EPC + F Siyo Muujiza na Hakuna Utawala Ambao Ungeshindwa Kuutumia Kama Ungekuwa ni Absolute Solution

Ndugu we umeingizwa chaka huyo kilaza hakuna analoju huyo ni mzushi mwongo wa siku zote. We isikilize na kuiamini serikali yako achana na hao wafuasi wa mwendazake wametemwa sasa wanataka kutututmia watanzania kwa maslahi yao. Atapata mazuzu lakini wenye akili wanmfahamu huyo Bams, fuatilia nyuzi zake zote, ni za kizushi zilizojaa chuki na ubaguzi
Mi natamani sana unifafanulie tofauti na Bams.
Naomba unifafanulie seriously mi siijui hiyo EPC + F
 
Tunawapongeza wale wote ambao kila siku, usiku na mchana, wanafikiria namna ya kutatua matatizo ya nchi na wananchi.

Lakini watu watambue kuwa hakuna muujiza wa kuifanya nchi ipate maendeleo, na kulala na kuamka, matatizo ya nchi na wananchi yakaisha, zaidi ya kufanya kazi kwa bidii, kujinyima, umakini wa mipango na usimamizi, kuzuia ufisadi na miradi yenye mikataba ya hovyo, weledi na uadilifu wa wasimamizi na watendaji wa Serikali.

Nchi yetu ina vitu vingi vya kuisaidia ipige hatua kwenda mbele. KIKUBWA INACHOKIKOSA NI SERIKALI MAKINI, ILIYOJAA WATU WAADILIFU NA WENYE WELEDI. Hilo ndiyo tatizo kubwa la nchi yetu, kuliko mengine yote.

Matatizo yetu kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na mipango mibovu, sera mbaya, sheria mbaya, usimamizi mbaya, wizi, ufisadi, ubadhirifu na weledi mdogo wa wafanya maamuzi na watunga sera.

Serikali yetu imekuwa ni Serikali ya hadaa kwenye mambo mengi. Ni Serikali inayofanya jambo dogo halafu kelele za kujisifu ni kubwa kupindukia. Hata inapofanya makosa, ni mwiko kukiri kuwa imefanya makosa, badala yake ni kuongeza nguvu na jitihada za kujisifu. Ni Serikali defensive, yaani kulinda kwa gharama yoyote yale makosa ambayo inakuwa imefanya.

Angalia hata mkataba wa DP, ni dhahiri kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, mkweli wa nafsi na mwadilifu, ataona kwa uwazi kabisa mkataba huo ulivyo wa hovyo na mapungufu mengi, lakini Serikali na watu wake wanapambana usiku na mchana kuwahadaa wananchi kuwa ni mkataba mzuri sana, utakaoondoa tatizo la ajira, na kuifanya nchi iwe tajiri, na kuwezesha kufutwa kwa kodi nyingi na tozo.

Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.

Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.

Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.

Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.

Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.

Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.

Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.

Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.

Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?

Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?

Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.

Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.

Utawala wa Samia japo unajitahidi kwenye ujenzi wa miundombinu lakini tusizidishe sifa za uwongo. Siyo kweli kuwa utawala huu utajenga barabara nyingi kuliko tawala zote. Ukweli ni kwamba, hakuna utawala uliojenga kilometa nyingi za barabara za lami kuliko awamu ya 4. Zaidi ya 60% ya barabara zote ndefu za lami zimejengwa wakati wa awamu ya 4. Hakuna utawala uliojenga taasisi nyingi na kubwa mbalimbali kama vile viwanda, hospitali na vyuo, tena vyenye ubora wa hali ya juu, kama utawala wa Mwalimu Nyerere. Hakuna utawala ulioanzisha miradi mingi mikubwa kwa wakati mmoja, kama utawala wa Magufuli. Hakuna utawala uliojenga mifumo mizuri ya uchumi, na aliyeweza kushusha mfumko wa bei kutoka two digits mpaka single digit, kama Mkapa.

