EPL ndo ligi bora duniani

Unajua kitu nilichojifunza hapa ni kwamba watu wanafananisha Ligue na Mashindano mafupi kama CL na Europa Ligue,yaani hyo ni sawa na kusema Kwakua Hussein Bolt anaweza mpita Mo Farah kwenye mbio za mita 100 basi Bolt ni mkimbiaji bora zaidi ya Mo ambae ni bigwa wa mita 1000+ ,hyo logic haimake sense

Timu za la liga ndyo huwa zimedominate hichi kipindi cha miaka 10 lakn yale ni mashindano mafupi huwezi fananisha na mashindano ya ligue ambayo ina mechi 38 hvyo kusema la liga ni bora kwa style hyo sio fair assesment, ukiangalia timu zinazoshinda hyo mashindano yenyewe ya ulaya mara nyingi ni zile zile hyo ina maaanisha hzo timu chache ndo zinafanya ligi ionekane bora kwasababu hizo timu chache zilizojazwa vpaji ndo zinaifanya ligue zima ionekane bora ila ukilinganisha timu moja moja kiuwezo unakuja kuona kwamba sio kweli.

Na pia tungeanza kujiuliza ligue bora inatakiwa kuwa na vigezo gani? Kama Spain ni Ligue bora zaidi kwann mashabiki wa Mpira wengi wanapenda kucheki mechi za PL zaidi ya La liga? Mimi kwa mtizamo wangu,Ligue bora ni ile yenye ushindani mkubwa,Yenye wachezaji bora Wengi,Yenye kuangaliwa na kupendwa na watu wengi zaidi,ambayo haitabiriki mshindi mpka mechi za mwisho kutokana na kutokuwa na tofauti kubwa sana ya viwango katika Club zake!
 
Heshima yako Chifu, naomba huu uzi uishie hapa hapa kwa uchambuzi mzuri ulioutoa hapa
 
Kaka uko vzr sana kwa madini mazuri kichwani, unabishana kwa hoja nzuri na mifano halisi, big up Man.
Wabongo wengi wananunua Vitz sababu za kiuchumi sio kwasababu wanaipenda Vitz sana,EPL inaangaliwa zaidi ya La Liga sababu inapendwa zaidi sio kwasababu za kiuchumi so huwezi fananisha hvyo Vitu!
 
Wabongo wengi wananunua Vitz sababu za kiuchumi sio kwasababu wanaipenda Vitz sana,EPL inaangaliwa zaidi ya La Liga sababu inapendwa zaidi sio kwasababu za kiuchumi so huwezi fananisha hvyo Vitu!
Mkuu naona umejijibu tayari na hakuna tofauti na nilicho comment mimi,tumewasilisha kwa lugha tofauti tu,kupendwa kuangaliwa epl sio kipimo cha ubora wa ligi.
 
Kila mwaka ligi kubwa zinatoa timu bora nne zinazoenda kucheza mashindano makubwa(champions ligue) na timu mbili zilizofanya vizuri zinaenda kwenye mashindano(ueropa ligue). Kama ndani ya miaka kumi kuna ligi moja imetawala mashindano yote mawili kwa kwa kipindi hicho kwa nini tusiite bora? Hata kenya wanaonekana wako mbele kwenye riadha kuliko sisi kwa sababu mashindano makubwa ya riadha wanatawala wao na sio sisi. Tuipende EPL lakini bado haiaifikia la liga kwa ubora hata mashindano ya kombe la dunia mara nyingi wachezaji wanaofanya vizuri la liga inatoa wengi kuliko ligi nyingne.
 
Mimi kwa mtizamo wangu,Ligue bora ni ile yenye ushindani mkubwa,Yenye wachezaji bora Wengi,Yenye kuangaliwa na kupendwa
Sasa kama ligi ya uingereza ndo ina wachezaji bora wengi kwanini wanashindwa kubeba UEFA cup na badala yake kwa mwaka wa kumi sasa timu za Spain ndo zinaongoza kwa kuchukua hilo kombe?

Au ubora wa hao wachezaji unaonekana wakiwa uingereza tu kwenye ligi yao wakipambanishwa na wanaume wenzao wa ligi nyingine kubwa ulaya uwezo na ubora wao unashuka?

Kubalini tu ukweli kwamba ligi yenu ya uingereza imejaza average players na ligi yenu wala sio bora kwa maana ya ubora inavyofahamika.

Ligi yenu ina competition kubwa hilo liko wazi na competition kuwa kubwa haina maana kuwa bora ndo mana timu za Spain zinawaonea kwa sana tu pindi mkutanapo.
 
Na leo liver anaaga champions
 
Sasa kama ligi ya uingereza ndo ina wachezaji bora wengi kwanini wanashindwa kubeba UEFA cup na badala yake kwa mwaka wa kumi sasa timu za Spain ndo zinaongoza kwa kuchukua hilo kombe?

Unajua mnapofeli nyie ni pale mnapoamini kwakuwa timu mbili tatu za Spain zina dorminate basi ndo mna Assume au kupotoka kwamba ligi nzima ni bora, ligi sio timu nne ligi ni timu 20+,ukiangalia hzo timu za Spain zinazodominate miaka yote ni zile zile tu tunazijua Barca,Madrid,Atletico na Sevilla sasa kama hyo ligi kweli ni bora mbna timu zinazoshinda ni hizo hizo? mbna hatuoni timu nyingine?? EPL wachezaji wazuri wapo wengi sema wapo dristributed kwenye timu tofauti tofauti wakati La liga wamejazana kwenye timu 2 sijui 3 mna super teams lakin msijidanganye kwamba hyo ligi ni bora! unafikiri EPL stars kama Hazard,Debruyne,Aguero,Kante,Van dijk wangekuwa timu moja wangeshindwa ku dorminate hyo CL? kama Barca na Madrid?


