Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Enyi Manabii wa kizazi kipya ni kweli mmepewa nguvu na Mwenyezi Mungu, au ni ushirikina tu?

Kama hawamo kwenye kitabu kitakatifu basi hao sio manabii watokanao na kitabu kile yawezekana wanavyo vitabu vyao.
Nabii unasema eeeti 1988 ulionana na Yesu Mara sijui una namba zake za WhatsApp.
Wizi mtupu
Hili swali nime jiuliza sana Nabii hatambuliki kwenye vitabu vya dini
 
Wewe unaamini upande upi mkuu...?? Mungu, mizimu Au huamini chochote kile. πŸ€”πŸ€”
Sitaki kuamini, nataka kujua.

Kuamini unaamini tu, hata uongo unaweza kuamini.

Mimi natafuta ukweli uko wapi.

Hizo habari za Mungu wa vitabuni, na huyo wa mizimu, zote ni hadithi za uongo tu.
 
Manabii wa uongo wapo na wa kweli wapo...

Kazi ipo kwako wewe ambaye unaongozwa na mwili na kukariri neno bila kulifanyia kazi...

Wanaoongozwa na Roho Mtakatifu wanajua Nabii wa kweli na wa uongo...
Mtu utajuaje kuwa unaroho mtakatifu?

Au

Wewe mwenye roho mtakatifu unaweza nitafautishia kati ya nabii mwamposa na yakobo?
 
Hakuna nabii yoyote wala mtume yeyote wakizazi hiki wakweli wote wachumia tumbo tu au kujipa vyeo vya kuaminika ila ki uhalisia hakunam

Hakuna nabii yoyote wala mtume yeyote wakizazi hiki wakweli wote wachumia tumbo tu au kujipa vyeo vya kuaminika ila ki uhalisia hakuna.
Kwani manabii wa kizazi cha zamani walikuwa na nini cha muhimu kuliko wa kizazi cha sasa?
 
Hiyo inadhihirisha watu wanaishi karne ya 21 lakini akili zao zinatumia software za dark ages. Ongezeko la manabii na watu kutapeliwa kwa neno la mungu, ni dhahiri mungu huyo hayupo,angekuwepo asingeruhusu huo ujinga uwepo hata kwa bahati mbaya.

β€’ Mkuu mungu yupo, ukipitia pitia baadhi ya vitabu, Biblia : Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinachojumuisha Agano la Kale na Agano Jipya.

β€’ Qur'an : Kitabu kitakatifu cha Uislamu.

β€’ Vedas : Maandiko matakatifu ya Uhindu, ambayo ni pamoja na Rigveda, Samaveda, Yajurveda, na Atharvaveda.

β€’ Tanakh : Maandiko matakatifu ya Uyahudi, ambayo ni pamoja na Torati, Nabi, na Maandiko

β€’ Mojawapo ya mistari inayojulikana ni mwanzo wa Biblia, katika Kitabu cha Mwanzo, sura ya 1, ambapo inaanza na maneno "Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi."

β€’ Pia, Yesu Kristo katika Agano Jipya anazungumza mara kwa mara kuhusu Baba yake wa mbinguni na kutoa mafundisho kuhusu ufalme wa Mungu.

β€’ Hata ukiangalia jaribio la Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Wanajaribiwa kutii amri ya Mungu ya kutokula tunda fulani, lakini wanashindwa na kutokea madhara.

β€’ Katika Agano Jipya, Yesu mwenyewe anapitia majaribu. Mathayo 4:1-11 na Luka 4:1-13 zinatoa maelezo ya majaribu ambayo Yesu alikutana nayo jangwani baada ya kufunga kwa siku 40. Katika kila jaribio, Yesu anapinga majaribu ya Shetani kwa kutumia Maandiko.
 
Wanajiona wao wana atima ya maisha ya watu kumbe mwenye hatima ya maisha mtu ni mwenyezi mungu pekee
 
Ukiona mwanafunz anamuulza mwalimu swali huku akijifanya analeta lakini lakini nyingi ujue anajifanya anajua kwahyo unamuacha abaki na anachojua kwasab sio lazma sana nlichonacho uwe nacho na ulicho nacho niwe nacho.
Asante sana mkuu, Kwa mchango mzuri ✍️✍️✍️
 
β€’ Mkuu mungu yupo, ukipitia pitia baadhi ya vitabu, Biblia : Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinachojumuisha Agano la Kale na Agano Jipya.