Mpaka sasa, hakuna kipya, hata kama kuna mambo mazuri yanafanyika.

Tupunguze sifa za hadaa, tufanye kazi. Nchi bado ni maskini, watu bado ni maskini. Katiba yetu na sheria zetu bado ni mbaya. Uadilifu ndani ya Serikali bado ni hafifu sana. Ubunifu, weledi na umakini ndani ya Serikali bado ni duni. Spidi ya miradi ya maendeleo na ongezeko la pato la Taifa ni ndogo kuliko ongezeko la watu.

Sifa nyingi tunazoipa serikali ni sifa bandia. Tunachotakiwa ni kuzidi kuisukuma serikali kuongeza speed zaidi ili iendane na ongezeko la mahitaji ya nchi.
Si mngefanya sasa?

Yaani kila kitu kikifanyika ndio mnakuja kujifanya wajuaji

No wonder nchi inasuasua

Let’s accept kwamba an ainnovative approach has been adopted and the progress is here

Haters mtakufa midomo wazi
 
Yes

Kama ni kitu cha kwawaida waishindwa nini kufanya

Tukubali tu Samia kaacha wataalam wafanye kazi

Mwamba alikua kila kitu anafanya yeye

She is more efficient
Mimi siwashindanishi JPM na SSH
 
Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa.

Tena mkopo ulio na kulipwa kwa fedha ya kigeni.

Hakuna kampuni ya kiTanzania ijenge barabara hizi kwa zege, nondo, simenti zinazozalishwa Tanzania na viwanda vya ndani Twiga cement, Dangote n.k hivyo kulipwa 100% kwa fedha yetu ya shilingi ya kiTanzania

Barabara nyingi the Philippines na Marekani ya Kusini ni zege wameondokana na utegemezi wa kuagiza lami toka nje ya nchi zao na miradi hii mikubwa ya barabara kutengeneza makampuni makubwa ya mabilionea wapya raia wa nchi zao.

Tanzania kuyalipa makampuni ya nje kutoka China, Turkey na lami ya Uarabuni ni mambo ya kizamani sana wakati ma engineer / technicians waTanzania wapo, mawe, kokoto, nondo, cement vinapatikana ndani.

Kwa barabara za mitaa ya mijini, Halmashauri pia vijijini barabara za mawe zipewe nafasi yake kutokana na gharama ndogo, hudumu muda mrefu na zinaweza kujengwa na kampuni ndogo za waTanzania

Picha moja wa mitaa ya Igogo na Kitangiri jiji la Mwanza, Tanzania
1687082243363.png

Duh watanzania mna nongwa sana, hata mfanyiwe nini hamridhiki.

Huo mtindo wa ujenzi ni mahususi kwa ajili ya kuboost uchumi kwa maana serikali italipa zaidi lakini hela itawafikia watu kupitia hao wakandarasi. Kupitia huo ujenzi kuna vibarua, wafanyakazi mbalimbali wataajiriwa, wauza materials watapata pesa n.k so pesa mtaani itakuwepo.
Acha uongo! Angalia Resident engineers wote wanatoka Ethiopia na hata materials nyingi za ujenzi zitatoka nje, nyie Watanganyika mtakuwa vibarua tu na kubaki kuuziana chai na chips!
 
Huu utaratibu ungekuwa na tija kama tungekuwa na wakandarasi wa ndani wenye uwezo na kusaidiwa pia na mabenki yetu kwa riba nafuu ingawa hatuna displine ya kulipana, refer madeni anayodai Tanesco hadi wengine wanasamehewa tu.

Hili ni bomu linakuja, Financiers watatoa pesa kwa riba za ajabu na masharti magumu then tusishangae serikali ikaja kuzidiwa na madeni hatarishi na kushindwa kulipa kwa wakati na kupelekea client na financier kuamua kutoza pesa wanaopita kujilipa. Tunaweza kuona haitakuwa hivyo lakini kwa tatizo la rushwa na umakini mdogo tutajiingiza kwenye matatizo.

