Si Mpenzi wa kusikiliza kipindi chake cha JAHAZI lakini mara nyingi sana nimebahatika kumsikia Jamaa huyu akiropoka sana, kusema ukweli nilimheshimu sana Kibonde lakini kwa sasa namuona hana maana tena kwa sababu zifuatazo;
Anashabikia mambo yenye ukweli usiopingika, mfano swala la DOWANS ambalo jana alilizungumzia kwa mbwembwe sana, asijue kuwa anazidi kuharibuhali ya hewa, alidai kuwa nchi haiwezi kukosa usingizi kwa sababu ya mtu mmoja anaetaka madaraka kwa nguvu na kwamba kama ni suala la lkutaka kupigiwa kura basi asubiri 2015; sina tatizo na maoni yake kwa hili,, ugomvi wangu ni yeye kujifanya kuwa ndo mwakilishi wa Watanzania wote, aliongea kwa kebehi kubwa sana, je na sisi tutafute au tutumie nafasi zetu kumkebehi?
Pili, Kusisitiza kwake kuwa ni sahihi DOWANS kulipwa na kama kuna anaebisha basi akae kimya, nimemuona ni mtu asie busara kuliko hata mvuta bangi (samahani kama nimekosea)
Tatu, kutaka viongozi wa dini eti wasiingiliea mambo ya nchi ni ujinga kama wanasiasa; na hapa na mimi namuomba kuwa kama yeye si mwana siasa basi aachane na mambo ya siasa la sivyo aondoke kwenye utangazaji aje kwenye siasa.
La mwisho, nawaombeni sana, lugha ya kuwakebehi wengine na kuwaona hawana maana airekebishe upesi; akumbuke alivyokuwa anamponda Mr.Two, lakini yuko wapi sasa, mwenzie ni mbunge na bado yeye ni watch dog tena mropokaji mtaani anaetafuta umaarufu kwa madereva wa daladala na makondakta.
Na kama vipi basi arudi akaendelee na matangazo yake ya Zain yasiyo na impact yoyote.
Narudi tena baadae