Kama ni kutumiwa na watawala, wewe ndo unatumiwa maana unajifanya huoni makosa kwenye huo mkataba wakati unayajua lakini kwa kuwa umelipwa hutayaona haya.
Ngoja nikwambie kitu kimoja ambacho pengine kwa upeo wako wewe hauwezi kukiona, na ndomaana inakuwa rahisi mno wanasiasa uchwara kuwatumia katika ajenda zao kwa faida zao.
Mwaka 2008 kuna wanasiasa uchwara ambao walikosa hoja kama ilivyo leo, wakamvamia waziri mkuu wa kipindi hicho mheshimiwa Lowasa na kuanza kusema kwamba ni fisadi. Kwa vile vijana wengi walikuwa na upeo mdogo wa kufikiri kama wewe wakajikuta wanakubaliana na wanasiasa uchwara hao na kuanza kushirikiana nao kumshambulia mzee Lowasa.
Mwaka 2015 wale wale waliokuwa wanasema kuwa Lowasa ni fisadi na ushahidi wanao kama wanavyowahadaa nyinyi sasa hivi, wakampokea jamaa awe mgombea wao wa uraisi na kudai kuwa Lowasa sio fisadi kama walivyohadaa huko nyuma.
Hii inaonesha fika kwamba walitumia njia ile ya Lowasa kujijenga kisiasa kama wanavyotumia njia hii ya bandari pia kujijenga kisiasa pamoja na chuki walizokuwa nazo kwa viongozi wa serikali nk.
Ndio maana mimi sitaki porojo za maneno matupu, bali facts za kunionesha sehemu ambayo inaonesha kuwa mkataba una makosa. Ukinionesha tu hiyo sehemu basi nitaomba radhi na kufuta post zote zinazo support huu mkataba.
Mimi sio wale watu wakushikiwa akili na wanasiasa uchwara, yani waniambie kitu nikubali bila kunionesha kile ambacho kitanishawishi mimi nikubaliane nao. Wewe endelea kuburuzwa kwa kisingizio cha uzalendo uchwara, huku wenzako wakivuta mpunga kutoka kwa watu waliokuwa wanapitisha mizigo yao bila kulipa kodi, wapitisha madawa ya kulevya na vishoka wa bandarini ili wawatetee.
Weka kipengele chenye makosa kwenye mkataba kwa faida ya mimi na wasomaji wengine ambao wanapingana na wanasiasa wenu uchwara, sio kuishia kuongea tu. Hizi sio zama za Lowasa watu tumeshajifunza, hatuwaamini wanasiasa kwa kigezo cha kelele tu mitandaoni, bali tunamuamini kwa kutuonesha ubaya wa kitu kupitia macho yetu ili wenye akili tumuunge mkono.