English Grammar: Benki ya Posta Tanzania ni TPB Bank au TPBank? Ni sahihi kwa neno "bank" kutumika mara mbili?

English Grammar: Benki ya Posta Tanzania ni TPB Bank au TPBank? Ni sahihi kwa neno "bank" kutumika mara mbili?

Hii hutokea mara nyingi kampuni inapoji-brand upya. Kwamba baada ya muda fulani unakuta initials zinakuwa zinajulikana kuliko kirefu chake.
Hivyo, huwa wanai-rebrand kwa kufanya hizo initials kuwa neno kamili kwa maana ya kwamba kirefu chake kinakuwa hakina maana tena.
Mfano, CRDB Bank.

Au
American Telephone and Telegraph Company ilivyojirebrand upya kama AT&T Corporation (bila kirefu chake hicho) mwaka 1885 hivi.
Kwamba haikubadilika kuitwa 'American Telephone and Telegraph Company Corporation' bali 'AT&T Corporation'.
Na sasa inaitwa just AT&T Inc.

Kifupi, jina likisajiliwa kisheria lina maana hiyo hiyo unless kirefu chake kimekuwa specified.
 
Hiyo inaitwa TPB Bank, sio Tanzania Postal Bank kama ilivyo CRDB Bank, ambayo sio Cooperative and Rural Development Bank.

Vv
Bila shaka utakuwa umekula bia za kutosha kwa comment ya namna hii
 
TPB kirefu chake ni "Tanzania Postal Bank" kama sikosei. Sasa TPB Bank maana yake ni Tanzania Postal Bank Bank? Ni sawa na mtu anayesema "daraja la Selander bridge" anakuwa ametamka "daraja na bridge" kwa wakati mmoja wakati maneno yote mawili yana maana sawa???
View attachment 1171492
View attachment 1171493
NB: NSSF nipeni fao langu la mkupuo. Mtaani maisha ni magumu sana. Mungu anawaona mjue?
hii ndo East Africa ya mashariki
 
CRDB BANK
Cooperative Rural Development Bank Bank
Ujinga na upumbavu ulianzia hapa.

Cha ajabu zaidi CRBD ina matawi mengine urban areas.
 
Wangeandika TP Bank basi. Kuna bank ya Canadians inaitwa Toronto Dominion Bank. Kifupi chake ni TD Bank, si TDB Bank.
Halafu Wabongo ambao kiingereza ni lugha ya Tatu wanajifanya kujua zaidi
 
Haya ni makosa yaliyozoeleka katika jamii yatu kwa sasa. Nimeyaona sehemu kubwa sana ya Tanzania yakitumika kama vile hayajakosewa. Mfano. Ukiwa Arusha mtu atasema naenda "uwanja wa stadium" akimaanisha uwanja wa Sheik Amri Abeid.
Ukiwa Dodoma utaskia mtu anakuambia anasoma University of UDOM, akimaanisha University Of Dodoma.
Yapo mengi sana kiasi kwamba sasa hadi wasomi wetu wameanza kuwa wakurupukaji na kuyafanya kuwa kama official.
Wasomi wetu wabadilike makosa madogo kama haya yasiwepo ni kudhalilisha taaluma husika.
 
Mimi niliwahi wauliza wenyewe lakini WAKASEMA WATALISHUGHULIKIA lakini mpaka leo kimya (Nahisi walinipuuza)
 
Tpb bank ni jina la kibiashara ambapo mmiliki wake ni Tanzania postal bank.
Hi Ni kutofautisha Kati ya Tanzania postal bank ile ya miaka ya nyuma(benki ya kiserikali) na hi mpya ambayo imefanyiwa marekebisho ya kisheria kuwa benki ya kibiashara.japo mmiliki Ni yule yule posta. Yaani sawa na tpb bank iwe Azam na Tanzania postal bank awe s.s bakheresa company
 
TPB kirefu chake ni "Tanzania Postal Bank" kama sikosei. Sasa TPB Bank maana yake ni Tanzania Postal Bank Bank? Ni sawa na mtu anayesema "daraja la Selander bridge" anakuwa ametamka "daraja na bridge" kwa wakati mmoja wakati maneno yote mawili yana maana sawa???

View attachment 1171492

View attachment 1171493

NB: NSSF nipeni fao langu la mkupuo. Mtaani maisha ni magumu sana. Mungu anawaona mjue?
Boss wao Ni engineer hivyo grammar kwao si hoja,Ila kikubwa mzee meko anaona mabadiliko[emoji2420][emoji2420]
 
mfano ukisema Nmb kwa Tz kuna mtu hataelewa unamaanisha bank?
Kwa hiyo unamaanisha NMB hawajaongeza neno Bank kwenye logo yao kwa maana jina lao ni maarufu kiasi kwamba mtu akisikia tu neno NMB automatically anajua tu ina maanisha ni bank???
 
TPB kirefu chake ni "Tanzania Postal Bank" kama sikosei. Sasa TPB Bank maana yake ni Tanzania Postal
Unakosea hiyo.benki.inaitwa TPB
Imeshabadili jina baada ya kuingia soko la hisa
Inaitwa TPB bila ya kirefu chake
Hivyo.hivyo kwa CRDB.na NBC acha kukariri maisha
 
Wangeandika TP Bank basi. Kuna bank ya Canadians inaitwa Toronto Dominion Bank. Kifupi chake ni TD Bank, si TDB Bank.
Wangeandika TP bank wangepata tabu sana kueleweka na watu, maana hiyo TPB Bank ndio watu walikuwa wakiita hivyo, na wenyewe wakaamua kunata na biti hivyo hivyo. Wangefanya rebranding kujiita TP bank wangechanganya watu, wangedhani ni bank mpya
 
Back
Top Bottom