Yani umejipinda kununua simu kali halafu uanze tena kutumia 4g wakati eneo lina 5g ya kutosha, Ahh wapi aisee !! miyeyusho hio !!
Ni tahadhari ya mapema kabisa naitoa, kama unataka kununua google pixel jifikirie mara 2, ukiachana na uadimu na bei pasua kichwa kwenye vioo kusababisha wengi kuzipaki simu makabatini, kuna kero nyingine ya kukosekana kwa 5g, kwa nchi za Africa.
Kwenye suala la 5g wapo tofauti na simu nyingine kama samsung / iphone zinazoruhusu kukamata 5g nchi zote
Google Pixel wanaruhusu simu zao zikamate 5g kwenye nchi maalum wanazozitambua, mfano google pixel 6 kuna model inakamata 5g Marekani tu, Nyingine ni kwa baadhi ya nchi za ulaya, nyingine kwa Japan tu.
Kila model kuna nchi zake lakini kwa ujumla kwa nchi zote hizi hapa:
AT (Austria) AU (Australia) BE (Belgium) CA (Canada) CH (Switzerland) CZ (Czech Republic) DE (Germany) DK (Denmark) ES (Spain) FR (France) GB (United Kingdom) IE (Ireland) IN (India) IT (Italy) JP (Japan) NL (Netherlands) NO (Norway) PL (Poland) PR (Puerto Rico) PT (Portugal) SE (Sweden) SG (Singapore) TW (Taiwan) UK (United Kingdom) US (United States)