Eng. Yazid Mabala, Mdau wa Maendeleo Anayeleta Chachu Ndani ya Mwibara - Bunda - Mara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

ENG. YAZID MABALA, MDAU WA MAENDELEO ANAYELETA CHACHU NDANI YA MWIBARA - BUNDA - MARA

Eng. Yazid Mabala ambaye ni Mdau wa Maendeleo aliyejikita kuleta chachu ya maendeleo ndani ya Mwibara, Bunda Mkoa wa Mara ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyewekeza sana katika kuwatumikia Wananchi wote na Watanzania kwa ujumla bila ubaguzi na anaeziishi 4R za Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa Vitendo.

Katika upande wa utunzaji wa Mazingira nchini, Eng. Yazid Mabala ametoa mchango mkubwa wa Utunzaji wa Mazingira kwa kutoa miche ya Miti 5,000 ikiwa ni Miche ya Miti mchanganyiko ndani ya Mwibara-Bunda, Mara ili kuhakikisha Tanzania inaendana na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kutokana na Sera ya Umoja wa Mataifa ya utunzaji Mazingira.

Aidha, Eng. Yazid Mabala katika eneo la Michezo amekuwa mstari wa mbele kuchangia sekta ya Michezo Mwibara- Bunda kutokana na Umuhimu wa Michezo kwenye jamii kwani Michezo inaleta Umoja, Michezo ni ajira kwa vijana, Michezo ni sehemu ya kujenga afya ya mwili na akili.

Mwaka 2021, 2022, 2023 na Mwaka 2024, Eng. Yazid Mabala amewezesha Ligi ya mchezo wa mpira wa miguu ndani ya Mwibara ambapo ametoa vifaa vya michezo ikiwemo Mipira, Jezi, Maji na Mbuzi kwaajili ya mshindi wa mashindano ya Michezo yaliyofanywa chini ya ufadhili wake.

Mwaka 2021 Eng Yazid Mabala akiwa kama MDAU mpenda maendeleo alipata Ombi kutoka Chama Wilaya la kuchangia katika uandikishaji wa Wanachama wapya akiwa kama MDAU WA MAENDELEO alifanikiwa kuchangia Simu Janja mbili ili kusaidia Ujenzi wa Chama hicho.

Mwaka 2021 Eng Yazid Mabala MDAU WA MAENDELEO aliwezesha kufanyika kwa kongamano kubwa la kuwajenga Vijana Kifikra katika kujisimamia Kiuchumi na kuziibua Fursa zilizojificha za Uzalishaji ili Vijana hao waendelee kujisimamia wao wenyewe siku zote ndani ya Jimbo la Mwibara na Mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Mhe Joshua Nasari Mkuu wa Wilaya ya Bunda wa Kipindi hicho na Mbunge wa Jimbo la Mwibara alipewa Mwaliko pia.

Mwaka 2021 alisaidia katika Ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Muungano kwa kuchangia trips za Mchanga na mawe katika Ujenzi huo.

Hayo yaliyotajwa hapo juu ni machache sana ambayo Eng Yazid aliyosaidiana na jamii yake, amefanya mengi sana na mengine si ya kutaja.

Mwisho, Eng. Yazid Mabala wakati akitoa salamu za Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya 2025 amesema kuwa, Mwaka 2025 utakuwa ni mwaka ambao atazidi sana . kuleta chachu ya jamii inayomzunguka ili iendelee kujisimamia katika uzalishaji kwa kuwapa mbinu mbalimbali za uzalishaji ili kuweza kukuza pato la mtu mmoja mmoja ili wawe kupiga hatua katika maendeleo ndani ya jamii inayozumzunguka kwani hiyo ndiyo furaha yake kuwatumikia wananchi na Watanzania kwa ujumla bila kujali Dini zao, Kabila zao, vyama vyao na hata Jinsia zao.
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-27 at 01.56.34.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-27 at 01.56.34.jpeg
    35.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.59.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.59.jpeg
    125.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.58.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.58.jpeg
    76.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.57.jpeg
    93.6 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.54.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.54.jpeg
    72.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.48.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.48.jpeg
    99.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.32.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.32.jpeg
    130.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.26.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.26.jpeg
    39.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.27.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.01.27.jpeg
    55.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.02.00.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.02.00.jpeg
    74.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.02.00 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-15 at 12.02.00 (1).jpeg
    60.8 KB · Views: 2
Naona anataka ubunge. Mnazunguka sana semeni anataka aende dodoma akapige meza hakuna kingine.
 
Kwa hapo Mwibara mtu ninayeweza kuwa na imani naye kama ataamua kugombea ni SADOCK MAGAI wa Bunere tuu (aliyekuwa na Fatma Karume, TAL kwenye Kampuni ya IMMA Advocates, na rafiki mkubwa wa Rais Hussein Mwinyi.). Hao waganga njaa wengine tupa kule.
 
Siasa imeanza kuelekea 2025, mwanza ilemela Kuna watia nia na wenyewe wanamikwala kama hii. CCM shughulikieni awa wanaozunguka majimboni na kwenye kata kabla ya muda wa uchaguzi.
 
Strategy uliyotumia ni ya kipuuzi mno.

Aisee!.
Asubiri tu April ama July, mbogamboga wataanza kupigana vikumbo. Kwa sasa akazane kuandaa kibunda.
 
