Enzi za Dkt. Bashiru kabla hajaonja ladha ya Madaraka

Enzi za Dkt. Bashiru kabla hajaonja ladha ya Madaraka

🤣 🤣 🤣 🤣 kabisa. Madaraka huwa yana corrupt akili za wasomi wetu.
Aisee kweli. Hapa alikuwa na akili zake timamu. Ila sasa hivi nina uhakika atakuwa amesharejewa tena na akili hii ya kuona umuhimu wa katiba mpya. Mama Samia naye na kina Kikwete, Zitto, Riziwani juzi juzi Magufuli alipokuwa ameshika hatamu nasikia walikuwa wanalia kichini chini mno kuwa yalifanyika makosa ya kutobadili katiba, lakini sasa hivi akili zimeshapeperuka tena wanasema tuwape muda.
 
😆😆kwan mkuu kuna jambo mhe.katibu mkuu kakufanyia ?
 
Nawasalimia wana jukwaa la Great Thinkers!

Kuna usemi unasema siku hizi ogopa Mungu na Technolojia. Hii imekuja kuwaumbua watu wengi sana ambao walisema mambo tofauti na mambo ambayo walikuja kuyaishi baadae. Dk. Bashiru Ally alikuwa muumini mkubwa sana wa katiba mpya na alipinga kwa nguvu kubwa uroho wa madaraka wa wanasiasa, akisisitiza kuwa Katiba ni takwa la nyakati kwaajili ya ustawi wa nchi. Lakin siku zilivyoenda alivyokuja kuonja utamu wa madaraka alibadilika kabisa. Hali hii sasa tunaenda kuiona kwa Mama Samia Suluhu.

Mikutano yake ya mwanzo baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa kila akihutubia "ulimi unateleza" na anatamka neno katiba mpya na akakiri kuwa lipo kichwani pake hasa. Lakin baada ya miezi mitatu ya kushikilia madaraka, ameshaanza kusema kipaumbele chake ni uchumi na katiba mpya itasubiri, mpaka lini hatujui.

Ninachoona hapa kilichompata Dk. Bashiru kabla hajayaonja madaraka ndicho kinachompata Rais Samia Suluhu baada ya kukamatia madaraka.

View attachment 1835474
Hapa ni kabla hajaonja na madaraka.

View attachment 1835502
Na hapa ni baada ya "kuula".
Kwa kweli Bashiru namvulia kofia. Hoja aliyojenga hapa ni kali mno, na itaendelea kuwa kali hata kama huyo aliyeijenga atafika mahali "akajingishwa" na kuwa MJINGA wa kupitiliza, kama ambavyo Bashiru wa siku hizi anajenga hoja kutoka tumboni, yaani kwa maslahi ya tumbo lake.
Hii hoja ya Bashiru ya umuhimu wa Katiba mpya, inatoa jibu zuri hata kwa wale wanaodai kwamba Hoja ya Katiba Mpya ni hoja ya CHADEMA.
Nawashauri wamsikilize vizuri Bashiru wa zamani, ana majibu mazuri, Comprehensive, Conclusive and Complete.
 
Nawasalimia wana jukwaa la Great Thinkers!

Kuna usemi unasema siku hizi ogopa Mungu na Technolojia. Hii imekuja kuwaumbua watu wengi sana ambao walisema mambo tofauti na mambo ambayo walikuja kuyaishi baadae. Dk. Bashiru Ally alikuwa muumini mkubwa sana wa katiba mpya na alipinga kwa nguvu kubwa uroho wa madaraka wa wanasiasa, akisisitiza kuwa Katiba ni takwa la nyakati kwaajili ya ustawi wa nchi. Lakin siku zilivyoenda alivyokuja kuonja utamu wa madaraka alibadilika kabisa. Hali hii sasa tunaenda kuiona kwa Mama Samia Suluhu.

Mikutano yake ya mwanzo baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa kila akihutubia "ulimi unateleza" na anatamka neno katiba mpya na akakiri kuwa lipo kichwani pake hasa. Lakin baada ya miezi mitatu ya kushikilia madaraka, ameshaanza kusema kipaumbele chake ni uchumi na katiba mpya itasubiri, mpaka lini hatujui.

Ninachoona hapa kilichompata Dk. Bashiru kabla hajayaonja madaraka ndicho kinachompata Rais Samia Suluhu baada ya kukamatia madaraka.

View attachment 1835474
Hapa ni kabla hajaonja na madaraka.

View attachment 1835502
Na hapa ni baada ya "kuula".
Enzi za Bashiru akiwa na akili.
 
Bashiru alipokuwa UDSM na mwanachama wa CUF alikuwa bingwa wa kuongea masuala ya haki, demokrasia, usawa na Utawala bora.

Alipoletwa CCM na Binamu yake Mrundi mwenzie Magufuli akawa ndiye ana ratibu dhuluma dhidi ya upinzani. Ameshiriki kuwanunua akina Gekul, Silinde na Patrobas. Ameshiriki kuiba uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020. Na aliwahi kunukuliwa akisema "Tutatumia dola kubaki madarakani"

Huyu mrundi ndiye ambaye Magufuli alikuwa anamuandaa kupokea U-RAIS wa Tanzania baaada ya mwenyewe kutosheka. Ila Mungu wetu ana maguvu, kasema HAPANA.
Hivi kuitwa mtu Murundi na hali siyo Murundi unapata burudani gani? Au ni njia nyingine ya udhalilishaji? Je! Nchi ya Burundi unaidharau? Kwa nini hukusema ni Mughana, Mutswana, MuSudani?
Kama ulikasirishwa na vitendo vyake ulivyovitaja je unamuadhibu kwa kumuita Murundi! Je urundi ni adhabu?
Maana ukianza kubagua mtu haijarishi unasemaje, kwa mfano - wewe si ni Mchaga? Lakini nikisema hawa wachaga eti ndio wanataka kuingia madarakani na kututawala! Hiyo statement utaichukia, hasa kama wewe siyo mchaga! japo kuwa unataka kufanya hivyo (kututawala). Be mature.
 
