Yanga imecheza zaidi ya mara 5 kwenye huo uwanja wa Sokoine dhidi ya Mbeya city, na mara zote hizo iliambulia tu sare na kipigo! Na kwa kipindi hicho ilikuwa chini ya usimamizi wa makocha tofauti!
Leo kama uliangalia mpira, wachezaji walijitahidi. Lakini utulivu usingekuwepo kwa sababu ya ubovu wa uwanja! Huo uwanja hata simba walishafunga mara nyingi tu na wapinzani wao.
Mashabiki tujitahidi kuwa na subira. Ligi ndiyo kwanza imeanza. Tukiingia kwenye siasa kama za mashabiki wa simba, kamwe haziwezi kuisaidia timu. Leo kwa kweli kocha alijitahidi kupanga kikosi sahihi ukilinganisha na mechi zilizopita. Ni vile tu ushindi haukuwa upande wao. Timu imepata sare, itajipanga kwa mechi zijazo.