Engineer kuongoza chuo cha biashara ni sahihi? Soma hapa

Engineer kuongoza chuo cha biashara ni sahihi? Soma hapa

frakitosho

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
802
Reaction score
256
Hatimaye chuo cha elimu ya biashara CBE kimempata mkuu mpya ambaye ni eng. prof. Emmanuel Mjema.

Wadau mimi najiuliza inakuwaje injinia awe mkuu wa chuo cha biashara?

Hamuoni kwamba ni mambo ya kujuana zaidi?
 
Hatimaye chuo cha elimu ya biashara CBE kimempata mkuu mpya ambaye ni eng. prof. Emmanuel Mjema. Wadau mimi najiuliza inakuwaje injinia awe mkuu wa chuo cha biashara? Hamuoni kwamba ni mambo ya kujuana zaidi?
unamfaham huyu mtu?? unajua ni rais wa wapi?? je unajua elimu yake kasomea nini?? ulichosomea hakimaanishi wewe ni kiongozi bora au la?? au una maanisha injinia haruhusiwi kuwa kiongozi??
View attachment 81684
 
Usihofu eng luhanga alivyokuwa vc kulikuwa hakuna mgomo lakn alivyoingia ngwinu mkandala mambo yakaanza kuharibika napenda kuwapongeza wana cbe wamepata kiongozi wamtumie vizuri ktk mabadiriko, mangwini kuwa viongozi ni kasheshe
 
Hivi hakuna kozi za finance engineering au business engineering? Maana kama kuna Bsc Finance mzumbe university then si ajabu tukasikia finance engineering.
 
unamfaham huyu mtu?? unajua ni rais wa wapi?? je unajua elimu yake kasomea nini?? ulichosomea hakimaanishi wewe ni kiongozi bora au la?? au una maanisha injinia haruhusiwi kuwa kiongozi??
View attachment 81684

Sijasema kwamba engineer hafai kuwa kiongozi ila ninachomaanisha ni kuwa ni vyema kiongozi akawa ana ujuzi kiasi fulani juu ya kile anachokiongoza.

Hata kwenye katiba mpya wengi wamependekeza mawaziri wasiwe wabunge ili watu waweze kuteuliwa kutokana na cv zao.

Kwa mfano waziri wa elimu angekuwa mwalimu by profession asingeweza kushindwa kujibu hoja za wabunge kuhusu mitahala ya elimu.
 
Sijasema kwamba engineer hafai kuwa kiongozi ila ninachomaanisha ni kuwa ni vyema kiongozi akawa ana ujuzi kiasi fulani juu ya kile anachokiongoza. Hata kwenye katiba mpya wengi wamependekeza mawaziri wasiwe wabunge ili watu waweze kuteuliwa kutokana na cv zao. Kwa mfano waziri wa elimu angekuwa mwalimu by profession asingeweza kushindwa kujibu hoja za wabunge kuhusu mitahala ya elimu

Huyu Prof ni mchapa kazi sana. Amenifundisha computer programming na pia kozi za engineering managements.

Kwa kifupi ukipata CV yake utawapongeza CBE kwa kupata mtu sahihi.

Sent using wireless by wire
 
Sio sawakabisa , unless tanzania imeishiwa hazina ya wanataaluma wazuri wa biashara.
 
akili nyingi mpaka akaitwa engineer sio kilaza,an engineer can fit in any field,we call him a SECOND GOD
 
akili nyingi mpaka akaitwa engineer sio kilaza,an engineer can fit in any field,we call him a SECOND GOD

Uongozi bora hautokani na akili bali ujuzi. Sasa huyu prof. ana ujuzi wa mambo ya biashara? Yeye ujuzi wake ni engineering.
 
Ni muhimu ungejua kwanza kazi zake kama mkuu wa chuo, hata hapo CBE kuna walimu tofauti na wanaofundisha masomo tofauti.

Kazi yake ni kuwaongoza hao walimu na wafanya kazi wengine kufanya wanachotakiwa kukifanya, kama mkuu wa chuo haendi kuchukua nafasi ya mwalimu wa somo fulani.

Uhandisi kama ulivyo, nina hakika hakuna tatizo kwake yeye kuteuliwa - na hapo ndio maana halisi ya 'engineering' inajikita.
 
akili nyingi mpaka akaitwa engineer sio kilaza,an engineer can fit in any field,we call him a SECOND GOD
Mungu baada ya kuumba dunia alimwachia Engineer aiendeleze kwa magari, majumba, ndege, umeme, meli, etc
 
Ki ukweli Mhandisi unaweza kumfananisha na tabibu tu(MD),hao ndio pekee wanaomudu vizuri kuingia kwenye fani nyingine bila shida.
Tofauti na wahasibu, wanasheria na wengineo,wao kamwe hawawezi kuingia kwenye taaluma ya uhandisi au utabibu.
 
Labda wanaanzisha business engineering. Lakini nafikiri kiongozi anatakiwa awe na technical skills za kule anakoongoza. Tuone wasije wakamfanya kile walichomfanyia Dr. Lugoe. Watoe ushirikiano kazi ziendeleee.
 
Sijasema kwamba engineer hafai kuwa kiongozi ila ninachomaanisha ni kuwa ni vyema kiongozi akawa ana ujuzi kiasi fulani juu ya kile anachokiongoza. Hata kwenye katiba mpya wengi wamependekeza mawaziri wasiwe wabunge ili watu waweze kuteuliwa kutokana na cv zao. Kwa mfano waziri wa elimu angekuwa mwalimu by profession asingeweza kushindwa kujibu hoja za wabunge kuhusu mitahala ya elimu
yah uko sahihi lakin unamfaham john magufuli?? je kasomea wapi maswala ya ujenzi?? mbona ni amefit kwenye nafasi yake!!! mi nadhan enginerr ni engineer tu,na uongozi hausomwi shule ni kipaji na uwezo wa mtu!
 
Mleta mada hapo ni suala la Management skills basi.Swali dogo tu, ina maana wakuu wa shule za sekondari wanajua kufundisha masomo yote?Nina imani kwa uzoefu wake lazima ana uelewa na mambo ya uongozi ndiyo maana yuko hapo.
 
unamfaham huyu mtu?? unajua ni rais wa wapi?? je unajua elimu yake kasomea nini?? ulichosomea hakimaanishi wewe ni kiongozi bora au la?? au una maanisha injinia haruhusiwi kuwa kiongozi??
View attachment 81684
Mkuu unataka kupotosha hoja ya msingi ya frakitosho,yeye kwanza kabisa anakubali Engineer anaweza kuwa kiongozi mzuri katika mambo ya engineering works,kama vile DIT na maeneo mengine yenye uhusiano na engineering works.Lakini kuongoza chuo kinachojiusisha na biashara purely ndiyo inamtatiza!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom