EPA na mambo yake

Bot officers who are involved with epa scandal lupango muda huu.

Mkuu FDR, aisee umesema majamaa wa bot nao wameswekwa lupango au ni mimi nimesoma vibaya? Kama nimesoma sawasawa then naweza kwa nguvu zote kusema kwamba sasa mwendo ni mdundo manake hii kitu sasa ni barabara!!
 
Mkuu FDR, aisee umesema majamaa wa bot nao wameswekwa lupango au ni mimi nimesoma vibaya? Kama nimesoma sawasawa then naweza kwa nguvu zote kusema kwamba sasa mwendo ni mdundo manake hii kitu sasa ni barabara!!


Inaweza kuwa ni funika kombe mwanaharamu apite, sisemi lolote had nione mwisho wa hii kitu. Hapo nitaweka thumb up or thumb down.
 
Mkuu FDR, aisee umesema majamaa wa bot nao wameswekwa lupango au ni mimi nimesoma vibaya? Kama nimesoma sawasawa then naweza kwa nguvu zote kusema kwamba sasa mwendo ni mdundo manake hii kitu sasa ni barabara!!

Ndio. Mkurugenzi wa madeni ya nje, Mr Mwakosya, E. Komu, na wengine wawili akiwemo mwanasheria mwandamizi wa BOT. JK anai-handle hii issue kwa umakini mkubwa tu. Najua kumsifia Rais wetu humu ni lazima uwe kama taahira hivi lakini habari ndio hiyo.
 
dhamana ni haki ya kila raia. Kama sheria zikitumika bila woga, haki itatendeka tu na watakaothibitika kuwa ni wakosaji watafungwa. Uchungu tulionao usitufanye tukikuke misingi ya haki za raia. Dhamana ni haki na acha wapate kama wakitimiza masharti

mkuu fdr, aisee umesema majamaa wa bot nao wameswekwa lupango au ni mimi nimesoma vibaya? Kama nimesoma sawasawa then naweza kwa nguvu zote kusema kwamba sasa mwendo ni mdundo manake hii kitu sasa ni barabara!!

wameswekwa ndani ndani leo hapo kisutu,
 

Mh,
kuna yule Kejo hivi hahusiki hapa au? nifahamishe tafadhali...
 
Nadhani hawatamsahau Mzee wetu Padre Slaa kama shahidi muhimu. Ametoa mchango mkubwa sana kwenye sakata hili.
 
EPA tycoons denied bail...

THIS DAY

PROSECUTORS filed new charges of conspiracy, fraud and theft yesterday against three more suspects linked to the massive looting of funds from the Bank of Tanzania’s external payment arrears (EPA) account, as business tycoons Jeetu Patel and Johnson Lukaza remain in police custody after failing to meet tough bail conditions.

Patel and Lukaza were forced to exchange their luxury beach-front homes at the affluent Msasani Peninsula area in the city with squalid prison conditions after the court ruled that they had to deposit at least half of the staggering amounts of money they are accused of stealing, which amounts to tens of billions of shillings.

The two business tycoons were among a group of 10 suspects arraigned in court on Wednesday to face separate charges of conspiracy, fraud and theft of a combined total of more than 31bn/- from the EPA account.

Jeetu alone faces four different criminal cases linked to the EPA scandal. In one case, he was required to deposit at least 940m/- at the court for bail purposes.

In other separate cases where he was charged with stealing more than 7.9bn/-, 3.3bn/- and 4.9bn/- respectively, the businessman and his co-accused persons were required to deposit at the court half of the stated amounts as part of the bail conditions.

Other accused persons in the high-profile cases were similarly unable to meet the bail conditions set by the court after being asked to deposit huge amounts of money.

The three additional suspects arraigned yesterday -- Malijala Shaban Hussein, Rajab Shaban Maranda and Japhet Laiyandumi Lema -- are alleged to have stolen more than 10bn/- between them from the key BoT account during 2005/06.

A team of prosecutors led by Principal State Attorney Stanslaus Boniface unveiled the latest suspects behind the EPA scandal at the Kisutu Resident Magistrate’s Court before a crowd of curious onlookers.

Hussein and Maranda, who are Dar es Salaam-based businessmen, were charged with multiple counts of conspiracy, forgery, uttering false documents and obtaining credit from the BoT by false pretence.

According to prosecutors, the duo obtained a total of 3,868,805,757.15/- from the central bank between January 18 and November 3, 2005 in Dar es Salaam, through their company, Mibale Farm.