Tena huo mfano wa Kenya mzuri sana Kenya kweli wale ni bora kwenye riadha na tofauti yao na uhuo mfano wako wa la liga ni kwamba Kenya wanatoa wanariadha wazuri tofauti tofauti karibia kila mashindano wakati La liga timu zinazofanya vizuri ni zile zile hazibadiliki sasa hapo utasema unatimu nzuri au Ligi nzuri?? kwan ligi ni timu 4 tu??
 
Mkuu naona umejijibu tayari na hakuna tofauti na nilicho comment mimi,tumewasilisha kwa lugha tofauti tu,kupendwa kuangaliwa epl sio kipimo cha ubora wa ligi.

Kwamba watu hawana akili wanalipia hela kwenda kuangalia utumbo au? acheni kuongea vitu vya ajabu kama hyo La liga ni bora sana mbna watu hawana habari nayo ss? mpka ifike el Clasico ndo utaanza kusikia watu wakiiongelea mpka hapo unakuwa umejifunza nn kwa akili yko?Ligi ikifika katikati tu tayari ushamjua mshindi kuna ligi hapo? vile vile EPL big mechi zipo nyingi sana uhasama na ushindani unazidi kuongezeka kila mwaka kushinda ubingwa au kuingia Top 4 tu vinazidi kuwa kazi zaidi,makocha bora karibia wote either wapo tayari au wanataka kuja EPL unafikiri kwann labda? vitu vizuri kila siku ndo vinapendwa zaidi mzee
 
Too many words with almost zero substance.

Kwani nyie mmekatazwa kujaza wachezaji wazuri kwenye timu zenu ili mdominate mashindano yote ya ulaya?

Au dhumuni la kufanya usajili kwa kila timu ni nini kama sio ku accumulate wachezaji wazuri watakaoipa timu mafanikio(kuchukua vikombe)?

Au kuna sheria zinazowakataza nyie waingereza msikusanyanye wachezaji wazuri kwenye timu moja kama timu za Spain ili muwe mabingwa wa ulaya?

Halafu hii sababu yako ni less than weak.

Nyinyi hata Europal league ni mwendo wa kuonewa na timu za Spain halafu unaleta tantalila za sijui mmejaza wachezaji wazuri kwenye timu moja.

Mkuu ebu njoo na sababu za kueleweka kuitetea ligi yako mbovu.

Usisahau jana Tottenham kafumuliwa na ajax tena kwao...
 

Kwa hoja ulizotoa hapo unaonesha dhahiri kwamba dhumuni lako hapa ni ili ishinde tu mada tunayo discuss lakini sio kuwa objective na concept halisi,hapa tuna zungumzia LIGI BORA ww unatetea accumulation ya top players kwenye timu moja kitu ambacho kina leta uneven distribution of talents kwenye hyo "ligi yako bora",sasa kama umekusanya wachezaji karibia wote wakali kwenye hyo ligi kwenye timu 3 hapo utabaki na ligi bora au timu 3 bora sana?? hebu tafakari kwanza mkuu.
 
Hahahaaaaaaa.
Mnaruka ruka tu.
Kipimo cha ubora wa ligi za ulaya ni champions league tu. Hizi nyingine kelele.
Kipimo cha shule bora sio mitihani ya mhula ni National examination.
Huwezi jipima ubora kwa kujishindanisha wewe mwenyewe.
Go out there and show your quality.
 
Yani wewe unapima kutazamwa kwa Laliga kwa reference ya Tanzania?
Ufatiliaji wa ligi ni mazoea tu yaliyojijenga toka miaka ya nyuma, zipo nchi zinatazama laliga zaidi kuliko epl.

EPL is full of avarage players na ndio mana unaona kuna ushindani, ushindani hauletwi na ubora wa juu, ukisema ushindani wa timu moja kufunga nyingine ni kipimo cha ubora basi ligi ya bongo nayo ni bora kuliko laliga??

Man U anafungwa na Cristal Palace sio kwasababu Cristal Palace ni bora, ni kwasababu Man U ni mbovu, same applies kwa hizo timu nyingine. Unataka kuniambia Cristal Palace ataenda laliga akaisumbue Baca au Real Madrid pamoja na kiwango chake kibovu kwa sasa??

Kipimo pekee ni champions league na Europe league. Ndio mana ikaitwa ligi ya mabingwa. Inamana kwamba wenye uwezo wa juu katika kila ligi wanawakilisha ligi zao kwenye michuano kuona nani bora zaidi.

Hii mambo ya kuambiana kwamba timu yoyote inaifunga timu nyingine ndio ubora ni invalid kabisa. Hii ni ushindani, kushindana sio lazima muwe na ubora wa juu.

Hii kusema laliga sio bora kwasababu timu ni 2 tu alafu mnasahau kwamba hizi timu mbili kwa misimu kadhaa sasa zimekua zikipokezana kikombe kinachotambulisha mabingwa wa ulaya nzima ni uvivu wa kufikiri.

Real na Baca zimekua katika ubora wajuu sana sio tu laliga bali ulaya nzima.

Sasa timu bora ulaya nzima zitaachaje kushinda vikombe kwenye ligi yao??

Na ukiwatoa hawa real na Baca, hembu angalia records za hawa wengine kutoka laliga kwenye michuano mingine ya ulaya alafu urudi tena.
 
Sijaona fact yeyote hapo zaidi ya mahaba niue,mlikua mnasema Guardiola ni kocha mzuri coz yupo ligi nyepesi,amekuja epl amevunja rekodi kibao za City na bado anawaburuza,jana hiyo team inayocheza ligi ngumu imepigwa 3-0 na Barca,sasa inakuaje ligi ngumu inazalisha team vilaza?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…