EPA, ESCROW na RICHMOND nazo zilitetewa kama inavyotetewa DP World

Kama ni kutumiwa na watawala, wewe ndo unatumiwa maana unajifanya huoni makosa kwenye huo mkataba wakati unayajua lakini kwa kuwa umelipwa hutayaona haya.
 
Kama ni kutumiwa na watawala, wewe ndo unatumiwa maana unajifanya huoni makosa kwenye huo mkataba wakati unayajua lakini kwa kuwa umelipwa hutayaona haya.
Ngoja nikwambie kitu kimoja ambacho pengine kwa upeo wako wewe hauwezi kukiona, na ndomaana inakuwa rahisi mno wanasiasa uchwara kuwatumia katika ajenda zao kwa faida zao.

Mwaka 2008 kuna wanasiasa uchwara ambao walikosa hoja kama ilivyo leo, wakamvamia waziri mkuu wa kipindi hicho mheshimiwa Lowasa na kuanza kusema kwamba ni fisadi. Kwa vile vijana wengi walikuwa na upeo mdogo wa kufikiri kama wewe wakajikuta wanakubaliana na wanasiasa uchwara hao na kuanza kushirikiana nao kumshambulia mzee Lowasa.

Mwaka 2015 wale wale waliokuwa wanasema kuwa Lowasa ni fisadi na ushahidi wanao kama wanavyowahadaa nyinyi sasa hivi, wakampokea jamaa awe mgombea wao wa uraisi na kudai kuwa Lowasa sio fisadi kama walivyohadaa huko nyuma.

Hii inaonesha fika kwamba walitumia njia ile ya Lowasa kujijenga kisiasa kama wanavyotumia njia hii ya bandari pia kujijenga kisiasa pamoja na chuki walizokuwa nazo kwa viongozi wa serikali nk.

Ndio maana mimi sitaki porojo za maneno matupu, bali facts za kunionesha sehemu ambayo inaonesha kuwa mkataba una makosa. Ukinionesha tu hiyo sehemu basi nitaomba radhi na kufuta post zote zinazo support huu mkataba.

Mimi sio wale watu wakushikiwa akili na wanasiasa uchwara, yani waniambie kitu nikubali bila kunionesha kile ambacho kitanishawishi mimi nikubaliane nao. Wewe endelea kuburuzwa kwa kisingizio cha uzalendo uchwara, huku wenzako wakivuta mpunga kutoka kwa watu waliokuwa wanapitisha mizigo yao bila kulipa kodi, wapitisha madawa ya kulevya na vishoka wa bandarini ili wawatetee.

Weka kipengele chenye makosa kwenye mkataba kwa faida ya mimi na wasomaji wengine ambao wanapingana na wanasiasa wenu uchwara, sio kuishia kuongea tu. Hizi sio zama za Lowasa watu tumeshajifunza, hatuwaamini wanasiasa kwa kigezo cha kelele tu mitandaoni, bali tunamuamini kwa kutuonesha ubaya wa kitu kupitia macho yetu ili wenye akili tumuunge mkono.
 
Kwa haya maelezo maana yake mwenye tatizo ni serikali kwahiyo serikali ndo ibinafsishwe
 
Wewe unaitetea DP World kupewa bandari zetu kwa mkataba gani uliyoiona? Tusipende sana kutetea ujinga, viongozi wetu wanashindwa ata kwenda hapo China wakajifunze namna ya kutengeneza tamaduni mpya ya kuongoza watu anawadai hawana uwezo.
Viongozi wanataka kukimbia tatizo badala ya kutatua tatizo...ujinga kwelikweli.
Hoja zinazotolewa na serikali ni za kijinga sana, hazina logic kabisa.
 
Nani anayepinga ubinafsishaji?
Tunachopinga sisi ni vile vipengere au yale makubaliano ni makubaliano ya kinyonyaji na kitapeli.
Yale makubaliano yanaonekana ni kama uuzaji wa bandali mazima.
Tutajie hivyo vipengele mkuu.
 
The question is: hiyo mikataba ya huko Marekani, UK, na kwingineko inasomeka sawa huu wa Tz?

