EPA, ESCROW na RICHMOND nazo zilitetewa kama inavyotetewa DP World

Tatizo lenu kila jambo mnataka kulifanya la kisiasa. Wakati wa raisi Kikwete hao wanaokutuma upige kelele leo ndio waliokuwa wanajifanya kupiga kelele kuwa serikali ya Kikwete imeshindwa kupambana na wauza madawa ya kulevya, na kwamba wao wakiingia watawakamata wote na kuwatupa ndani.

Magufuli alivyoingia akalifanyia kazi swala hilo kwa kuanza kamata kamata. Kilichotokea kila mtu anakijua. Wauza madawa hao hao wakaungana na hao waliokuwa wanapiga kelele kuhujumu oparation ile ili isiendelee.

Kwahiyo hapo bandarini hata serikali ingesema ichukue hatua ambazo unasema, wale wapiga kelele wangehongwa tena ili wapaze sauti ili ionekane wameonewa, na pengine na wewe leo ungekuwa mmoja wa watetezi wao kisa tu kuna mwanasiassa au kiongozi mmoja unaempenda kawatetea.

Kuwafunga watu au kuwatesa kila siku hapo bandarini haiwezi kusaidia kitu. Sana sana vyama vya upinzani na hao jamaa wa haki za binadamu wangelalamika kuwa jamaa wanaonewa na hivyo nchi kutengwa kimataifa na pia kuendelea kupoteza mapato ya bandari.

Ndomaana serikali imeamua kufukuza majizi yote ili tuanze upya.

Hao wanaoalalamika wengi ni wanufaika wa mfumo mbovu uliyopo sasa hivi bandarini.
 
CCM haikwepi lawama, lakini wangemuelewa Samia na malengo yake wasingekuwa na aina hii ya mawazo waliyonayo.
Wapiga madili bandarini, vishoka na wakwepa kodi wao sasa hivi maji yamewafika shingoni. Na ukizingatia wamehonga watu mamilioni ili wawasaidie kupiga kelele.

Sasa mamilioni yameliwa na serikali imewapuuza.

Serikali imeshagundua kwamba ikicheka na nyani itavuna mabua.
 
Siku zao zinahesabika.
 

Umeongea vizur Mkuu,

Wala Rushwa na wapiga madeal lazima wapinge sura mpya kuingia pale bandarin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…