Engineer kuongoza chuo cha biashara ni sahihi? Soma hapa

that isn't always a case mkuu...je unamfaham magufuli??? je yeye kasomea wapi maswala ya ujenzi?? na mbona anaongoza secta za ujenzi na anafanya vizuri! mfano mwingine ni rais wa zanzibar yeye ni daktari lakini mbona kawa rais!! UONGOZI SI ELIMU BALI NI UWEZO WA MTU!!!
 
Mkuu fuatilia mtililiko wa hoja vizuri,unayepaswa kumjibu ni frakitosho.Mimi nilikuwa najalibu tu kufafanua hoja yake ili umuelewe vizuri!
 
Last edited by a moderator:


Sio sahihi kufananisha ngazi ya urais na ukuu wa chuo. Rais anaongoza nchi yenye shughuli za aina mbalimbali ikiwamo ile aliyoisomea yeye. Suala linakuja kwenye kuongoza chuo ambacho ni special kwa masomo ya biashara pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu (business consultancy). Je huyu engineer ataweza kusimamia vyema bila kudanganywa na wasaidizi wake? Hebu kumbuka jinsi mama Zakia Meghji alivyozungukwa na wazee wa EPA na akakubali kuidhinisha fedha za EPA "bila kujua" (source yeye mwenyewe). Je angelikuwa mtaalamu wa masuala ya fedha na uhasibu asingeokoa zile fedha za EPA?
 
je unaifaham sua? mkuu wa chuo kasoma kilimo?? jamaa ni kiongoz urais pia ni uongozi so unavyosema nisifaninishe sijui unamaanisha nini?? na kama nchi ina shughuli mbali mbali kwani rais hawezi danganywa kwenye zile secta ambazo hazijui?? swala la wizi lipo tu hata kama umesomea au hujasomea!!! cha msingi jamaa kawa mkuu,basi ndo hali halisi mpeni sapoti na sio kukaa na kusema hafai akati watu wamekaa wameona anafaa wakampa nafasi!!!!!
 
Hii mada ilinipita......huyu jamaa anafaa na kaletwa hapo hili kuwanyoosha na kweli ameanza kuwanyoosha.CBE ya miaka ilee na amin si sawa na ya huyu Prof!!!!
 

Uongoz ni uongoz tu.....ni namna yakudil na watu wako wachini,wapo viongoz ambao hawana shule kivile lakin wanaongoza vizur na mambo yanakuwa mswano.
Jamani mwacheni tu huyu Prof awanyooshe!!!!
 
Huyo mzinguaj 2 tumeshazoea cbe ya totoz wauza utamu huyo anaharibu chaka lawauni
 
Eng..kuongoza ni sawa kabisa Prof huyo anauwezo wa kuongoza vizuri sana namjua fika,,,To be an Eng doesn't mean you can not rule the college
 
Swala la msingi hapa ungeweka Majukumu ambayo hatafanya kwa ufanisi kwa kutokua Mtaalamu wa mambo ya Biashara... Kabla ya kulaumu kuwa na ushahidi kwanza mkuu.
 

kwani daktari hawezi kuwa raisi?
 
Eng..kuongoza ni sawa kabisa Prof huyo anauwezo wa kuongoza vizuri sana namjua fika,,,To be an Eng doesn't mean you can not rule the college

Wanaomchukia huyo prof wapenda maovu....hataki upumbavu kabisa baba wa watu!!!Fanya kazi prof,nyumba uliyohamia ni chafu usiogope kusafisha la sivyo hata ww utachafuka.
 

Ndugu yangu frakitosho, kwenye mambo ya vyuo haiko hivyo kabisa, Luhanga ni Engeneer wa Umeme na alikuwa anaongoza Chuo pale UDSM chuo kilichokuwa na Facults mbalimbali ambazo sio za kiinjinia, SCience, Arts, Business, Law nk, sasa Luhanga alikuwa anawezaje kusimamia Facult ya sharia wakati yeye ni injinia? ............. hiyo hali unayoisema ni vyuo vyote iko hivyo, usiwe na shaka mambo yataenda tu
 
Last edited by a moderator:
Hatimaye chuo cha elimu ya biashara CBE kimempata mkuu mpya ambaye ni eng. prof. Emmanuel Mjema. Wadau mimi najiuliza inakuwaje injinia awe mkuu wa chuo cha biashara? Hamuoni kwamba ni mambo ya kujuana zaidi?

Kwangu sioni tatizo kama ana uwezo unaohitajika kuongoza hicho chuo.
Mbona head wa MBA pale Open University, Biafra ni Engineer na mambo yanakwenda sawa sawa. Hilo lisikupe taabu mheshimiwa labda jadili uwezo wake. Vile vile sijasikia kuwa Prof Eng Mbwete kashindwa kuendesha OUT simply kwa sababu ni engineer.
 

Umenichekesha sana mkuu
 
Hatimaye chuo cha elimu ya biashara CBE kimempata mkuu mpya ambaye ni eng. prof. Emmanuel Mjema. Wadau mimi najiuliza inakuwaje injinia awe mkuu wa chuo cha biashara? Hamuoni kwamba ni mambo ya kujuana zaidi?
hujui maana ya uongozi e,,,kama unajua maana ya uongozi basi hata HKL anaweza kuwa waziri wa nishati na madini na aka i run Tanesco /industry hiyo vizuri sana,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…