Engineer Hersi Said kuna vitu hufanyi kiprofessional bali unakurupuka

Ila sio muda utaungana namimi kimtazamo, hata hersi mwenyewe atatimiza niliyoyaandika hapa kwa kumtimua Romain Folz
 
Tunakumbushana tu historia na pia kuweka kumbukumbu sawa. Wala hakuna ugomvi.
 
Wanae moloko
Leo Matola ndiyo alikuwa kocha mkuu eti wakati wanaongea na waandishi wa habari. Halafu kocha wa timu pinzani ya Namungo ni Juma Mgunda! Wakati anahojiwa, alikuwa anawashambulia tu waandishi wa habari, huku akileta ujuaji wake wa hapa na pale.

Kesho mtegemee upangaji wa matokeo usio na shaka yoyote ile kati ya Simba A vs Simba B.
 
Mkuu msimu ulioisha Yanga hawakutumia huu uwanja? Hakukuwa na viwanja vibovu kuuzidi huu uwanja wa Sokoine? Kwa taarifa yako ni kwamba Yanga ndio ilikuwa timu inayoongoza kushinda mechi nyingi za away pamoja na kuwa ni viwanja vibovu. Usitafute sababu zisizo za msingi, mpira sio history kwamba kwavile michezo ya nyuma timu ilishindwa kushinda basi tukariri kuwa Yanga haiwezi Mbeya city. Tumeona mpira na nilitoa angalizo tokea ile mechi dhidi ya wale wa Angola kuwa hamna kocha japo timu inashinda. Hatuona nafasi yoyote iliyotengenezwa zaidi ya uwezo binafsi wa Pacome na Diara. Hana mbinu na mpira ni hesabu za mbinu.
 
Uko sahihi mkuu, ila mwalimu huyu sio wa soka lile, hapo ndipo mnapagawa. Mshazoea sexy football ndio maana hamfurahii.
Tunachotaka sio sex football bali tunataka tuone timu inacheza mpira wa mipango. Mbona mnakuwa wagumu kuelewa? Hata tulivyokuwa na makocha waliotangulia, sio mechi zote ilicheza mpira wa pasi nyingi ila tuliona mbinu na mipango sahihi. Sasa timu hata kupiga counter attack haiwezi, build up haiwezi, mpira wa kasi haiwezi. Kwwnye kujilinda, muundo wake upo hovyo ni rahisi sana kupiga pasi inayovunja shape ya kiulinzi.
 
Kwake yeye wala hakurupuki ila anaamini afanyavyo ndivyo washabiki wake watakavyo, mfano siku ya yanga day kuna tukio lilokuwa na vibe kubwa zaidi ya utambulisho na mauno ya tsabalala? hapana, ndipo akili za mashabiki wa bongo zinapoishia na yeye engineer anapita humohumo, niliwahi kushauri hapa kuwa viongozi wetu waachane na siasa za utani wa simba na yanga zinatuchelewesha, twende kwenye professionalism
 
Umeuongea mpira mkuu hata mimi nakereka sana na hizo siasa
 
Mpira una matokeo matati. Yanga haijaandikiwa kushinda tu. Na ingekuwa hivyo, basi hata ladha ya mpira wa miguu nayo ingepotea.
 
Hapo mwisho kwa huyo msemaji wenu,huyu dogo naweza sema limbukeni amuangalie manara sasa hivi watu hawana shobo nae kila kitu kiende kwa kiasi bahati mbaya wanafamya dhihaka hadi kwenye brand za wadhamini. Sidhani wasemaji wa timukubwa wanatakiwa kua hivyo atleast yule Ahmed ana kiasi.
 
Reactions: Tui
Mpira una matokeo matati. Yanga haijaandikiwa kushinda tu. Na ingekuwa hivyo, basi hata ladha ya mpira wa miguu nayo ingepotea.
Unaongea kama vile sio mtu wa mpira, watu kiu yetu sio kushinda kwasababu timu haiwezi kushinda mechi zote. Ila tunataka tuone timu ikiwa inacheza kwa mipango kama timu sio kila mchezaji kutumia uwezo binafsi. Tuliwahi kutoa sare ama kufungwa huko misimu iliyopita na kila shabiki wa Yanga aliridhika na performance ya timu. Ila hujiulizi, kwanini timu ilikuwa imeshinda lakini bado watu walikuwa wanakosoa uwezo wa kocha? Hapa kwa Mbeya city ni trela tu, ila kwa kocha huyu, timu itapoteza point nyingi sana kwenye viwanja vya mikoani.
 
Mwananchi kuwa na imani na timu yako. Yanga bado ni timu nzuri. Na huyo kocha apewe muda. Rais wako wa klabu Injinia, anapenda makocha wasio na CV kubwa ili aweze kuwaburuza kwenye baadhi ya maamuzi ya ndani na nje ya uwanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…