Hakuna mtu atajenga barabara kwa fedha zake alafu uchelewe kulipa huku pesa amekopa asichukue hatua! Financier lazima watatumia any means kupata chao.

Hii serikali naona inakurupuka sana. Hapa haina tofauti na kubinafsisha ujenzi wa barabara na matokeo yake kwa haraka ni gharama kubwa kutumika wakati serikali ndio ina nyezo za kupata mikopo ya gharama na masharti nafuu.
Uko sahihi, hiki kitanzi kimekuja ili kuendana na zile sifa kuwa maendeleo tumeyaona kwa macho yetu. Inaonekana ili awamu hii ionekane inafanya kazi ni lazima ijenge miundombinu ili watu waseme hayo maendeleo yanaonekana kwa macho.

Kwamba ni mikataba mibaya kwao sio tatizo,maana wananchi wengi hawana uelewa wa haya mambo kwa kina zaidi ya kuona barabara kwa macho.
 
Tunawapongeza wale wote ambao kila siku, usiku na mchana, wanafikiria namna ya kutatua matatizo ya nchi na wananchi.

Lakini watu watambue kuwa hakuna muujiza wa kuifanya nchi ipate maendeleo, na kulala na kuamka, matatizo ya nchi na wananchi yakaisha, zaidi ya kufanya kazi kwa bidii, kujinyima, umakini wa mipango na usimamizi, kuzuia ufisadi na miradi yenye mikataba ya hovyo, weledi na uadilifu wa wasimamizi na watendaji wa Serikali.

Nchi yetu ina vitu vingi vya kuisaidia ipige hatua kwenda mbele. KIKUBWA INACHOKIKOSA NI SERIKALI MAKINI, ILIYOJAA WATU WAADILIFU NA WENYE WELEDI. Hilo ndiyo tatizo kubwa la nchi yetu, kuliko mengine yote.

Matatizo yetu kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na mipango mibovu, sera mbaya, sheria mbaya, usimamizi mbaya, wizi, ufisadi, ubadhirifu na weledi mdogo wa wafanya maamuzi na watunga sera.

Serikali yetu imekuwa ni Serikali ya hadaa kwenye mambo mengi. Ni Serikali inayofanya jambo dogo halafu kelele za kujisifu ni kubwa kupindukia. Hata inapofanya makosa, ni mwiko kukiri kuwa imefanya makosa, badala yake ni kuongeza nguvu na jitihada za kujisifu. Ni Serikali defensive, yaani kulinda kwa gharama yoyote yale makosa ambayo inakuwa imefanya.

Angalia hata mkataba wa DP, ni dhahiri kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, mkweli wa nafsi na mwadilifu, ataona kwa uwazi kabisa mkataba huo ulivyo wa hovyo na mapungufu mengi, lakini Serikali na watu wake wanapambana usiku na mchana kuwahadaa wananchi kuwa ni mkataba mzuri sana, utakaoondoa tatizo la ajira, na kuifanya nchi iwe tajiri, na kuwezesha kufutwa kwa kodi nyingi na tozo.

Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.

Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.

Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.

Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.

Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.

Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.

Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.

Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.

Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?

Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?

Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.

Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.

Utawala wa Samia japo unajitahidi kwenye ujenzi wa miundombinu lakini tusizidishe sifa za uwongo. Siyo kweli kuwa utawala huu utajenga barabara nyingi kuliko tawala zote. Ukweli ni kwamba, hakuna utawala uliojenga kilometa nyingi za barabara za lami kuliko awamu ya 4. Zaidi ya 60% ya barabara zote ndefu za lami zimejengwa wakati wa awamu ya 4. Hakuna utawala uliojenga taasisi nyingi na kubwa mbalimbali kama vile viwanda, hospitali na vyuo, tena vyenye ubora wa hali ya juu, kama utawala wa Mwalimu Nyerere. Hakuna utawala ulioanzisha miradi mingi mikubwa kwa wakati mmoja, kama utawala wa Magufuli. Hakuna utawala uliojenga mifumo mizuri ya uchumi, na aliyeweza kushusha mfumko wa bei kutoka two digits mpaka single digit, kama Mkapa.

