ENOKO: Duniani mpaka mbingu ya 10

ENOKO: Duniani mpaka mbingu ya 10

Cha kushangaza unaambiwa shetani hapo mwanzo alikuwa malaika.
Alipo hasi akatupwa mbali MUNGU, kwa maelezo mengi sheni ni mweusi Sasa sijui alibadilika rangi na muonekano baada ya kumkosea Mungu?!!
Vitabu vya dini vina mambo mengi sana ya kuhojiwa. Ni Kama hadithi za kutunga (myth).
Na kwanini awe mweusi hii dharau, kwamba sisi weusi ndio mashetani? 🤣🤣🤣
 
SEHEMU YA 02

Enoko anaendelea kusema kwamba malaika wale wawili wakamchukua na kumpeleka kwenye mbingu ya pili na huko akakutana na haya mambo.

Kwanza kulikuwa na giza kubwa, giza ambalo duniani hakuna lakini pia akawaona malaika wakiwa wamening’inizwa kwa staili ya kunyongwa, kufungwa na minyororo huku wakitazamwa na wengine waliokuwa wamesimama.

Hapa ngoja nikwambie kitu kimoja. Hao malaika hawakuwa kama hawa tunaowasoma sehemu mbalimbali, hawa ni malaika ambao kwa kuwaangalia walionekana kuchoka sana, weusi, na muda wote walikuwa wakilia machozi meusi tii, na wanalia kila dakika. Yaani pamoja na kunyongwa huko, hawakuwa wamekufa.

Enoko akauliza hawa ni akina nani? Akajibiwa kwamba ni baadhi ya wale malaika waliotaka kupambana na Mungu, wamechukuliwa na kuning’inizwa hapo wakisubiri hukumu siku ya mwisho.

Okay! Sasa hapa mimi kama Nyemo najiuliza kitu. Hawa malaika wataonekana tena mbingu ya tano, na wengine watatu walishushwa duniani. Swali ninalojiuliza ni moja. Kwa nini Mungu aliamua wengine kuwaacha mbinguni wakiteseka na wengine kuwashusha duniani? Ngoja tuendelee kwanza.

Wengine walikuwa wakimwambia Enoko: “Mtu wa Mungu, tuombee kwa Mungu atusamehe!”

Enoko akawa anawajibu: “Mimi ni nani mpaka niwaombee? Ni binadamu, nisiyekuwa na lolote lile. Kama nikiwaombea ninyi, nani ataniombea mimi?”

Baada ya hapo malaika hao wakamchukua na kumpeleka mbingu ya tatu. Huko akakutana na sehemu iliyotawaliwa na miti mingi mizuri iliyokuwa inamea matunda mazuri, ni kama bustani kubwa sana. Ilipendeza machoni mwake, ilikuwa ni sehemu ambayo ilimvutia kila alipokuwa akiiangalia.

Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na mti mkubwa wa uhai, ni kama ule ambao uliwekwa kwenye bustani ya Eden ambapo kama Adam na Hawa wangekula hakika wasingekufa.

Mti huo ulikuwa na muonekano wa tofauti na miti yetu ya duniani. Ulikuwa kama umetengenezwa kwa mafuta yanayoteleza lakini pia ulionekana kuwa na muonekano wa dhahabu.

Mti huo ulikuwa na uwezo wa kuotesha kila aina ya tunda unalolijua wewe na usilolijua katika maisha yako. Pia katika bustani hiyo kulikuwa na mito, si ya maji, bali ilikuwa ni ya asali na maziwa.

Na pia kulikuwa na mingine ambayo ilikuwa inatiririsha mafuta na mvinyo (wine). Ukiachana na hiyo, pia kulikuwa na malaika mia tatu ambao walikuwa wanaitunza bustani hiyo kubwa huku wakiimba kila wakati.

Kwa namna walivyokuwa wakiimba, Enoko anasema hakuwahi kuona ama kusikia mtu duniani akiimba kama hivyo.

Hiyo ndiyo sehemu ambayo watakatifu watakwenda na kuishi. Yaani kama wewe unatenda mema duniani, utakwenda kuishi kwenye bustani hiyo milele na milele.

Baada ya hapo, malaika wale wakamchukua na kumpeleka upande wa Kaskazini mwa mbingu ile ya tatu. Sasa huko ndipo wale wasiokuwa watakatifu walipokuwa wanahifadhiwa, ndipo jehanamu ilipo.

Enoko anasema alipopelekwa huko, aliogopa kwa kuwa ilionekana kuwa sehemu iliyojaa mateso makubwa ambayo hakuwahi kuyaona. Mwanga pekee uliokuwa ukipatikana ni wa moto ambao ulikuwa unaunguza kila kilicho humo.

Pia kulikuwa na mto, huu haukuwa wa maji bali mto wa moto. Kulikuwa na moto kila kona. Ila mbali na moto huo, pia kulikuwa na barafu kila sehemu. Yaani kulikuwa na mateso ya aina mbili ambayo watu walikuwa wakiyapata. Ya kuunguzwa sana na moto lakini pia ya kupigwa na baridi kali kiasi cha kuganda kabisa.

Moto haukuwa ukiyeyusha barafu zile, watu walipigwa na vitu vyote hivyo viwili kwa wakati mmoja. Watu walikuwa wakilia kwa majuto lakini pia walilia kwa sababu ya kiu kali waliyokuwanayo.

Pia kulikuwa na malaika asiyekuwa na huruma hata kidogo, aliyeogopwa, mwenye hasira na alishika silaha kubwa kwa ajili ya kuwatesea watu.

Enoko akasema: “Hii sehemu imejaa mateso makubwa mno” na malaika akamwambia: “Hii ni sehemu ya watu waliotenda maovu duniani, watu ambao hawakumuheshimu Mungu sehemu ya wachawi, waovu, wabakaji, wala rushwa, matapeli na wengineo.”

Baada ya kuyaona hayo yote, malaika wale wakanichukua na kunipeleka mbingu ya nne.

Itaendelea kesho.
 
Na sehemu inayounguza yenye moto mkali na muda huo huo kuna barafu kali.!! 🙄
Sasa barafu si inayeyuka sababu ya moto??!
Jamani hivi vitabu vina mauongo mengi.
Au Enoko alikuwa kwenye njozi?
 
Elia ,Enoko,jesus,Musa,Ibrahim,Noah wote ni fictional charachters kama tu spider man,tom and jerry,kibanga aliyempiga mkolini,pazi na jogoo unaweza kuongezea
Bila kumsahau super man na Batman
 
Back
Top Bottom