It was alleged in court that on January 15, 2005, the two accused persons forged certificate of business registration number 46211 and on September 12, 2005, uttered the false documents to the United Bank of Africa (UBA), purporting to show that the forged documents were duly issued to their company.

Hussein and Maranda were also jointly charged with forging similar documents purporting to show that they were the bona fide business partners in another company, Money Planners & Consultants Limited, and subsequently uttered false documents to this effect to the UBA Bank.

Prosecutors told the court that the accused persons had on September 8, 2005, also allegedly forged a deed of assignment between P.Gracel Company Limited of Germany and Money Planners & Consultants of Tanzania, purporting to show that one Jonas Back and Fundi H. Kitengo were directors of the respective companies.

The two accused persons were further charged with presenting forged documents to the central bank and fraudulently obtaining a total of 2,266,049,041.25/- from the BoT on December 7, 2005.

In another case before a separate magistrate, the same accused persons were charged with stealing 1,864,949,294.45/- from the BoT between April 1 and September 2, 2005, through fraud.

The two suspects are alleged to have forged certificate of business registration number 151025 and later presented the false document to UBA Bank, purporting to show that they were the owners of a company known as Kiloloma and Brothers Limited.

Maranda was arraigned in the same court before another magistrate for a different criminal case in which he was charged with allegedly forging a deed of assignment between Rashish Limited of Tanzania and General Market Limited of India.

The forged document purported to show that the Indian firm had credited a sum of 207,284,391.44/- to the Tanzanian company. Maranda went on to steal the stated amount from the BoT on the basis of the forged document, prosecutors told the court.

On the other hand, Japhet Laiyandumi Lema, who is one of the shareholders of the Moshi/Arusha-based Njake Hotels and Tours Limited and Njake Enterprises Limited, was charged with stealing more than 2.6bn/- from the BoT on August 25, 2006.

Prosecutors said the businessman allegedly obtained the stated amount from the EPA account through conspiracy, fraud and theft by forging legal documents between his firm and a foreign creditor company, C.ITOH of Japan.

Sources close to the prosecution side did not rule out the possibility of yet more suspects being arraigned in court in connection with the EPA scandal.
 
EPA yamnasa kigogo wa CCM

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

IDADI ya watuhumiwa wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezidi kuongezeka, baada ya jana watuhumiwa wengine watatu, akiwemo kigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rajab Shabani Maranda, kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Mbali ya Maranda, ambaye ni Katibu wa Uchumi na Fedha mkoani Kigoma, wengine waliofikishwa mahakamani jana ni mfanyabiashara maarufu wa mkoani Kilimanjaro na Arusha, ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Njanke Enterprises Ltd, Japhet Lema na Farijala Shabani Hussein.

Wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Hadija Msongo, Mwanasheria wa Serikali, Edger Luhoga, alidai kuwa Farijala na Maranda wanakabiliwa na mashitaka matano likiwemo kosa la kula njama, wizi, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kujipatia ingizo la fedha kwenye akaunti yao.

Alidai katika tarehe na mwezi tofauti mwaka 2005, jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao waliwasilisha nyaraka za kughushi katika Benki ya Afrika, wakijifanya wamiliki wa Kampuni ya Kiloloma & Brothers iliyonunua deni la sh 3,868,805,737.13 kutoka Kampuni ya BC Cars Exports Ltd ya Mumbai, nchini India.

Katika kesi hiyo, Hakimu Msongo alitoa dhamana kwa washitakiwa kwa sharti la kila mshitakiwa kutoa nusu ya fedha zinazodaiwa kuibwa, wadhamini wawili ambao wataweka bondi ya sh milioni 900 au hati za mali isiyohamishika, yenye thamani ya kiasi hicho cha fedha na kwamba ziwe zimefanyiwa thamini na mamlaka husika.

Pia washitakiwa hao wametakiwa kuacha hati za kusafiria mahakamani. Walishindwa kutimiza masharti na kurudishwa rumande hadi Novemba 11 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.

Katika kesi ya pili, mtuhumiwa Maranda anakabiliwa na makosa manne, yakiwemo shitaka la kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, wizi na kujipatia ingizo kwenye akaunti yake isivyo halali.

Katika kesi hiyo iliyopo mbele ya Hakimu Henzironi Mwankenja, Wakili wa Serikali, Fredrick Mnyanda, alidai kati ya mwaka 2004 na 2005, mtuhumiwa huyo alijifanya mmiliki wa kampuni hewa ya Rasshes, iliyoteuliwa kukusanya madeni ya Kampuni ya General Market & Co Ltd na kujipatia ingizo la fedha kutoka BoT, lenye thamani ya sh milioni 200.7.