Mpaka sasa, hakuna kipya, hata kama kuna mambo mazuri yanafanyika.

Tupunguze sifa za hadaa, tufanye kazi. Nchi bado ni maskini, watu bado ni maskini. Katiba yetu na sheria zetu bado ni mbaya. Uadilifu ndani ya Serikali bado ni hafifu sana. Ubunifu, weledi na umakini ndani ya Serikali bado ni duni. Spidi ya miradi ya maendeleo na ongezeko la pato la Taifa ni ndogo kuliko ongezeko la watu.

Sifa nyingi tunazoipa serikali ni sifa bandia. Tunachotakiwa ni kuzidi kuisukuma serikali kuongeza speed zaidi ili iendane na ongezeko la mahitaji ya nchi.
Mbegu ya hii tabia ya kusifia uongozi wa kisiasa kuwapamba na hata kuwahami viongozi wa kisiasa ilipandwa awamu ya nne (4). Kwa mara ya kwanza tulianza kushuhudia raia wa kawaida wakijipa jukumu la kumsemea kiongozi na serikali yake. Awamu ya tano (5) tabia hii iliendekezwa zaidi na kuchukua sura tofauti. Kipindi hiki raia wanaomsemea kiongozi na serikali yake waliongezeka sana. Aidha katika kutekeleza jukumu hilo nguvu za hoja zilitumika zaidi ikiwa ni pamoja na watu wenye mawazo tofauti kupachikwa majina mabaya na kutishwa.

Swali la kujiuliza ni je, nini chimbuko la tabia hii? Kwa maoni yangu ni udhaifu katika uongozi. Kadri nchi yetu inavyopata viongozi dhaifu ndivyo tatizo hili linavyoshamiri na kuchukua sura ya kutia kinyaa. Uongozi wa awamu ya 4 ulikuwa dhaifu sana hivyo ukajikita katika giliba, propaganda na matumizi ya mabavu. Uongozi ulioko madarakani sasa ni mwendelezo wa awamu ya tano hivyo hakuna kikubwa kilichobadilika. Sana sana kinachoonekana ni kupungua kwa matumizi ya mabavu. Wakati huo huo kuna hisia na hofu kubwa ya uongozi kupwaya. Kufidia pengo la kupungua kwa matumizi ya mabavu na hofu ya uongozi kupwaya, imebidi kuongeza propaganda inayojikita zaidi katika kumjenga kiongozi binfsi.
 
Wewe ni kati ya watu ambao mnatakiwa kupigwa mawe kama kibaka na uwashie tyre ya moto .Kenge Mkubwa
Kichaa ukikutukana uliye na akili timamu, unamwonea tu huruma maana siamini ameupata ukichaa kwa kupenda.

Nakuonea huruma, na ndugu zako wanaokuhudumia. Kumtunza kichaa kunahitaji uvumilivu wa pekee.
 
Hiyo mimba bado hujazaa? Utahangaika sana mwishowe itachoropoka tu. Unahangaika sana na uzushi, uwongo, kueneza chuki kwenye serikali hii kuleta kila kioja cha kipuuzi, jua watanzania wamekupuuza hutafanikiwa. We ni nyau mdogo sana na mbaya uwezo wako kichwani nimdogo sana. Rais wetu ni mtu mwenye maono makubwa anatujengea barabara 7 zenye Km 2035 kwa wakati moja, haijawahi tokea. Hizo porojo zako zingine mpelekee mamako aliyezaa jinga km wewe.
Crap from a low mind. Ignored.
 
Back
Top Bottom