Last emperor
JF-Expert Member
- Mar 22, 2015
- 10,351
- 9,855
- Thread starter
-
- #21
Hayo aliyoyaongea kwa kifupi unayaonajeungeweka kipindi kizima ,si huu mtindo uliotumia wa kuleta kipande ili mpate sehemu ya kumtukania,si sawa,imani yangu kuna mengi ya msingi kaongea
Halafu akaugeuzia uso mgongoniMwendazake alimziba mdomo....!
Aisee kweli. Hapa alikuwa na akili zake timamu. Ila sasa hivi nina uhakika atakuwa amesharejewa tena na akili hii ya kuona umuhimu wa katiba mpya. Mama Samia naye na kina Kikwete, Zitto, Riziwani juzi juzi Magufuli alipokuwa ameshika hatamu nasikia walikuwa wanalia kichini chini mno kuwa yalifanyika makosa ya kutobadili katiba, lakini sasa hivi akili zimeshapeperuka tena wanasema tuwape muda.🤣 🤣 🤣 🤣 kabisa. Madaraka huwa yana corrupt akili za wasomi wetu.
Hata za mshahara tu akipata ataona wapangaji wenzake wote vibwengo.Mtu mweusi ukitaka kujua tabia yake mpe pesa au madaraka
SureHata za mshahara tu akipata ataona wapangaji wenzake wote vibwengo.
Alisema yeye ashachanjwa kwenye nchi sa wanao jielewa ahahahahna wale form six wliopata zero kama mbowe nao sijui akili zao zinaharibika na nini?
Kwa kweli Bashiru namvulia kofia. Hoja aliyojenga hapa ni kali mno, na itaendelea kuwa kali hata kama huyo aliyeijenga atafika mahali "akajingishwa" na kuwa MJINGA wa kupitiliza, kama ambavyo Bashiru wa siku hizi anajenga hoja kutoka tumboni, yaani kwa maslahi ya tumbo lake.Nawasalimia wana jukwaa la Great Thinkers!
Kuna usemi unasema siku hizi ogopa Mungu na Technolojia. Hii imekuja kuwaumbua watu wengi sana ambao walisema mambo tofauti na mambo ambayo walikuja kuyaishi baadae. Dk. Bashiru Ally alikuwa muumini mkubwa sana wa katiba mpya na alipinga kwa nguvu kubwa uroho wa madaraka wa wanasiasa, akisisitiza kuwa Katiba ni takwa la nyakati kwaajili ya ustawi wa nchi. Lakin siku zilivyoenda alivyokuja kuonja utamu wa madaraka alibadilika kabisa. Hali hii sasa tunaenda kuiona kwa Mama Samia Suluhu.
Mikutano yake ya mwanzo baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa kila akihutubia "ulimi unateleza" na anatamka neno katiba mpya na akakiri kuwa lipo kichwani pake hasa. Lakin baada ya miezi mitatu ya kushikilia madaraka, ameshaanza kusema kipaumbele chake ni uchumi na katiba mpya itasubiri, mpaka lini hatujui.
Ninachoona hapa kilichompata Dk. Bashiru kabla hajayaonja madaraka ndicho kinachompata Rais Samia Suluhu baada ya kukamatia madaraka.
View attachment 1835474
Hapa ni kabla hajaonja na madaraka.
View attachment 1835502
Na hapa ni baada ya "kuula".
Enzi za Bashiru akiwa na akili.Nawasalimia wana jukwaa la Great Thinkers!

Hivi kuitwa mtu Murundi na hali siyo Murundi unapata burudani gani? Au ni njia nyingine ya udhalilishaji? Je! Nchi ya Burundi unaidharau? Kwa nini hukusema ni Mughana, Mutswana, MuSudani?Bashiru alipokuwa UDSM na mwanachama wa CUF alikuwa bingwa wa kuongea masuala ya haki, demokrasia, usawa na Utawala bora.
