Epuka kuwambia watu huna kazi au huna mchongo! Hutapata wa kukukopesha wala kukusaidia

Epuka kuwambia watu huna kazi au huna mchongo! Hutapata wa kukukopesha wala kukusaidia

Sikatai kabisa unalosema appearance matters and cloths makes a pirate..., ila point yangu ni kwamba conscious wise kudanganya vitu kama haujazoea pia ni mzigo (na kuishi fake life pia ni shida) kwahio ndio maana nasema if you can be real try to be.....
Upo sahihi kabisa ku fake life ni mzigo..
unawachek wana mwishowe hawapokei simu unawadelete, ukitoboa baadae wao wanakuchek unaona nmba mpya unapokea unauliza we nani?..unakata simu then una mblacklist

Show imeisha!
 
Uko sahihi. Shida zako ziishie chumbani kwako. Ukitoka vaa vizuri, kuwa mchangamfu huku ukitabasamu na epuka kuongelea shida zako. Ukikutana na watu ongelea ishu zao positively badala ya kuongelea ishu zako. Ukipata bahati ya kukutana na matajiri jizuie kuwapiga mizinga au kuonyesha kiashiria chochote cha tamaa. Kwa mfano umekutana nao sehemu ya starehe wakakupa ofa agiza hata maji tu na sio kukimbilia vitu vya gharama.
Hujawahi kushikwa njaa ya kufa chief
 
Wakuu
Ukiulizwa unapiga mishe gani we wambie watu unapga kazi fulani.
Usiwambie sina kazi wanaanza kukuepuka

Kumbuka kua
1.Kila mtu anahitaji mchongo
2.Kila mtu anahitaji connection
3.kila mtu anajisogeza kwa mwenye uafadhari
4.Kila mtu anataka ajuane na mtu mwenye msaada hata kwa baadae
5.Kila mtu anataka mtu useful

Sometimes watu wanatafuta watu au mtu wakumpunguza kwenye circle hasa useless

NB ISHI NAYO HII UTANISHUKURU
Kusema huna kazi, nikosa jinai.
 
Hujawahi kushikwa njaa ya kufa chief
Mkuu sio kitu kizuri kujisifia kupita kwenye shida ila nikuhakikishie nimepita kwenye nyakati ngumu sana wakati fulani kwenye maisha yangu. Mimi kinachonisaidia sio kulia kuwa sina kazi. Huwa nafanya yoyote ya halali iliyoko mbele yangu. Hiyo njaa ya kufa humpata mvivu.
 
Kuna watu wanaamini kuwa na kazi ni mpaka uajiriwe serikalini..ukiajiriwa sekta binafsi au mfanya biashara bado watakuita huna kazi..mi nshaikubali hiyo na nikiulizwa kazi nawambia sina kazi ..kwanza unaepuka mizinga isiyo na maana
 
Kuna watu wanaamini kuwa na kazi ni mpaka uajiriwe serikalini..ukiajiriwa sekta binafsi au mfanya biashara bado watakuita huna kazi..mi nshaikubali hiyo na nikiulizwa kazi nawambia sina kazi ..kwanza unaepuka mizinga isiyo na maana
hao ni machizi
 
Back
Top Bottom