Hapo hakuna kitu amefanya. Huwezi kwenda dodoma kwa pesa isiyozidi hata milioni nne ambayo hata bodaboda wa nanyumbu A anaweza toa.
Mipira 4 x 25,000 + Jersey full 16,000 x 22(set 2) + mbuzi 150,000 + printing jersey 1,500 = 655,000 + kamisaa na referees wanakula 15,000-20,000.

Kuwa mdau wa maendeleo peleka huduma za maji, umeme, ujenzi wa vituo vya afya, shule. Support ujenzi hapo utakuwa mdau wa maendeleo kwasababu hiyo hela anayoitoa kwenye michezo ni bei ya kitasa kimoja tu hapa mjengoni kwangu.

Ushauri. Akomae kwenye engineering huko CCM na mbowe watamlia hela hadi achanganyikiwe na ubunge asiupate.
 
ENG. YAZID MABALA, MDAU WA MAENDELEO ANAYELETA CHACHU NDANI YA MWIBARA - BUNDA - MARA

Eng. Yazid Mabala ambaye ni Mdau wa Maendeleo aliyejikita kuleta chachu ya maendeleo ndani ya Mwibara, Bunda Mkoa wa Mara ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyewekeza sana katika kuwatumikia Wananchi wote na Watanzania kwa ujumla bila ubaguzi na anaeziishi 4R za Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kwa Vitendo.

Katika upande wa utunzaji wa Mazingira nchini, Eng. Yazid Mabala ametoa mchango mkubwa wa Utunzaji wa Mazingira kwa kutoa miche ya Miti 5,000 ikiwa ni Miche ya Miti mchanganyiko ndani ya Mwibara-Bunda, Mara ili kuhakikisha Tanzania inaendana na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kutokana na Sera ya Umoja wa Mataifa ya utunzaji Mazingira.

Aidha, Eng. Yazid Mabala katika eneo la Michezo amekuwa mstari wa mbele kuchangia sekta ya Michezo Mwibara- Bunda kutokana na Umuhimu wa Michezo kwenye jamii kwani Michezo inaleta Umoja, Michezo ni ajira kwa vijana, Michezo ni sehemu ya kujenga afya ya mwili na akili.

Mwaka 2021, 2022, 2023 na Mwaka 2024, Eng. Yazid Mabala amewezesha Ligi ya mchezo wa mpira wa miguu ndani ya Mwibara ambapo ametoa vifaa vya michezo ikiwemo Mipira, Jezi, Maji na Mbuzi kwaajili ya mshindi wa mashindano ya Michezo yaliyofanywa chini ya ufadhili wake.

Mwaka 2021 Eng Yazid Mabala akiwa kama MDAU mpenda maendeleo alipata Ombi kutoka Chama Wilaya la kuchangia katika uandikishaji wa Wanachama wapya akiwa kama MDAU WA MAENDELEO alifanikiwa kuchangia Simu Janja mbili ili kusaidia Ujenzi wa Chama hicho.

Mwaka 2021 Eng Yazid Mabala MDAU WA MAENDELEO aliwezesha kufanyika kwa kongamano kubwa la kuwajenga Vijana Kifikra katika kujisimamia Kiuchumi na kuziibua Fursa zilizojificha za Uzalishaji ili Vijana hao waendelee kujisimamia wao wenyewe siku zote ndani ya Jimbo la Mwibara na Mgeni Rasmi katika kongamano hilo alikuwa Mhe Joshua Nasari Mkuu wa Wilaya ya Bunda wa Kipindi hicho na Mbunge wa Jimbo la Mwibara alipewa Mwaliko pia.

Mwaka 2021 alisaidia katika Ujenzi wa darasa katika Shule ya Msingi Muungano kwa kuchangia trips za Mchanga na mawe katika Ujenzi huo.

Hayo yaliyotajwa hapo juu ni machache sana ambayo Eng Yazid aliyosaidiana na jamii yake, amefanya mengi sana na mengine si ya kutaja.

Mwisho, Eng. Yazid Mabala wakati akitoa salamu za Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya 2025 amesema kuwa, Mwaka 2025 utakuwa ni mwaka ambao atazidi sana . kuleta chachu ya jamii inayomzunguka ili iendelee kujisimamia katika uzalishaji kwa kuwapa mbinu mbalimbali za uzalishaji ili kuweza kukuza pato la mtu mmoja mmoja ili wawe kupiga hatua katika maendeleo ndani ya jamii inayozumzunguka kwani hiyo ndiyo furaha yake kuwatumikia wananchi na Watanzania kwa ujumla bila kujali Dini zao, Kabila zao, vyama vyao na hata Jinsia zao.
Hivi ni KWA NINI UJINGA HUU UNAENDEKEZWA NA KUSHAABIKIWA? MBONA UCHAFUZI UKIKARIBIA HAYA YANATOKEA SANA?
TUACHE HAYA MAMBO YA KALE,TULETE MAENDELEO NA SIYO MBUZI WA KITOWEO.
 
Sawa, tumesikia single tu ulingoni, hapa jukwaani sidhani km kunafaa sana kuleta wasifu wake, nahisi wana-Bunda ni wachache sana huku.! 😢
 
Back
Top Bottom