Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bahati mbaya hakuna anayehoji. Hata wale wabunge batili hakuna wanachofikiria zaidi ya kusubiria rushwa ili waisifie mikataba ya hovyo.Huu ni wizi na utaleta mzigo mkubwa sana kwa serikali zi azo kuja
1. Hakuna anaye jua haya makubaliano zaidi ya samia na mbarawa
2. Hakuna anaye jua interest rate iliyo kubaliwa.
3. Hakuna anaye jua gharama halisi za miradi hii .
4. Hakuna uwazi, hawa wachina wasije siku wakazitaka hizi barabara
Yawezekana unakaribia kupagawa. Eti mimi Bams ni mfuasi wa marehemu Magufuli!Ndugu we umeingizwa chaka huyo kilaza hakuna analoju huyo ni mzushi mwongo wa siku zote. We isikilize na kuiamini serikali yako achana na hao wafuasi wa mwendazake wametemwa sasa wanataka kutututmia watanzania kwa maslahi yao. Atapata mazuzu lakini wenye akili wanmfahamu huyo Bams, fuatilia nyuzi zake zote, ni za kizushi zilizojaa chuki na ubaguzi
Tuache unafiki wa kujisifia na kujipongeza sana kwa mafanikio kiduchu. Kuridhika na kujipongeza sana kwa mafanikio kidogo kunajenga moyo wa kurudhika na kutojishughulisha zaidi na kwa kasi zaidi.Hakuna awamu ambayo hikukopa Tena magufuli ndio aliyekopa kwenye nabenk
Kwaiyo maoni yako ni nini?
Tuungane kupaza sauti, na wakati fulani kupinga kwa nguvu zetu zote, serikali inapotufanyia hadaa.Tungekua na kiongizi aina yako hakika tungefika mbali wapo baadhi lakini system haiwaruhusu kutoa maoni Yao wanabk tu kusifia ...rip Magu
ulitaka jipya litoke kutoka wapi katika dunia hii? Hebu punguzeni povu musije pata pressure bureMpaka sasa, hakuna kipya, hata kama kuna mambo mazuri yanafanyika.
DP, serikali na makampuni makubwa yasiyo na uadilifu, ndio wenye pesa za kuwahonga watu.Nasikia kuna watu wanalipwa humu kushambulia serikali...Kwa hiyo usishangae threads za kushambulia Hadi mbinu za kutatua matatizo
Ni vema ukaja na uzi wenye kuelezea uhalisia wa jambo na kukanusha upotoshaji kwa hoja sahihi, kinyume chake kumtusi mleta mada ww ndie unastahili kupigwa mawe kama kibakaUmelewa kwa maana huyu mpuuzi amepotosha saaana
CrapAcha uongo! Angalia Resident engineers wote wanatoka Ethiopia na hata materials nyingi za ujenzi zitatoka nje, nyie Watanganyika mtakuwa vibarua tu na kubaki kuuziana chai na chips!
I would wonder if a gay person like you could understand! You keep on being sodomized, that is what you can afford!Crap
Very crappy project haijaanza tayari umeshapanga safu
You are such an ass
Losing argument kijinga Hivi only works for idiotsI would wonder if a gay person like you could understand! You keep on being sodomized, that is what you can afford!
🖕
I thought you were a man! Now I know you are a shithole!Losing argument kijinga Hivi only works for idiots
Issue za matusi Hivi only comes from assholes
Umesikia vibaya. Sifa kuu ya JF ni kukosoa bila kuogopa. Aidha, ni sehemu ambapo anaekosolewa ana haki ya kujitetea bila kuogopa. Ndivyo ilivyokuwa. Hapa hapakuwa mahali pa vuvuzela. Kiongozi makini anathamini wale wanaomueleza ukweli wao kuliko wale ambao wanaona kuwa wajibu wao ni kumsifia hata pale ambapo dhahiri amekosea. Watu kama nyie ambao badala ya kuitetea serikali kwa kujibu hoja kwa hoja mnakimbilia kumwaga matusi na kuwashutumu wenzenu kuwa wamenunuliwa mnatia doa platform hii.Nasikia kuna watu wanalipwa humu kushambulia serikali...Kwa hiyo usishangae threads za kushambulia Hadi mbinu za kutatua matatizo
HakikaTatizo la Tanzania na matumizi ya anasa
Acha kujitoa ufahamu. Njoo waone vibarua wa SGR wanalipwa kiasi gani ni shilingi unaiona mtaani. Hamnaga kitu kama hichoeti fesa zitajaa mtaani. Labda uchumi wa kwenye karatasi.Duh watanzania mna nongwa sana, hata mfanyiwe nini hamridhiki.