Alipoletwa CCM na Binamu yake Mrundi mwenzie Magufuli akawa ndiye ana ratibu dhuluma dhidi ya upinzani. Ameshiriki kuwanunua akina Gekul, Silinde na Patrobas. Ameshiriki kuiba uchaguzi wa Serikali za mitaa wa 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020. Na aliwahi kunukuliwa akisema "Tutatumia dola kubaki madarakani"
Huyu mrundi ndiye ambaye Magufuli alikuwa anamuandaa kupokea U-RAIS wa Tanzania baaada ya mwenyewe kutosheka. Ila Mungu wetu ana maguvu, kasema HAPANA.
Warundi na Wanyarwanda wana DNA ya kuchukiana na kuuana. Kamwe nchi yetu isijichanganye na hiyo laana. Angalia Mwendazake alikokuwa anatupeleka.Hivi kuitwa mtu Murundi na hali siyo Murundi unapata burudani gani? Au ni njia nyingine ya udhalilishaji? Je! Nchi ya Burundi unaidharau? Kwa nini hukusema ni Mughana, Mutswana, MuSudani?
Kama ulikasirishwa na vitendo vyake ulivyovitaja je unamuadhibu kwa kumuita Murundi! Je urundi ni adhabu?
Maana ukianza kubagua mtu haijarishi unasemaje, kwa mfano - wewe si ni Mchaga? Lakini nikisema hawa wachaga eti ndio wanataka kuingia madarakani na kututawala! Hiyo statement utaichukia, hasa kama wewe siyo mchaga! japo kuwa unataka kufanya hivyo (kututawala). Be mature.
Hiyo clip kamili ukiitafuta YouTube ipo, ni kipindi cha nusu saa. Anayoongea huko kwingine ni hayohayo. Mtoa mada amelenga hasa alichosema Bashiru kuhusu Katiba Mpya. Binafsi niliipenda sana hoja yake kali sana. Kwamba:ungeweka kipindi kizima ,si huu mtindo uliotumia wa kuleta kipande ili mpate sehemu ya kumtukania,si sawa,imani yangu kuna mengi ya msingi kaongea
Hii habari ya fulani mrundi, fulani mtusi, fulani si mtanzania, ilianzia kwa Rais Mkapa. Baada ya kukosa hoja za kumjibu Jenerali Ulimwengu enzi hizo, alipoanza kuikosoa serikali ya Mkapa, baada ya kumpigia kampeni kali kupitia Rai ya Jenerali katika gazeti la Rai enzi hizo, Serikali ya Mkapa ikamtangaza Jenerali kwamba si raia. Alikuwa na cheo fulani Baraza la Michezo, na vingine vya heshima, vyote vikapukutika.Hivi kuitwa mtu Murundi na hali siyo Murundi unapata burudani gani? Au ni njia nyingine ya udhalilishaji? Je! Nchi ya Burundi unaidharau? Kwa nini hukusema ni Mughana, Mutswana, MuSudani?
Kama ulikasirishwa na vitendo vyake ulivyovitaja je unamuadhibu kwa kumuita Murundi! Je urundi ni adhabu?
Maana ukianza kubagua mtu haijarishi unasemaje, kwa mfano - wewe si ni Mchaga? Lakini nikisema hawa wachaga eti ndio wanataka kuingia madarakani na kututawala! Hiyo statement utaichukia, hasa kama wewe siyo mchaga! japo kuwa unataka kufanya hivyo (kututawala). Be mature.
Na chakula hasa msosi mmatumbi yaniiMtu mweusi ukitaka kujua tabia yake mpe pesa au madaraka
Mbowe ni msomi, anajua kujenga hoja, hadi anawatisha wasomi wooote waccm na serikali, wanaogopa kiasi kwamba wanaamua "kumnyamazisha" kwa kumtandika kesi la ugaidi lisilo na dhamana. Mpaka lifutwe, atakuwa kakaa gerezani sio chini ya mwaka.na wale form six wliopata zero kama mbowe nao sijui akili zao zinaharibika na nini?
Kabisa mkuuNa chakula hasa msosi mmatumbi yanii
Nasikia pia waafrika wana DNA ya kutokuwa na akili! Wanasema hivyo wanaotuogopa kwa uwezo wetu mkubwa kwa kila kitu!Warundi na Wanyarwanda wana DNA ya kuchukiana na kuuana. Kamwe nchi yetu isijichanganye na hiyo laana. Angalia Mwendazake alikokuwa anatupeleka.