Teko Modise
JF-Expert Member
- May 20, 2017
- 2,331
- 7,733
Bodi la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) wameamua kupeleka makombe mawili yanayofanana katika viwanja viwili vya Emirates ambapo utapigwa mchezo wa Arsenal Vs Everton.
Kombe la pili litapelekwa kule Etihad ambapo kutakuwa na mchezo wa Man City Vs West Ham.
Sambamba na hayo pia, watapeleka medali 40 katika viwanja vyote viwili ambavyo kiwanja kimojawapo kinategemea kutupa bingwa wa EPL.
Pia itapeleka majukwaa ya ubingwa, shampeni, na itifaki zote za sherehe za ubingwa katika viwanja hivyo viwili.
Japo bosi wa EPL yeye atakuwa Emirates kushudia pambano la Arsenal.
Wenzetu wamejiapanga sana, kuhakikisha kuwa hakuna linaloharibika.
Timu za Man City na Arsenal zinagombania ubingwa ambao utaamuliwa leo katika siku ya mwisho ya msimu, huku Man City akiwa juu kwa tofauti ya alama mbili.
Kwangu mimi kila la heri kwa Man City katika mbio hizo za ubingwa!!