Enyi Viongozi: Kwa kutushurutisha mnatukosea sana, waajiri wenu ni sisi

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Haisaidii kuacha kuwaambia bayana. Kwa Hakika mmejisahau mno.

Kwamba mna agenda zisizokuwa na baraka zetu? Kwamba hata mna tozo mlizo asisi nyie, tusizoziafiki?

Kwingine mbona si hivyo?

IMG_20220819_141624_340.jpg

Nyie hata mnatuasa kwamba kama vipi hata Burundi nayo ni nchi?

Alisema Mwalimu: "Nchi siyo mashamba yenu." Mwisho wa kumnukuu.
 
Embu jaribu uwe unasoma pia ulichoandika kabla ya kukipost, kusudi ulekebishe makosa madogo madogo yatakayo fanya ueleweke una lenga Nini, lakini kwa kukusaidia Ni kwamba mh Rais anafanya kazi kubwa Sana na amekuwa mtumishi mwema kwa watanzania tangia aliposhika mamlaka na madaraka ya kuwa Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama

Mh Rais Ni msikivu na mnyenyekevu kwa watanzania maana anajuwa watanzania ndio mabosi, ndio maana unaona namna anavyokubalika kila Kona ya nchi kama namna alivyowekeza huduma za kijamii kila Kona ya nchi hii , zinazogusa kila mwananchi hasa mnyonge
 
Sina hakika kama umeelewa kilichomaanishwa hapo, Watanzania tuna appreciate kazi anayofanya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Watanzania ndiye tulimpa kazi kupitia kura zetu, hivyo hakuna ubaya kusema Mh. Rais kazi tuliyokupa unaifanya vizuri, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe ulinzi zaidi, ni uungwana kumshukuru mtu akikufanyia kazi nzuri.

Jiandae kuhesabiwa 23. 08. 2022

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Mbariki Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
 
Sisi sote ni watanzania na tunaishi humu nchini.Anayoyafanya mama tunayaona sote Wala hatuhitaji kuhadithiwa.Pamoja na hayo wananchi wanamalalamiko Yao hasa kulingana na hali ya kiuchumi na hizi tozo.Nadhani ni sahihi wakaeleza kile ambacho wanaona kina wapa shida huenda kikarekebishwa.Kumbuka mwananchi ndio mwajiri Wa viongozi.
 
Embu jaribu uwe unasoma pia ulichoandika kabla ya kukipost, kusudi ulekebishe makosa madogo madogo yatakayo fanya ueleweke una lenga Nini, lakini kwa kukusaidia Ni kwamba mh Rais anafanya kazi kubwa Sana na amekuwa mtumishi mwema kwa watanzania tangia aliposhika mamlaka na madaraka ya kuwa Rais na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama

Mh Rais Ni msikivu na mnyenyekevu kwa watanzania maana anajuwa watanzania ndio mabosi, ndio maana unaona namna anavyokubalika kila Kona ya nchi kama namna alivyowekeza huduma za kijamii kila Kona ya nchi hii , zinazogusa kila mwananchi hasa mnyonge
Ewe chawa mbobezi ulizingatia kweli unayo shauri hapa, au ni kutokokifahamu kiswahili vyema tu?

IMG_20220819_213724_214.jpg
 
Sisi sote ni watanzania na tunaishi humu nchini.Anayoyafanya mama tunayaona sote Wala hatuhitaji kuhadithiwa.Pamoja na hayo wananchi wanamalalamiko Yao hasa kulingana na hali ya kiuchumi na hizi tozo.Nadhani ni sahihi wakaeleza kile ambacho wanaona kina wapa shida huenda kikarekebishwa.Kumbuka mwananchi ndio mwajiri Wa viongozi.
Badala ya "ninyi watanzania" ungeandika "ninyi chawa wabobezi" ungeeleweka vyema zaidi mkuu.

Watanzania? Humo tumo n wengine ambao Hichilema tunamwelewa sana tu kwenye haki na kuwasikiliza wananchi wake.
 
Back
Top Bottom