Warundi na Wanyarwanda wana DNA ya kuchukiana na kuuana. Kamwe nchi yetu isijichanganye na hiyo laana. Angalia Mwendazake alikokuwa anatupeleka.
 
ungeweka kipindi kizima ,si huu mtindo uliotumia wa kuleta kipande ili mpate sehemu ya kumtukania,si sawa,imani yangu kuna mengi ya msingi kaongea
Hiyo clip kamili ukiitafuta YouTube ipo, ni kipindi cha nusu saa. Anayoongea huko kwingine ni hayohayo. Mtoa mada amelenga hasa alichosema Bashiru kuhusu Katiba Mpya. Binafsi niliipenda sana hoja yake kali sana. Kwamba:
"Medani ya kujenga muafaka wa kitaifa kabla ya 1992, ilikuwa chama kimoja, baada ya 1992, Medani ya kujenga muafaka wa kitaifa, ni KATIBA MPYA".
So Beautifully stated!
Yaani wana ccm wanaowashambulia CHADEMA , au akina Shaka pamoja na Palamagamba, wanaodai katiba ya sasa imefanya "mengi mazuri", kwa hiyo iendelee tu, wanahitaji kumsikiliza Bashiru hapa. Hata Mwenyekiti wa ccm, mama Samia, anahitajika kumsikiliza Bashiru
 
Hivi kuitwa mtu Murundi na hali siyo Murundi unapata burudani gani? Au ni njia nyingine ya udhalilishaji? Je! Nchi ya Burundi unaidharau? Kwa nini hukusema ni Mughana, Mutswana, MuSudani?
Kama ulikasirishwa na vitendo vyake ulivyovitaja je unamuadhibu kwa kumuita Murundi! Je urundi ni adhabu?
Maana ukianza kubagua mtu haijarishi unasemaje, kwa mfano - wewe si ni Mchaga? Lakini nikisema hawa wachaga eti ndio wanataka kuingia madarakani na kututawala! Hiyo statement utaichukia, hasa kama wewe siyo mchaga! japo kuwa unataka kufanya hivyo (kututawala). Be mature.
Hii habari ya fulani mrundi, fulani mtusi, fulani si mtanzania, ilianzia kwa Rais Mkapa. Baada ya kukosa hoja za kumjibu Jenerali Ulimwengu enzi hizo, alipoanza kuikosoa serikali ya Mkapa, baada ya kumpigia kampeni kali kupitia Rai ya Jenerali katika gazeti la Rai enzi hizo, Serikali ya Mkapa ikamtangaza Jenerali kwamba si raia. Alikuwa na cheo fulani Baraza la Michezo, na vingine vya heshima, vyote vikapukutika.
Baada ya hapo, serikali za ccm zilizofuatia zilipenda sana kutumia risasi ya URAIA kuwacharaza wale ambao walikuwa mwiba kwa serikali, hasa kama wanatoka mikoa ya pembezoni.

Magufuli naye hakusita kuitumia vilivyo. Yeye alikwenda mbali zaidi: akina Askofu Kakobe, Askofu NiweMugizi, na padre Sabas (marehemu sasa), wote walipata janga la kunyang'anywa paspoti. Hivyo ukiwazidi hoja tu, wewe ni mrundi.

Kumuita Magufuli mrundi (= siyo raia) wala haishangazi, maana mwenyewe alipenda kuwaita hivyo wale asiowapenda. Waingereza wanaita giving somebody a taste of his own medicine.

Na utaona serikali zooote za ccm hasa baada ya Nyerere, zinapenda mambo ya mkato. Mfano badala ya kujihangaisha na kuwatoza kodi wenye nyumba za kupangisha, serikali inakuja na tozo za miamala na kodi ya umeme. Ndiyo, ni kodi ya umeme sababu hata kama huna jengo, mradi unatumia umeme, utailipa. Serikali zote za ccm zinapenda mteremko. Kutoza kodi ya umeme na tozo za miamala ni rahisi sana kukusanya pesa yake.
 
na wale form six wliopata zero kama mbowe nao sijui akili zao zinaharibika na nini?
Mbowe ni msomi, anajua kujenga hoja, hadi anawatisha wasomi wooote waccm na serikali, wanaogopa kiasi kwamba wanaamua "kumnyamazisha" kwa kumtandika kesi la ugaidi lisilo na dhamana. Mpaka lifutwe, atakuwa kakaa gerezani sio chini ya mwaka.

Lakini wasichojua ccm ni kwamba jinsi Mbowe anavyozidi kukaa gerezani, ndivyo atazidi kuwa kaa la moto. Itafika mahali watalazimika kumtema, tena kwa aibu.
Ndio ile habari ya NJOMBA, UCHIMUNG'UNYE, UCHIMEJE, UCHITEME. UKITEMA NCHALE. UKIMEJA NCHALE. UKIMUNG'UNYA NCHALE. Kazi ipo.
 
No integrity in most of our politicians! Labda Warioba na Lissu tu!! Ambao watasema ukweli daima!!
 
Warundi na Wanyarwanda wana DNA ya kuchukiana na kuuana. Kamwe nchi yetu isijichanganye na hiyo laana. Angalia Mwendazake alikokuwa anatupeleka.
Nasikia pia waafrika wana DNA ya kutokuwa na akili! Wanasema hivyo wanaotuogopa kwa uwezo wetu mkubwa kwa kila kitu!
 
Back
Top Bottom