuachia Feisal Salum = 270,000,000

P.S. Feisal ataambiwa hata ile pesa aliyotakiwa kurudisha ili avunje mkataba amesamehewa abaki nayo. Kabla msimu haujaisha rasmi, Feisal atakuwa ameanza mazoezi Bunju.
 
Rais Samia amesema "ANAOMBA" wakalimalize swala la Feisal, hapendezwi na ugomvi. Hajasema kama kuwalazimisha au kama amri. Ni "OMBI" ametoa ambalo linaweza likakubaliwa au kukataliwa na hao viongozi wa yanga!!!

Kosa lake ni nini hapo? Mipaka gani achunge?
 
Bwana mdogo ulikua hujui kwamba Rais wa Nchi hii ni Alpha na Omega?

Usijichoshe kubonyeza Keyboard hapa ukidhani kuna chochote kitabadilika zaidi ya agizo la Rais ni amri.

Bear in mind hata boss wenu GSM kaahidiwa kutobinywa binywa katika biashara zake. Sijui wewe una uwezo wa kuwa mwekezaji ili GSM akuachie timu?

Eng. Hersi na cabinet yake usiku huu wameshajadiri namna ya kumrelease dogo, sasa tunatarajia wewe na jamaa zako muandamane kumpinga Hersi.

Goodnight.
 
Back
Top Bottom