Nasikia watu wanahofia the way mkataba unavyozungumza kwenye baadhi ya vipengere.🙇🙇
 
The question is: hiyo mikataba ya huko Marekani, UK, na kwingineko inasomeka sawa huu wa Tz?

Nasikia watu wanahofia the way mkataba unavyozungumza kwenye baadhi ya vipengere.[emoji144][emoji144]
umeeleza vizuri, wanasheria wanaokubaliana na huu mkataba huwa hawachambui kipengele kimoja kwa sababu kuna vipengele vinategemeana ili kuleta maana iliyokusudiwa.

Na wale wanaopinga wanasoma kipengele kimoja kimoja.

Hata vitabu vitukufu vya dini anaweza mtu mmoja akasoma aya moja na akaitumia kukuaminisha lile alilokusudia, bila kuangalia kama aya hiyo inategemea pia aya nyingine.

Ukitaka kujua ukweli wa huu mkataba sikiliza wanasheria wa pande zote mbili na hasa wale ambao hawana maslahi ya kisiasa.
 

Mkuu ukiwa kama baba ama mama wa familia hapo kwako.

Watoto wako wakiwa watukutu, kufuja mali hovyo, umalaya, wizi mtaani na tabia zote mbaya utamkodisha jirani akusaidie kuchukua hatua dhidi ya wanao.

Wizi, ufujaji wowote ule wa mali za umma ni kutokana na kuwa na serikali yenye viongozi hovyo wasioelewa wajibu zao kwa dhamana waliyopewa.

Serikali hasi duniani kote hujificha kwa udhaifu huo ili wao wajinufaishe.

Tujifunze kuwa wazalendo na wawajibikaji katika mali za umma lakini kuchukua hatua kali kwa wabadhirifu wote na wazembe.
 

Weka mkataba waliongia huko kwengine tulinganishe na hapa.

Kwa nini hamjifunzi huko kwenye madini, reli, dawasa wale wahuni gani sijui kutoka SA.

Umewekewa na mifano hapo, yote ilikuwa nija njema lkn kilichotokea unakijua.
TICTS si ilikuwepo hapo, unakumbuka wakati inapewa kandarasi na utetezi kwao.?
 
Wewe kwenye hili ungekaa kimya tu maana kama unautetea Mkataba wa DP World ni kwasababu ya udini tu na huna lolote!

Wewe baba paroko tulia usinipangie Cha kuongea kama Niko Kwa mwamposa hapa

Niutete mkataba wa DP World Kwa sababu ya udini kwani umeambiwa wanakuja kusilimisha nyinyi makafir muwe waislam had niwatetee Kwa udini.?

Au PENGO ameshawaongopea tayar huko kuwa waarabu wanakuja kuwasilimisha,maana PENGO ana laana yule,Rais akiwa muislam tuh kwake nongwa pi.mbi yule
 
HII NCHI NI MALI YA CCM ACHENI KELELE WAKIAMUA WANAKUUZA HATA WW
 
Escrow na Richmond haifanani kabisa na DPW ni vitu viwili tofauti kabisa.

Escrow na Richmond ni wizi wa kimfumo wa viongozi wa ngazi za juu, DPW ni uwekezaji wa pande mbili kwa maana ya biashara ya serikali ya Tanzania na ile ya Dubai.

DPW inahusisha utaalam wa masuala ya upakuaji wa makasha pale bandarini kama ilivyokuwa TICTS wakati Escrow ni wizi wa pesa za masuala ya umeme.

Mwenye uzoefu na masuala ya uongozi wa TZ anajua fika kwamba uzi huu ni wa kujaribu kuendelea kupotosha umaa juu ya malengo mazima ya uwekezaji na faida zake pale bandarini lengo haswa likiwa ni kuwalinda wezi wetu halisi na wahujumu uchumi.
 
Kwanini wewe unaepinga huo mkataba usituwekee hapa ili na sisi tuone hayo maeneo mnayosema hayafai?
Unataka mimi nikuwekee mkataba badala ya wewe kuanza kuonesha njia ya kutuwekea wa hapa ili tuone mapungufu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…