Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Ki ukweli kabisa kwa wanaojua biolojia na psycholojia ya watoto watakubaliana namimi hii haiko sawa...sisi wazazi tunamatakwa yetu juu ya watoto wetu.Ni saa 10 na nusu alfajiri ninaamka kujiandaa kwa ajili ya kwenda harakati, nafuata taratibu zangu za kila siku, napiga goti namshukuru Mungu kwa uzima naingia bafuni kujishikashika na sabuni pamoja na maji ya baridi ili kuzimua akili ikae mguu sawa. Huwa nachukua nusu saa tu kujiandaa na kwenye saa 11 kamili ninakuwa njia kuelekea ofisini ila kuna kitu nimekiona hakipo sawa kwa zaidi ya miaka miwili.
Tokea kumekuwepo na utiritiri wa hizi shule za binafsi maarufu kwa jina la English Mediums basi sio ugeni kukutana na gari la shule (School bus), mabasi ya njano, haswa majira haya ya saa 11 na saa 11 na nusu zikiwa na watoto wadogo wakienda shule. Ni jambo la kufikirisha sana, kiasi kwamba ukitazama ndani ya magari hayo utakuwa kitoto kimeuchapa usingizi bila wasiwasi, hajafunga mkanda, kiufupi usalama ni mdogo kwa watoto wetu.
Masuala ya msingi ambalo nimepata kuona tunawaumiza watoto wetu ni mambo mawili:
Suala la kuamka kuwahi shule, kwa hakika ninathubutu kusema kuwa Mtoto anayesoma shule ya Msingi Muungano anaenjoy Maisha ya shule kuliko ambaye anasoma St. X English Medium. Unaweza kukataa ila nitakupa scenario hizi kadhaa uone mtoto wa kidumu na mfagio anaishi huku wenzake wakiishia. Mtoto anayesoma Muungano anaweza kuamka saa 12 na nusu tena kwa bakora za kutosha kutoka kwa Bi Mkubwa na darasani akaingia saa 1 na nusu, Maisha yanasonga. Mapumziko kwake ni kwenda kucheza mpira na kula barafu za mama Aisha. Turejee kwa Mtotoanayesoma St. X English Medium ambapo tokea saa 11 na nusu au saa 12 anazunguka na basi mji mzima na akiingia darasani saa 1 kamili, mapumziko yao watakunywa uji na kupumzika kweli. Wadau wa elimu tazameni kwa ukaribu jambo hilo, binafsi kuna shule zaidi ya tano ambazo saa 12 kasoro mbasi yao yanazunguka na watoto wakiwa wameuchapa usingizi wa kutosha. Montesorri, Jabal Hira, pamoja na Buyegi Archbishop Mayala nimepata kupishana na magari yenu mara kadhaa alfajiri watoto wakiwa wameuchapa.
View attachment 3052567
Suala ya mabegi makubwa na mazito, nina Rafiki yangu ambaye mtoto wake amepata ulemavu kwenye mgongo, mtoto wa darasa la nne ila anabeba begi zito utadhani utingo. Hakuna maana ya uwepo wa ratba za masomo (timetable) halafu wanafunzi wakapewa maelekezo kuwa abebe vifaa vyote vya shule kila siku. Kwanini shule zisitengeneze makabati ambayo watoto watahifadhi vifaa vyao na kutembea na vifaa kiasi tu. Kuna wakati Bismarck na Tulele walikuwa wanaongoza kwa watoto wao kubeba vitu vizito, yaani begi utadhani mkimbizi!? Askari wa Barabarani kuweni makini na mabasi haya kwani sidhani kama ni utaratibu kuendesha watoto kwa mtindo wenye hatari namna hiyo. Simamisha gari kisha ingia watazame watoto waulize kama mikanda inafaya kazi, je kuna Fire extinguisher na vifaa vya usalama, ongea na msimamizi wa watoto upate kujua hali halisi ya watoto.View attachment 3052561
Mamlaka husika zifanye jitihada za msingi katika hili, watoto wetu tunawapatia ulemavu kwa uzembe wa kijinga jinga, watoto wapate usingizi wa kutosha, waamke mapema ila sio saa 10 au 11 kwa kigezo cha kuwahi shule! Hakuna tuzo ya mwanafunzi aliyewahi shule. Tuache kuweka pamba masikioni.
SIO KWA UBAYA! TUNAREKEBISHANA TU!
Yaani Mzazi anadictate nini mtoto aweze ku achieve bila kujia madhara na mzigo kwa mtoto.
Juzi natoka Kinondoni nasindikiza Mgeni wangu anayesafiri na Basi la Esta linampitia njiani saa kumi na moja nakutana na watoto wa dogo wa Aidha Nursery au La Kwanza wako njiani na mabegi.
Nilisikitika sana kwani hata mimi na utu uzima wangu kuamka usiku ni mbinde kwa sababu tu ya shida.
Kama mtoto saa kumi na moja yuko barabarani je huyu kaamka saa ngapi?
Je tunajali kwamba watoto lazima wapate haki yao ya Utoto? Wacheze, walale muda wa kutosha, wajifunze lugha na tabia za jamii yao na kupumzika?
After all umempeleka mtoto Kwenye hiyo Nursury yako je akimaliza anapata nini? Kunq faida kubwa kiasi gani mpaka ku jeorpadize haki ya mtoto?