Habari wanajukwaa na mashabiki wenzangu wa young Africans sports, natumai mko poa.
Binafsi kwa muda wa misimu kama mitatu hapa nyuma nimekua sifurahishwi na mwenendo wa raisi wa young Africans kwenye baadhi ya mambo.
Kwanza ameingia sana kwenye propaganda za simba, kila wanachofanya simba nayeye anaiga au mchezaji akiachwa na simba yeye anamsajili ama wale wanaomaliza mikataba anaforce mpaka anawasajili, ambapo zimekua ni sajili za hasara according to Mkude, Chama, na sasa Mohamed hussein.
Pili, sikuona sababu ya maana ya kumuacha Miloud Hamdi na kwenda kuchukua huyu zuzu Romain Folz ila ni ujinga uleule kisa simba walikua wana Fadlu David's kutoka south Africa 🇿🇦 nawewe ukafuata upepo wa kijinga kwenda kuchuka mwehu eti hacheki, huyu ni vyema mngemtafutia msaada wa kisaikolojia.
Na kama akiendelea kwa mechi kadhaa basi mwisho wa yanga kule CAF CL itakua ni makundi tena ikishika mkia.
Pia tutapoteza makombe yote tunayoshiriki, maana sioni kazi inayofanywa na huyu kocha.
Kubali tu kwamba uliyumba then fanya marekebisho turudi kwenye mfumo tuliouzoea.
Ali Kamwe pia apunguze maneno ya kwenye khanga yeye sio mvaa vijora, apunguze kuiongelea sana simba maana sio kazi yake, kama ni utani basi kwa kiasi.
#NB fanyeni kila kitu kwa kiasi.