Serikali yenu ni sikivu imesikia kilio chenu, naamini litafanyiwa kazi.
Fundi Mchundo said:Makandarasi wazuri wote wamekimbia nchi maana tunachokazania sisi ni bei nafuu na si ubora au ufanisi.
Ogah,
..kwani huko Tanroads tender zinakuwa awarded kwa uamuzi wa CEO peke yake?
..wakati CEO ni raia wa Ghana utendaji Tanroads ulikuwaje?
really can't say.........terminating a contract of such magnitude.........inaacha maswali meengi sana, mara zote contractor atakuwa victim kama akiharibu kazi.........je, huyu mkandarasi alikuwa anaharibu kazi kweli au alikuwa victimized tu??
NB:
..je, CEO wa Tanroads na wasaidizi wake wanapaswa kushtakiwa kwa mashtaka kama yale ya kina Mramba,Yona,na Mgonja?
WAKATI KUKIWA NA MALALAMIKO LUKUKI KUHUSU HALI MBAYA YA MIUNDO MBINU YA BARABARA NCHINI VIGOGO WA WAKALA WA BARABARA TANROADS PAMOJA NA WAKUU WA WIZARANI WAMEMUWA KUPEANA PESA ZA KUPONGEZANA KUPITIA UTARATIBU WA HONORARIA....
MIONGONI MWA MALIPO HAYO NI SH MILLION 40 ZILIZOLIPWA DECEMBER 23 MWAKA JANA KWA VIONGOZI 6 NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MIUNDO MBINU....MALIPO HAYO YALIFANYIKA KWA BARUA KUMB trd/hq/a/c/03/01 ya dec 17....mgao wa awali unaonyesha KATIBU MKUU WA MIUNDO MBINU BW OMAR CHAMBO ALIPWE SH MILLION 8(8,000,000) LAKINI IKAFANYIWA MAREKEBISHO NA AFISA MTENDAJI MKUU ALIPOIPITISHA DEC 18 AMBAPO ALIMUIDHINISHA MILLION KUMI(10,000,000) BADALA YA NANE....AFISA MMOJA ALIPOULIZWA UMUHIMU WA KUGAIANA PESA HIZO ALISEMA NI AHASANTE KWA WALIOFANIKISHA KUONGEZEKA KWA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI WA TANROADS NA HELA HIZO ZILIIDHINISHWA NA BODI NA MANAGEMENTE....LAAAHAULA...WENGINE KATIKA MGAO HONARIA ALIIDHINISHWA KULIPWA MILION SITA NA AFISA MTENDAJI NI KAMA IFUATAVYO...
1))J.M.E MWAKITOSI
2) LOYCE LUGOYE
3))AGNESS MEENA
4)N.J.KIPANDA
5)PETER MHIMBA
HAWA NDIO MAFISADI HALISI WANAOITAFUNA KAMPUNI YA TANROADS WAKISHIRIKIANA NA KATIBU WA MIUNDO MBINU BW OMY CHAMBO....KAZI KWELI KWELI SASA KIKWETE UTAREKEBISHA WIZARA IPI MBONA ZOTE ZINANUKA UFISADI MTUPU......MMMMHHHKWENU WANANCHI
SRCE
MWANAHALISI NEWSPAPER
Vigogo TANROADS wajigawia 'vijisenti'
Mwandishi Wetu Julai 29, 2009
Kigogo wizarani ashirikishwa
WAKATI kukiwa na malalamiko lukuki kuhusu hali mbaya ya miundombinu ya barabara nchini, vigogo katika Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) pamoja na Wizarani wanapongezana kwa kupeana mamilioni ya fedha kupitia utaratibu wa honoraria.
Miongoni mwa malipo ya aina hiyo ni shilingi milioni 40 zilizolipwa Desemba 23, mwaka jana kwa vigogo sita baada ya kuidhinishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS nchini, Ephraem Mrema.
Malipo hayo yalifanyika kufuatia barua kumbukumbu namba trd/hq/a/c/03/1 ya Desemba 17, 2008 ya Kaimu Afisa Utawala, ambaye hata hivyo hakuonyesha jina lake, kwenda kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TANROADS.
Katika barua hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari, Honoraria, Kaimu Afisa Utawala huyo (Ag HRA) anatoa sababu za pendekezo lake la kupatiwa vigogo hao honoraria hiyo kuwa ni kutokana na mchango wao mkubwa walioutoa hadi kufanikisha nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa TANROADS.
Mgawo wa awali wa honoraria hiyo unaonyesha kuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo alipwe shilingi milioni nane lakini ikafanyiwa marekebisho na Afisa Mtendaji Mkuu alipoipitisha Desemba 18, 2008 ambapo alimuidhinishia shilingi milioni 10.
Wengine katika mgawo huo wa honoraria ambao kila mmoja aliidhinishiwa kulipwa shilingi milioni sita na Afisa Mtendaji huyo wameorodheshwa kama ifuatavyo J.M.E Mwakitosi (Kaimu DAP wakati huo), Loyce Lugoye, Agnes Meena, N. J. Kipanda na Peter Mhimba