Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Mkuu nguvu za kishirikina si zinaendana na shetani? Kama ndio kwanini sijawahi sikia hao unaodai wana nguvu za kishirikina wakitumia jina shetani na wanaendelea kutumia yesu?

Embu tudadavulie?

• UShetan ni pale tu mtu anakuambia anakupenda wakati hakupendi 😄, Tukiachana na hayo.

• Jina "Lesu" linaweza kuwa mchanganyiko au kubadilishwa kutoka kwa neno "Yesu," ambalo ni jina la Kikristo linalorejelea Kristo. Hata hivyo, mabadiliko ya majina yanaweza kutumika kwa njia ya :-


1 • Kupotosha na Kudanganya: Wanaweza kutumia majina hayo ili kutoa uwongo na kudanganya watu, wakitumaini kwamba kwa kutumia majina matakatifu, watu watawaamini.

2 • Kupata Umaarufu na Ufuasi: Kutumia majina ya kidini yanaweza kuwasaidia kupata umaarufu na ufuasi kutoka kwa watu wanaojitambulisha na dini fulani.

3 • Kuundwa kwa Ushirika wa Uongo: Wanaweza kutumia majina matakatifu kujaribu kujenga jukwaa la kidini la uongo kwa kushirikisha watu katika mafundisho yasiyo sahihi.
 
Asante sana mkuu, Kwa mchango wako mzuri ✍️✍️.
 
Kupotosha na Kudanganya: Wanaweza kutumia majina hayo ili kutoa uwongo na kudanganya watu, wakitumaini kwamba kwa kutumia majina matakatifu, watu watawaamini.
Tujikite hapa.
Unaamini jina la yesu ni takatifu(NURU). Tunafahamu palipo mwanga hapawezi kuwa na giza.
swali, inawezekana vipi mtu akawa anatumia nguvu za kishirikina (Giza) akatumia jina la yesu(NURU)?

Huoni kwamba hili jina la NURU linakuwa halina kazi katika scenario hiyo? Maana ni takatifu lakini behind the scene ni giza?
Inawezekana vipi vifanye kazi pamoja?
 
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Kuamini unaamini tu, hata uongo unaweza kuamini.

Mimi natafuta ukweli uko wapi.

Hizo habari za Mungu wa vitabuni, na huyo wa mizimu, zote ni hadithi za uongo tu.

Nina imani mda wako hautoshi wa kumjua mungu, inaelezwa kwamba mitume walikuwa karibu na Yesu wakati wa huduma yake duniani, wakishuhudia miujiza, kusikia mafundisho yake, na kushiriki katika huduma yake. Lakini hawakufanikiwa kumjua mungu vilivyo. Na baadhi yao walipokea mafunuo maalum kutoka kwa Roho Mtakatifu baada ya Pentekoste.
 
Hivi vitabu mnavyoviita vitakatifu vinathibitisha vipi Mungu yupo?

Inakuaje ni vitabu vya Mungu kweli na sio hadithi za kutungwa na watu tu?
Mambo ambayo yanaweza thibitisha kuwa ni vitabu vya mungu :-
• Mafundisho: Ujumbe wa Biblia na mafundisho yake, kama vile maadili, amri za Mungu, na maelezo ya historia ya kidini, unaweza kuifanya ionekane kama kitabu takatifu.

• Historia na Utamaduni: Katika jamii nyingine, Biblia inaweza kuonekana kuwa takatifu kutokana na umuhimu wake wa kihistoria na kiutamaduni, hata kama haichukuliwi kama Neno la Mungu.

• Uthibitisho wa Kiroho: Baadhi ya watu wanaweza kusema kwamba wamepata uzoefu wa kiroho na maelezo yanayopatikana katika Biblia, na hivyo kuiona kama kitabu takatifu kwao
 
Manabii wasioweza kuona kinachotokea Kesho Kwa Nchi Si Nabii. Wangekuwepo wangeona COVID-19, wangeona Vita ya Ukraine,Urusi, Gaza. Tope la Hanang na Vifo vya Wakubwa.
Kwa hiyo hawa wa kizazi kipya, ni wapigaji tu na waliofungamana na ibirisi??
 
Wewe Mungu wako kwa Nini asikutokee wewe akuambie anachotaka mpaka amtokee mtu chumbani kwake ndo umwamini yeye...shtuka bro
 
Mtu anabinywa tumbo kama anakanda chapati..utaacha kutapika dagaa kweli?.ila kwny screen wanaonyesha kono kono...hahahah
 
Mungu mara nyingine anaelezewa kama mwenye huruma na upendo, lakini pia kama mwenye haki na uadilifu. Ikiwa Mungu ni mwenye haki, inaweza kumaanisha kwamba anaweza kuwa na utaratibu wa adhabu kwa vitendo vinavyokiuka maadili na misingi yake.

Hata hivyo, njia za adhabu au mawasiliano ya Mungu na mwanadamu zinaweza kutofautiana kulingana na imani na mitazamo. Mara nyingine, adhabu inaweza kueleweka kama mchakato wa kurekebisha au kutoa fursa ya kutubu na kurekebisha mwenendo.
 
Najaribu kufikiria kama umeelewa.
Umeelewa swali?
 
Kumuaminisha mtu kuwa kuna Mungu halafu yeye na misingi yake hairuhusu kuamini kuhusu Mungu ni jambo gumu sana tena sana ....ni Bora ubaki na unacho kiamini kaka
Hapana sehemu aliyosema anahitaji kuamini, umesoma vizuri comment yake?

Amekuambia thibitisha na si kuamini.
 
Wewe Mungu wako kwa Nini asikutokee wewe akuambie anachotaka mpaka amtokee mtu chumbani kwake ndo umwamini yeye...shtuka bro
Mipango ya Mungu, Katika imani nyingi, kuwa manabii wa zamani walihusishwa na mpango wa Mungu na sio uchaguzi wa kibinadamu. Ni wachache wanaitwa kwa kazi hii kulingana na mpango wa Mungu...

Lakini hawa manabii wa sasa, nina mashaka nao, Maana hawaendani na uhalisia wa zamani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…