Huo mtindo wa ujenzi ni mahususi kwa ajili ya kuboost uchumi kwa maana serikali italipa zaidi lakini hela itawafikia watu kupitia hao wakandarasi. Kupitia huo ujenzi kuna vibarua, wafanyakazi mbalimbali wataajiriwa, wauza materials watapata pesa n.k so pesa mtaani itakuwepo.
Wivu baada kupigwa za uso.Unatumia EPC+F kama una pesa na akili,wajinga wajinga kama Wajamaa hawawezi kutumia..Tunawapongeza wale wote ambao kila siku, usiku na mchana, wanafikiria namna ya kutatua matatizo ya nchi na wananchi.
Lakini watu watambue kuwa hakuna muujiza wa kuifanya nchi ipate maendeleo, na kulala na kuamka, matatizo ya nchi na wananchi yakaisha, zaidi ya kufanya kazi kwa bidii, kujinyima, umakini wa mipango na usimamizi, kuzuia ufisadi na miradi yenye mikataba ya hovyo, weledi na uadilifu wa wasimamizi na watendaji wa Serikali.
Nchi yetu ina vitu vingi vya kuisaidia ipige hatua kwenda mbele. KIKUBWA INACHOKIKOSA NI SERIKALI MAKINI, ILIYOJAA WATU WAADILIFU NA WENYE WELEDI. Hilo ndiyo tatizo kubwa la nchi yetu, kuliko mengine yote.
Matatizo yetu kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na mipango mibovu, sera mbaya, sheria mbaya, usimamizi mbaya, wizi, ufisadi, ubadhirifu na weledi mdogo wa wafanya maamuzi na watunga sera.
Serikali yetu imekuwa ni Serikali ya hadaa kwenye mambo mengi. Ni Serikali inayofanya jambo dogo halafu kelele za kujisifu ni kubwa kupindukia. Hata inapofanya makosa, ni mwiko kukiri kuwa imefanya makosa, badala yake ni kuongeza nguvu na jitihada za kujisifu. Ni Serikali defensive, yaani kulinda kwa gharama yoyote yale makosa ambayo inakuwa imefanya.
Angalia hata mkataba wa DP, ni dhahiri kwa mtu yeyote mwenye akili timamu, mkweli wa nafsi na mwadilifu, ataona kwa uwazi kabisa mkataba huo ulivyo wa hovyo na mapungufu mengi, lakini Serikali na watu wake wanapambana usiku na mchana kuwahadaa wananchi kuwa ni mkataba mzuri sana, utakaoondoa tatizo la ajira, na kuifanya nchi iwe tajiri, na kuwezesha kufutwa kwa kodi nyingi na tozo.
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.
Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.
Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.
Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.
Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.
Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.
Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.
Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.
Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?
Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?
Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.
Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.
Utawala wa Samia japo unajitahidi kwenye ujenzi wa miundombinu lakini tusizidishe sifa za uwongo. Siyo kweli kuwa utawala huu utajenga barabara nyingi kuliko tawala zote. Ukweli ni kwamba, hakuna utawala uliojenga kilometa nyingi za barabara za lami kuliko awamu ya 4. Zaidi ya 60% ya barabara zote ndefu za lami zimejengwa wakati wa awamu ya 4. Hakuna utawala uliojenga taasisi nyingi na kubwa mbalimbali kama vile viwanda, hospitali na vyuo, tena vyenye ubora wa hali ya juu, kama utawala wa Mwalimu Nyerere. Hakuna utawala ulioanzisha miradi mingi mikubwa kwa wakati mmoja, kama utawala wa Magufuli. Hakuna utawala uliojenga mifumo mizuri ya uchumi, na aliyeweza kushusha mfumko wa bei kutoka two digits mpaka single digit, kama Mkapa.
Mpaka sasa, hakuna kipya, hata kama kuna mambo mazuri yanafanyika.
Tupunguze sifa za hadaa, tufanye kazi. Nchi bado ni maskini, watu bado ni maskini. Katiba yetu na sheria zetu bado ni mbaya. Uadilifu ndani ya Serikali bado ni hafifu sana. Ubunifu, weledi na umakini ndani ya Serikali bado ni duni. Spidi ya miradi ya maendeleo na ongezeko la pato la Taifa ni ndogo kuliko ongezeko la watu.
Sifa nyingi tunazoipa serikali ni sifa bandia. Tunachotakiwa ni kuzidi kuisukuma serikali kuongeza speed zaidi ili iendane na ongezeko la mahitaji ya nchi.