Enzi za utoto....

Songa huyu wa tamaduni muziki??

Na kweli ukosefu wa mazoezi ulifanya niachane na sarakasi,japo home napo mama jolie alikua anapiga vita walahi nikikutwa najikunja kunja napigwa mpaka najuta hahaha

Baadae nilikujaga kumsikia akijadili na wamama wenzie wanamwambia asikubali niendelee kuruka sarakasi itanipa shida badae kwenye suala la kuzaa,eti sitazaa.Sarakasi ni za wanaume waliendelea kukazia nikapigwa vita vikali,japo ni kitu nnachokipenda....
 
kwa uwelewa wangu huu wa shule za kayumba nimekuelewa vizuri sana
 
Mimi ule mchezo wa baba na mama mpka kesho naucheza tu
 
Yes songa wa tamaduni music ana wimbo wake unaitwa Enzi za utoto.

Songa-Enzi za utoto.
"Kumbuka ni kitambo kabla ya Mr nice na Takeu/
Zishakuja kesi nyingi nimem'toa mtu ngeu/

Nilikuwa situlii akija mgeni labda uniwekee movie ya Brucelee na Jack chan"

Elimu pia ya wazazi wetu katika masuala ya michezo na Mambo mengineyo yakuhusu vipaji ilikuwa ni ndogo/bado ndogo.

Jana baada ya mechi ya man united vs arsenal Super sport tulikuwa tunaangilia mabinti wakinyonga nyoga viungo(mashindano) kwa ustadi mkubwa ilikuwa burudani sana.

Hahaha kwa hiyo saizi unapata watoto..?
 
Hahaha ngoja niende youtube kwanza nikamsikilize songa.


Bado sijaanza kujaribu kutafuta watoto heheehebehe
 
Hahaha ngoja niende youtube kwanza nikamsikilize songa.


Bado sijaanza kujaribu kutafuta watoto heheehebehe
Ayaaaa!!!kumbe bado upo upo kwanza,basi siku ukianza kutafuta watoto usimsahau Alisina,tunaweza leta akina Einstein na Isaac kwa awamu ya pili duniani,



Jolie Wa Jolie.!!
 
Kwahiyo utotoni mwako nyumbani mlikuwa na TV?
 
Kuna maza mmoja alikuwa anatengeneza keki za sherehe nikamsomea timing katoka nikapita na zile rangi za kupamba keki.........nikaza chupa za kutosha mchanganyiko wa maji rangi

tukienda shule jirani kucheza soka nakuja na product nikawapanga maneno hiyo inatumika baada ya 2 weeks ndo inakuwa tamu. Tena ikae kwenye Giza

Axe niliwaingiza kingi raia wengi wakaanza kunitafuta ningekamtwa meno ningepoteza manake nliwadanganya hadi wababe wa shule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…