Tuanzie kwenye sheria zinasemaje kwenye suala la kusaini mikataba nje ya nchi,,na waziri anaposafiri kwenda nje huwa anapata ruhusa kwa nani miongoni mwa viongozi wa nchi,,,Waziri pamoja na timu yake wakati wanaondoka kwenda Romania walitoroka bila kuwajulisha wakubwa zao.
Je usalama wa taifa pamoja na uhamiaji kwenye kiwanja cha ndege walichokitumia kupanda ndege hao viongozi hawakushituka kumuona kiongozi tena mwenye dhamana ya usalama wa Raia na mali zao akiondoka bila ruhusa ya wakubwa zake,,Usalama wa taifa unafanya kazi gani hadi unashindwa kumsaidia Rais kwenye kadhia hii?IGP SIRRO hakujulishwa na kamanda Andengenye kwamba anaenda nje ya nchi?
SIRRO hakumuliza mdogo wa kicheo kuhusu safari husika?na kama analijulishwa hakuweza hata kumshauri jinsi taratibu zinavyotakiwa kufanywa?hivi wizara haina mwanasheria wa kuwashauri viongozi wa wizara?Tutafakari kwa kina ili tujue chanzo ni nini?ikiwezekana wandishi wa habari waende Romania kujua zaidi ya zaidi maana kuna kizungumkuti.TUIJENGE TANZANIA KWA MUSTAKABALI WA KIZAZI KIJACHO.