Kwa upande wa serikali, ilisema upelelezi umekamilika na kwamba dhamana ipo wazi na mshitakiwa atatakiwa alipe nusu ya kiasi cha fedha anazotuhumiwa kuiba, au kuwasilisha hati ya mali isiyohamishika na wadhamini wawili ambao kila mmoja ataweka bondi ya sh milioni 69.

Aidha, katika kesi ya tatu, watuhumiwa Farijara na Maranda, wanadaiwa katika tarehe tofauti mwaka 2005, walighushi hati za BRELA, zinazoonyesha kuwa wao ni washirika katika Kampuni ya Money Planers&Consultant Ltd na kufanikiwa kujipatia ingizo la fedha kwenye akaunti yao, sh bilioni mbili kutoka BoT, na kwamba wameteuliwa kukusanya deni la Kampuni ya BC.Grancel&Co Ltd ya Ujerumani.

Watuhumiwa hao ambao walisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Nikumalila Mweseba, walikana tuhuma hizo na kesi kuahirishwa hadi Oktoba 11 mwaka huu, itakapotajwa tena.

Hakimu Mwaseba, alipanga tarehe hiyo baada kukataa ombi la mawakili wa utetezi, Mpaya Kamala na Martin Matunda, kuomba kesi hiyo iahirishwe hadi leo, kwa kuwa wateja wake watakuwa wamekamilisha masharti ya dhamana.

Katika kesi ya nne, Farijala na Maranda wanakabiliwa na makosa saba ya jinai na kwamba kati ya mwaka 2006 na wenzao wasiojulikana walikula njama na kutenda kosa kwa maelezo wao ni wamiliki wa Kampuni ya Mbare Farm na kujipatia sh bilioni 1.6, kutoka BoT, kwa madai kwamba waliteuliwa kununua deni la Kampuni ya Lakshni Textile Mills Coral Ltd.

Katika kesi ya tano ambayo inamkabili Japhet Lema anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Ezra Mwandu, ilidaiwa katika tarehe tofauti mwaka 2006, alitumia Kampuni ya Njake Enterprises Ltd kuchukua deni lenye thamani ya sh bilioni 2.6 la Kampuni ya C.Itoh&Co Ltd ya Japan, kutoka BoT.

Mtuhumiwa Lema ambaye alisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Euphemia Mingi, alikana tuhuma hizo na wakili wake aliiomba mahakama imwachie huru kwa jana, ili aweze kuletwa leo kwa ajili ya kupatiwa dhamana.

Wakili huyo alidai mtuhumiwa huyo alipigiwa simu Jumanne na makachero wa Polisi wakimtaka afike jijini Dar es Salaam bila ya kumweleza kitu walichomwitia.

"Mteja wangu alitii amri hiyo na kufika jijini, lakini ghafla jana aliambiwa na makachero hao anafikishwa mahakamani, hivyo ndugu zake ambao wangemdhamini walipata taarifa jana asubuhi na kwamba walikuwa wameanza safari ya kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kuja kumdhamini," alieleza.

Hata hivyo, Hakimu Mingi alikataa ombi hilo na kuamuru mtuhumiwa huyo apelekwe rumande na kuahirisha shauri hilo hadi leo, kwa ajili ya mtuhumiwa huyo kupewa dhamana.

Katika hatua nyingine, watuhumiwa 10 ambao walifikishwa mahakamani hapo juzi, jana walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za dhamana.

Hata hivyo, mtuhumiwa Johnson Lukaza hakufikishwa mahakamani jana na badala yake wakili wake, Alex Mgongolwa na ndugu zake walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za dhamana.

Baada ya ndugu hao kukamilisha tarartibu hizo, upande wa mashitaka uliandika hati ya kumtoa rumande mtuhumiwa huyo, ili aletwe leo kwa ajili kudhaminiwa.

Hata hivyo, mahakimu mbalimbali wanaosikiliza kesi nne zinazowakabili watuhumiwa wanne wenye asili ya Kiasia, Jayantkumar Chandubhai Patel ‘Jeetu Patel', Devendra K. Vinodbhai Patel, Amit Nandy na Ketan Chohan, waliongeza masharti ya dhamana kwa watuhumiwa hao, kwa kuwataka wawasilishe hati za mali zisizohamishika, ambazo zitakuwa zimefanyiwa tathmini na mamlaha husika.

Kesi hizo zimeahirishwa hadi Novemba 20 mwaka huu zitakapotajwa tena na washitakiwa hao kukamilisha taratibu za dhamana.

