Dhamana ni haki ya kila Raia. Kama sheria zikitumika bila woga, haki itatendeka tu na watakaothibitika kuwa ni wakosaji watafungwa. Uchungu tulionao usitufanye tukikuke misingi ya Haki za Raia. Dhamana ni Haki na acha wapate kama wakitimiza masharti
Mheshimiwa Zito hapo umetoa dira kwetu sote humu, kinachotokea pale Kisutu ni pratice of Rule of law-Tanzania hivyo ni vema tukaamini kuwa pale haki itatendeka kadri DPP alivyojipanga 1. Charge sheet against those Watuhumiwa,2. State attorneys watakavyoweza ku address fact na vithibitisho dhidi utetezi wa watuhumiwa.
Mahakama inalo jukumu moja tu pale, kutafsiri na kuhakikisha sheria inakata kila upande na hatimaye haki kutendeka kwa kila upande.
Mheshimiwa napenda kuungana na baadhi ya wana sheria nchini waliosomeka ktk gazeti la Mtanzania kuwa hii issue kama mlivyoiibua kisiasa na sasa imejengewa image ya kisiasa pale Kisutu, namna Kisutu inavyopelekeshwa sidhani kama lengo sahihi litafikiwa, nalo lile la kuruhusu kila muhimili wa dola kufanya kazi kwa uhuru na haki, game iliyopo Kisutu ni kuichafua mahakama na si kuipa haki stahili mahakama kama wengi wanavyodhania.
Wale mahakimu tayari wameshaanza kuandamwa na kashfa tangu juzi eti washakula mlungula!!!! Wanaowatuhumu wanasema chanzo chao inadaiwa ni UWT, tunasikia hizi tetesi tangu juzi zinavuma, wasimamizi hawa sasa hawajiamini ktk kutekeleza wajibu wao, hawaaminiani miongoni mwao na zaidi wanaona serikali inataka kuwaingiza ktk matatizo ya makusudi dhidi ya wananchi,ukiangalia yale masharti wanayoyatoa pale yanaashiria hofu na mashaka ktk ku pratice mamlaka waliyonayo kikatiba kama mahakimu,hii inaifanya Kisutu na Judiciary as whole kubeba sura au laana ya kuinyima jamii yetu kile kinacholiliwa na wengi. Je ktk hali hii kuna uwezekano wa kweli na haki kupatikana bila kujali nani mshindi?
Mheshimiwa fanya utafiti wako kama kijana mwenzangu mjenga nchi, juu ya hilo lakini ni vema ukaendelea na hili la kuhubiri hapa Jf na ktk majukwaa yako kisiasa , kuwa haki ya yeyote yule ni pale mahakama itakapoamua aidha kukubalina na washitaki au washitakiwa.
Mheshimiwa na wana Jf, safari ni ndefu ktk vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu (Mmomonyoko wa maadili ya Taifa letu), Mheshimiwa Rais yuko ktk right track ktk kuishape nchi, miaka takriban mitatu tayari ameonyesha dhamira yake. Haihitaji kushangiliwa maana yeye anawajibika according to his job description, sisi nasi tusimame ktk zamu zetu ktk kulipeleka taifa hili mbele.
Mjenga nchi ni Mwananchi / Mbomoa nchi ni Mwananchi- Tuache utamaduni wa kulalamika hovyo kanakwamba sisi ni wapangaji ktk nchi hii,tuwajibike waungwana.
Twende Pamoja, Inawezekana.
Mungu Ibariki Tanzania.