Katika Agano la Kale la Biblia, makanisa kama tunavyoyaelewa leo hayakuwepo kama taasisi ya kidini. Makanisa, kama vile yanavyoonekana katika muktadha wa Kikristo, yalianza baada ya Yesu Kristo, hasa katika Agano Jipya.
Hata hivyo, katika Agano la Kale, kulikuwa na manabii walioitwa na Mungu kutoa ujumbe wake kwa watu wa Israeli. Hawa manabii hawakuanzisha makanisa, bali walikuwa wanahubiri na kutangaza ujumbe wa Mungu kwa jamii ya watu wa Israeli. Walitumwa kurekebisha, kuonya, na kuelekeza watu kwa njia ya haki...
Kwa maandiko haya, hao manabii wa sasa ni matapeli...
Swala la hao ni matapeli Hilo ni lakwako Mimi nmekupa elimu juu ya nabii ni Nan na anatakiwa kuwaje? Lakini pia uwezo wakujua nabii Gani ni mkweli na nani tapeli linategemea wewe binafsi na mahusiano yako na Mungu full stop.
Lakini pia soma Biblia usiandike tu utakuwa huelew hata unachokiandika.
Aliyekwambia katika agano la kale hakukuwa na makanisa nani ? Au Biblia ipi hiyo unayitumia wewe
unafahamu kama hekalu ndio kanisa Kwa kiswahili Cha kisasa?
Na unafahamu kama kuhani ndio Mchungaji ?
Agano lakale linatambua uwepo wa kuhani na uwepo wa nabii na majukumu yao ni tofaut kasome Biblia Tena usitake kubishana Hali yakuwa huna contents za kutosha
Na nimalize Kwa kukwambia tu huo mfumo wa Ibada unaouona watu wanaingia kanisan wanaimba halaf Mchungaji anasimama na kusoma neno ndio huohuo hata kweny agano la kale ulikuwepo ,
Walawi walifanya mambo yote hukusu kumsifu Mungu Kwa kumwimbia na makuhani walifanya majukumu yao kma wafanyavyo wachungaji na manabii walikuwa na majukumu yao kama waonaji wa habari za Sirini.
Mfano mdgo kwenye agano la kale Kuna mtu alikuwa anaitwa Eli huyu ni kuhani lakini Kuna mtu alikuwa anaitwa Samwel huyu ni nabii na, na huyo Samwel alilelewa katika Mikono ya Eli ambaye ni kuhani Kwa lugha nyingn alikuw chini ya uchungaji.
Usiwe mvivu wa kusoma kasome kitabu japo Cha Samweli tu utaona Vingi kuhus hizi habar tunazojadiri. Na utajua hata sadaka pia zilikuwa zinakwenda Kwa nabii au kuhani hahahahahah
unapoambiwa hakuna jipya chini ya jua uwe unaelewa maana yake ni nini.
Umeleta Uzi halafu hujui hata ulichokiandika kinatoka wap kabla ya kuandika Uzi humu muwe mnapitia notes kwanza vzr JF sio FB ndio maana unaona Kuna had majukwaa mbalimbali