Peponi hakuna Usiku wala mchana
Peponi hakuna Jua wala mwezi
Peponi hakuna siku,mwezi wala mwaka ni maisha ya milele tu.
Peponi hakuna kifo.
Ni maisha ya Raha ambayo jicho halijapata kuona,sikio halijapata kusikia wala akili haijapata kuwaza.
Mtu wa chini yule wa mwisho kabisa atapewa mara kumi ya ufalme wa wafalme wa dunia hii.
Kuhusu wanawake wala usishtuke kwasababu Mungu ameumba wanawake wa peponi wanaitwa (Hur al ayn) ni wazuri jicho halijapata kuona na pia wanawake wa ulimwengu huu ambao watafuzu kuingia peponi watakuwa warembo sana zaidi ya hata hao Hur al ayni. Watakutanishwa na waume zao ambao nao watakuwa wamefuzu kuingia peponi .
Mwanaume mmoja wa peponi atakuwa na nguvu sawa na wanaume mia moja wa ulimwengu huu. Hivyo kuwatimizia haki wake zake huko peponi haitakuwa jambo gumu hata kidogo.
Karibu katika Uislam ili usalimike na adhabu kali za moto wa Jahannam