Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,351
- 9,855
Nawasalimia wana jukwaa la Great Thinkers!
Kuna usemi unasema siku hizi ogopa Mungu na Technolojia. Hii imekuja kuwaumbua watu wengi sana ambao walisema mambo tofauti na mambo ambayo walikuja kuyaishi baadae. Dk. Bashiru Ally alikuwa muumini mkubwa sana wa katiba mpya na alipinga kwa nguvu kubwa uroho wa madaraka wa wanasiasa, akisisitiza kuwa Katiba ni takwa la nyakati kwaajili ya ustawi wa nchi. Lakin siku zilivyoenda alivyokuja kuonja utamu wa madaraka alibadilika kabisa. Hali hii sasa tunaenda kuiona kwa Mama Samia Suluhu.
Mikutano yake ya mwanzo baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa kila akihutubia "ulimi unateleza" na anatamka neno katiba mpya na akakiri kuwa lipo kichwani pake hasa. Lakin baada ya miezi mitatu ya kushikilia madaraka, ameshaanza kusema kipaumbele chake ni uchumi na katiba mpya itasubiri, mpaka lini hatujui.
Ninachoona hapa kilichompata Dk. Bashiru kabla hajayaonja madaraka ndicho kinachompata Rais Samia Suluhu baada ya kukamatia madaraka.
Hapa ni kabla hajaonja na madaraka.
Na hapa ni baada ya "kuula".