English Medium mnawachosha watoto wetu.

Ki ukweli kabisa kwa wanaojua biolojia na psycholojia ya watoto watakubaliana namimi hii haiko sawa...sisi wazazi tunamatakwa yetu juu ya watoto wetu.

Yaani Mzazi anadictate nini mtoto aweze ku achieve bila kujia madhara na mzigo kwa mtoto.

Juzi natoka Kinondoni nasindikiza Mgeni wangu anayesafiri na Basi la Esta linampitia njiani saa kumi na moja nakutana na watoto wa dogo wa Aidha Nursery au La Kwanza wako njiani na mabegi.

Nilisikitika sana kwani hata mimi na utu uzima wangu kuamka usiku ni mbinde kwa sababu tu ya shida.

Kama mtoto saa kumi na moja yuko barabarani je huyu kaamka saa ngapi?

Je tunajali kwamba watoto lazima wapate haki yao ya Utoto? Wacheze, walale muda wa kutosha, wajifunze lugha na tabia za jamii yao na kupumzika?

After all umempeleka mtoto Kwenye hiyo Nursury yako je akimaliza anapata nini? Kunq faida kubwa kiasi gani mpaka ku jeorpadize haki ya mtoto?
 
Changamoto ilioko hapo ni shule kutokuwa na usafiri wakutosha unakuta usafiri mmoja unachukua watoto mitaa zaidi ya 20 hapo unategemea dereva aamke saangapi paka anakuja kumaliza mtaa wa mwisho ni saa ngapi na shule anaingia saa ngapi na masomo yanaanza saa ngapi. Mamlaka husika kabla ijaipa kibali shule iangalie idadi ya usafiri ili kuepusha hii kero mtt hapati muda wa kutosha wa kupumzika kwa kweli anatoka amechelewa na kurudi anachelewa vilevile
 
Tunafeli sana! Tunawachosha watoto kabla ya kuwa watu wazma
Hizo shule zenyewe sasa hata akimaliza hakuna anachojua zaidi ya English.

English nayo ambayo haina makubwa/maajabu sana kwenye maisha yao.

Wazazi tunajifurahisha kupitia mateso ya watoto. Unajisikia raha kuona Mwanao anaonge Ngeli.
 
Nadhani wazazi ndio mnachagua kutesa watoto. Dudu liumalo halipewi kidole, ninyi mbona mnawapa shule za namna hiyo watoto.
 
Yani sahv shule kibao tena karibu na makazi,kumpeleka mtoto wa nursery au shule ya msingi private shule ambayo ni mbali na makazi yako na inabidi aamke saa 10 huko,huo ni uzembe wa mzazi, dogo anaamka saa 1 na 1 na nusu yupo shule
Kila mtu ana mapenzi yake na namna ya kulea watoto.

Nilipiga Stop kupeleka mtoto Boarding hadi aanze Sekondari sijali watu wanasemaje. Kwanza nalinda Uchumi wa mtoto hapo baadae.

Siwezi kumsomesha shule ya mamilioni kwa hela hizi hizi na uchumi wa tozo.

Wenye nazo wawapeleke watoto wao wanapotaka mimi nawekeza akimaliza awe na pakukimbilia.

Nimesoma na nimejifunza mengi kwenye haya maisha ya Elimu.
 
Mzazi analipa nauli ili mtoto akae kwenye kiti au asafirishwe kwa hali yoyote ile mradi afike shule??
Usalama ni jambo muhimu sana! Mtoto anaamka asubuhi na kulala tena! Sidhani kama ni jambo jema!
 
Tusiruhusu watoto wetu wapitie mitihani migumu ambayo tumepitia sisi!
 
Mpeleke mwanao St kayumba acha hizi siasa
 
Tusiruhusu watoto wetu wapitie mitihani migumu ambayo tumepitia sisi!
Kutafuta Elimu na kuhaso ni mtihani mgumu? Dont be negative....... That was learning and not torturing.

Kuna watu wana madeni wanashindia mchicha na mihogo ukimuuliza kwanini anakwambia eti anasomesha😅😅
 
Kutafuta Elimu na kuhaso ni mtihani mgumu? Dont be negative....... That was learning and not torturing.

Kuna watu wana madeni wanashindia mchicha na mihogo ukimuuliza kwanini anakwambia eti anasomesha😅😅
Hapa ila tujitahidi mtoto asione kama amekuja kuteseka! Kuna watu wengi wana maisha mazuri sana ila wanavyowalea watoto wao ni kipuuzi sana! Sina maana kwanza ni vibaya mtoto kuona na kusihi kwenye ugumu ila isiwe kwenye dhana ya kukomoa!
 
Hapa ila tujitahidi mtoto asione kama amekuja kuteseka! Kuna watu wengi wana maisha mazuri sana ila wanavyowalea watoto wao ni kipuuzi sana! Sina maana kwanza ni vibaya mtoto kuona na kusihi kwenye ugumu ila isiwe kwenye dhana ya kukomoa!
We mlee kwa uwezo wako. Usije ukafa njaa bure kwa kujikamua vitu ambavyo huna. mwisho wa siku utaishia kwa kiboko ya Wachawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…