Elimu ya bure..
Kwa gari lako na kwa mazingira ya Tanzania tumia 5w 30,
Ukikosa nenda 10w 30.....
.Anayekuambia hizi oil ni za nchi za baridi amekariri bila kusoma...
Iko hivi..
5w 30 ina uwezo wa kuhimili baridi kali kuanzia -30°C bila kupoteza viscosity yake...pia oil hii ina uwezo wa kuhimili kiwango cha juu cha joto ambacho ni +40 °C bila kupoteza viscosity yake..
Hiki kiwango cha joto nilichotaja ni joto la mazingira unayoishi (outside temperature)
10w 30 ina iwezo wa kufanya vizuri kuanzia joto la -20°C mpaka joto la +40°C...
Hii ina maana kwamba oil 5w30 na 10w 30 zina uwezo wa kusambaa haraka sehemu za injini hata kama gari limewashwa kwenye mazingira ya baridi sana kibongo bongo tunasema Arusha, Iringa, Mbeya na maeneo mengine yenye baridi.
Pia inahimili joto kali kama la Dar, Zanzibar nk.
Kwa hiyo hizi oil zinamudu mazingira yote na ndiyo maana car manufacturers wa siku hizi wana recommend oil hizi zaidi siyo Nissan, Toyota,Honda, Subaru,Mazda n.k...
Ukinunua nunua full synthetic ukikosa ndiyo ununue hizi mineral oil ambazo usivushe 3000 km.
Synthetic unaweza ukaenda km 5000 na zaidi kama umefunga oil filler genuine ndiyo ufanye service nyingine..
Full synthetic inahimili dhoruba ngumu kama milima, matope, joto, baridi, racing bila kupoyeza viscosity yake....na bei yake imesimamia kucha.
Agalia fundi wa mwembeni asikushauri uweke SAE 40 ya kawaida...hii oil ni nzito sana na utakuwa unalitesa gari bila wewe kujua...
Oil ndiyo DAMU ya engine.....zingatia if you love your car.