Aidha, katika kesi nyingine inayomkabili Jeetu Patel na wenzake watatu, inatarajiwa kutolewa uamuzi wa kupatiwa dhamana leo katika mahakama hiyo.
 
Jamani kwanza kabisa ni kweli kulikuwa na marundo ya fedha katika benki ya Exim na waliopeleka wanajulikana, lakini kitaaluma huwezi kuwataja ktk gazeti

Tutajie hapa basi
 
Mimi binafsi naona mwizi anaye liibia taifa hana tofauti na muuaji.
Angalia wangapi wanakufa kwa kukosa angalau panadol,wangapi wanakufa kwa maralia ,wangapi wanakufa kwa kukosa vifaa vya kujifungulia?
Sasa iweje hawa jamaa wapewe dhamana?Wanatofauti gani na muuaji?Hawana tofauti kabisa wanawakosesha watu haki ya kupata huduma mhimu za kijamii kwa kujinufaisha wao binafsi na jamaa zao kwa mabilioni kisha eti tufuate haki tufuate haki kwa muuaji?
Hapo hapana wao hawafai kabisa katika jamii inabidi watengwe kwa njia zote ni wezi kila kukicha tunapiga kelele kuhusu wezi leo mnawaachia kwa dhamana wakifanya dili tena ili washughulikia kesi zao si wataendelea na mchezo huu huu mchafu?
Sheria ya China ni nzuri sana ningependa itumike hata hapa kwa kukata vichwa watu wanao hujumu uchumi wa nchi ili iwe fundisho kwa wengine. Watu wanajinufaisha wao na jamaa zao huku wakiwaacha mamilioni ya waTZ wakihangaika huku na huku leo hii ukilipwa 100,000 kwa mwezi haina maana utafanyia nini?Watu tunazidi kuwa maskini kwa ajili ya wachache na tunawaonea aibu na huruma kwa nini tusiwatenge katika jamii hawa??????????
 
mimi sijui nimesoma vibaya,yaani MANJI karudisha takribani hela yote aliyochukua.kweli tanzania kichwa cha mwendawazimu,unacheza game,wakistuka unawapoza,and when the coast is clear you rise up and play the game again.i have a feeling we are trying to appease donors au CCM is laying the GROUNDWORK ya the coming election.wana JF its very important we read between the lines
 


Yasemekana Manji ana mitambo ya kuchapisha noti bandia.
 
yasemekana watuhumiwa wa epa wakipatikana na hatia watahukumiwa kuanzia kifungo cha maisha hadi adhabu ya kifo
 

innocent until proven guilty.....
Ndio maana bail ni haki. Na kama wana wakili mzuri anaweza aka question iyo bail amount iliyowekwa, maana inakuwa sawa na kuwanyima bail. The amount is too high, assuming they are innocent they wouldnt have that much
 

Ndugu/Mh Zitto ni maoni mazuri..Lakini itawezekana vipi? Je unamaanisha hilo litatokea ama unataka litokee?
Na kama unataka litokee kwanini usiwaambie wananchi wa Jimbo lako waichaguwe ccm?
Je kama wananchi kila kona wamechoshwa utawaambia waichaguwe ccm?
Je ni majimbo gani utakayoyachaguwa kuwa yaichaguwe ccm?
Wananchi wakikataa kama Taifa watakataa vipi? Ama unazungumza na jimbo lipi?
Mh Zitto maswali ni mengi sana kwenye hiyo hoja yako ni matumaini yangu utajaribu hayo mawili matatu hapo juu.
Natanguliza shukrani.
 
Yasemekana Manji ana mitambo ya kuchapisha noti bandia.

Mkuu Invicible!! akiona hii Kuhani lazima akuulize source ya hii tuhuma maana si kitu kidogo. Jamaa anapesa nyingi sana za EPA na other evil deals ndo maana watu wanahisi huenda anazifyatua mwenyewe!!
 
Heko JK kwa maendeleo ya EPA......but you are too damn slow maan........ile story ya kuwa tungezikosa pesa kama tungewakamata mapema......mimi kama Ogah i don't buy it..........

Ushauri kwa JK
...wale wote walio serikalini waliojihusisha na EPA........anza nao............na usiwaonee huruma fukuza kazi......Mtu kama Mgonja sijui unamcheleweshea nini.......
 

Toka zako na uongo wako huyo ndugu yake gani mwenye pesa Makubo ? wote wezi tuu na mabwenga tunawajua kwa uana mtandao hamna lolote mdomo tuu
 
The Lukazas are THIEVES!!..........no any other word can describe them better than that......damn......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…