Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Tatizo lenu kila jambo mnataka kulifanya la kisiasa. Wakati wa raisi Kikwete hao wanaokutuma upige kelele leo ndio waliokuwa wanajifanya kupiga kelele kuwa serikali ya Kikwete imeshindwa kupambana na wauza madawa ya kulevya, na kwamba wao wakiingia watawakamata wote na kuwatupa ndani.Mkuu ukiwa kama baba ama mama wa familia hapo kwako.
Watoto wako wakiwa watukutu, kufuja mali hovyo, umalaya, wizi mtaani na tabia zote mbaya utamkodisha jirani akusaidie kuchukua hatua dhidi ya wanao.
Wizi, ufujaji wowote ule wa mali za umma ni kutokana na kuwa na serikali yenye viongozi hovyo wasioelewa wajibu zao kwa dhamana waliyopewa.
Serikali hasi duniani kote hujificha kwa udhaifu huo ili wao wajinufaishe.
Tujifunze kuwa wazalendo na wawajibikaji katika mali za umma lakini kuchukua hatua kali kwa wabadhirifu wote na wazembe.
Magufuli alivyoingia akalifanyia kazi swala hilo kwa kuanza kamata kamata. Kilichotokea kila mtu anakijua. Wauza madawa hao hao wakaungana na hao waliokuwa wanapiga kelele kuhujumu oparation ile ili isiendelee.
Kwahiyo hapo bandarini hata serikali ingesema ichukue hatua ambazo unasema, wale wapiga kelele wangehongwa tena ili wapaze sauti ili ionekane wameonewa, na pengine na wewe leo ungekuwa mmoja wa watetezi wao kisa tu kuna mwanasiassa au kiongozi mmoja unaempenda kawatetea.
Kuwafunga watu au kuwatesa kila siku hapo bandarini haiwezi kusaidia kitu. Sana sana vyama vya upinzani na hao jamaa wa haki za binadamu wangelalamika kuwa jamaa wanaonewa na hivyo nchi kutengwa kimataifa na pia kuendelea kupoteza mapato ya bandari.
Ndomaana serikali imeamua kufukuza majizi yote ili tuanze upya.
Hao wanaoalalamika wengi ni wanufaika wa mfumo mbovu uliyopo sasa hivi bandarini.