β€’ Qur'an : Kitabu kitakatifu cha Uislamu.

β€’ Vedas : Maandiko matakatifu ya Uhindu, ambayo ni pamoja na Rigveda, Samaveda, Yajurveda, na Atharvaveda.

β€’ Tanakh : Maandiko matakatifu ya Uyahudi, ambayo ni pamoja na Torati, Nabi, na Maandiko

β€’ Mojawapo ya mistari inayojulikana ni mwanzo wa Biblia, katika Kitabu cha Mwanzo, sura ya 1, ambapo inaanza na maneno "Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi."

β€’ Pia, Yesu Kristo katika Agano Jipya anazungumza mara kwa mara kuhusu Baba yake wa mbinguni na kutoa mafundisho kuhusu ufalme wa Mungu.

β€’ Hata ukiangalia jaribio la Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni. Wanajaribiwa kutii amri ya Mungu ya kutokula tunda fulani, lakini wanashindwa na kutokea madhara.

β€’ Katika Agano Jipya, Yesu mwenyewe anapitia majaribu. Mathayo 4:1-11 na Luka 4:1-13 zinatoa maelezo ya majaribu ambayo Yesu alikutana nayo jangwani baada ya kufunga kwa siku 40. Katika kila jaribio, Yesu anapinga majaribu ya Shetani kwa kutumia Maandiko.
Hivi vitabu mnavyoviita vitakatifu vinathibitisha vipi Mungu yupo?

Inakuaje ni vitabu vya Mungu kweli na sio hadithi za kutungwa na watu tu?
 
KUNA WATU WANAJIFUNZA KWA KUSIKIA, WENGINE KWA KUONA(YAWATOKEE).
MUDA/WAKATI NI MWAMUZI MZURI.

EBU FIKIRIA
-UMEPELEKA KUCHA, NYWELE..
-UMEKULA KEKI, MAANDAZI YA UPAKO, UMEKUNYWA MAJI YA UPAKO, UMEPAKA MAFUTA YA UPAKO.....
-UMESUBIRI NDOA, KONTENA ZA CHINA, NYUMBA, GARI.......

NA BADO UCHUMI MBAYA, VYUMA VIMEKAZA, HUNA MATUMAINI YA SIKU ZIJAZO .
KITU UNACHO MILIKI NI MADENI TU!

KIBAYA ZAIDI HUNA SIFA YA KWENDA HUKO MBINGUNI.
Mboga ya shetani, hapo baadae πŸ€”πŸ€”
 
Manabii wasioweza kuona kinachotokea Kesho Kwa Nchi Si Nabii. Wangekuwepo wangeona COVID-19, wangeona Vita ya Ukraine,Urusi, Gaza. Tope la Hanang na Vifo vya Wakubwa.
 
Kwanini jibu lije nje ya muda ninaotaka mimi ili hali mungu ana uwezo wa kunijibu muda huohuo, na kwanini huyo mungu aombwe wakati anaijua shida yangu.

β€’ Muda wa Mungu: Mungu anaona wakati wote na anajua ni wakati gani wa kutoa majibu. Kwa hiyo, kuchelewesha kwaweza kuwa sehemu ya mpango wake usioeleweka vyema na binadamu.

β€’ Majaribio na Ukuaji: kuchelewesha kama njia ya kujaribu imani na uvumilivu, na hivyo kuwa fursa ya ukuaji wa kiroho na kujifunza.

Tukiangalia baadhi ya vitabu vya dini,
Isaya 55:8-9 (Neno: "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu, asema Bwana.")

Zaburi 40:1 (Neno: "Nalimngoja Bwana kwa saburi; akainama, akaisikia kilio changu.")

Zaburi 27:14 (Neno: "Ngoja kwa Bwana, uwe hodari, na moyo wako na uthibitike; naam, ngoja kwa Bwana."
 
Back
Top Bottom