Huyu Pfunk namkumbuka alikuwa bwana mdogo sana wakati mimi naanza rap pale SINZA. Nilipokuja sikia baadae kuwa ndo producer mkubwa pale kijitonyama alafu anawapeleka mputa wasanii just kurecord, alafu siyo bure bali kwa hela zao tena na appointment zake mwenyewe pfunk. Nikawa naongea na rafiki yangu mwingine pale bongo akaniambia jamaa (pfunk)noma, anajiona sana. Nakumbuka nikamwambia rafiki kuwa asijali sana kama kuna nyimbo anataka kirecord aende kwa master jay akarecord aachane na pfunk. Akanisikiliza. So pfunk kaishiwa...sababu kubwa za kuishiwa ni zifuatazo:
1. Hakujiandaa kukabiliana na upinzani wa studios zingine zilizofuatia
2. Hakuwa innovative enough na ndo maana hadi leo ukisikiliza productions zake hamna kipya, yale yale tu madudu
3. Bado hajui what is music business, ndo maana anaropoka wasanii wanaonewa wakati hakuna hata msanii mmoja bongo (si jidde wala ali kiba) ila diamond tu ambaye rasmi anatumia music publisher - Babu tale kupeleka nyimbo zake radioni na ktk TV stations.
MSIMLAUMU BABU TALE YEYE NI MUSIC PUBLISHER ILAINABIDI AWE RASMI NA ALIPIE USHURU NA AWE NA MIKATABA RASMI YA WAZI WAZI ILI WASANII WAWE WANAMTAFUTA.
Wasanii wengi walikuwa wanapeleka nyimbo radioni kiholela holela tu, kishkaji kukwepa kuuza copyright zao kwa publishers kama babu tale, lakini wanasahau kuwa hata akina dr.dre wanafuata misingi ya music business yaani kutumia pubishers alafu baadae mnakubaliana upya jinsi ya kugawana catalogue value ya copyrights za nyimbo zako. Jambo ambalo diamond atalifanya baadae.
4. Tanzania tunapenda kuepuka kufanya mambo kiholela holela. Wengi walikuwa wanapeleka nyimbo radioni kishkaji tu. Leo wanalalamika haki zao wakati radioni nyimbo zilifika kishkaji tu hakuna contract yoyote signed.
5. Nenda google tafuta music publisher hakuna mbali ya remmy ongala na ochestre matimila.( haya remmy aliyaina mapema sababu alifanya music na akina peter gabriel). Alikuwa mjuzi.
6. Ushauri kwa pfunk na wasanii wote wa bongo flava (kama watasoma yangu): jifunzeni kupita vyombo maana hapo mlipo copyright zenu anamiliki priducer wa studio. Mkishajua kupiga vyombo mnaweza kujadiliana na music publisher kuhusu haki zenu mkaeleweka. Ni rahisi that way kuliko kivingine..
- tumieni publishers ili mjulikane rasmi, na mlipwe haki zenu rasmi, hata mkifa kama akina ngwear ndugu zenu waweze kufuatilia haki zenu wazi wazi. Jiulizeni..NDUGU ZA NGWEAR WATAMDAI NANI HAKI ZA KIMUZIKI ZA NGWEAR??
wasalaam. Ni mimi msanii mwenzenu ughaibuni lakini soon nakuja bongo kiachia nyimbo zangu RASMI..