Expensive life
JF-Expert Member
- May 2, 2020
- 2,971
- 9,437
Ndugu zangu, juzi nikiwa katika pita zangu mitaa ya Kariakoo, baada ya mizunguko kadhaa nikaona ngoja niingie moja ya maduka makubwa ya Bakhresa yanayouza vinywaji baridi ili nipoze koo kidogo.
Baada ya kuingia katika duka lile nilimkuta muhudumu mmoja hivyo nikamuomba anipatie kinywaji.
Ajabu akaniambia hatuuuzi vinywaji muda huu nikamjibu kwa nini? Akanijibu mwezi wa Ramadhani hatuuzi vinywaji mchana mpaka saa moja usiku.
Nikamuuliza sasa kama hamuuzi mmefungua kwa nini? Jamaa akaendelea kunijibu kwa ukali nimesema hatuuzi chochote muda huu.
Ndugu zangu Waislamu kama mnajua hamtoi huduma kwa kuwa mpo kwenye funga ni bora mkafunga kabisa ili tujue moja.