Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui

Erasto Mfugale: Kilichotokea kazini sisi hatujui

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Erasto Mfugale: Kusema kweli hatukuwa tumepata taarifa dhahiri hata imetokea nini kwasababu mimi Jumapili iliyopita nilikuwa kwake Temboni, nimekuwa na mazungumzo naye mpaka saa saba usiku lakini akaniambia kesho nina kikao kidogo kule Dodoma, kwahiyo nitatoka na ndege ya mchana. Nikamuaga nikasema naenda.

Alivyokuwa kule, mtoto wake Aron Mfugale alikuwa anaumwa pia akamtakia hali. Asubuhi amepata chai pale nyumbani kwake Dodoma, akatoka kwenda kazini.

Sasa kilichotokea kazini sisi hatujui, mwisho wa siku nashkuru wizara ya ujenzi kupitia Edgar Msigala nikapigiwa simu lakini akaona hatuelewani, baadae Hija akapiga simu na akaniambia moja kwa moja Engineer amefariki dunia, nilikuwa barabarani Bagamoyo, nilitaka nigongwe na gari maana sikuwa nimetegemea kwasababu jana yake mimi nimekuwa na dada yangu, Frida Mfugale alikuwa na andiko, akasema mimi silielewi peleka kwa kaka yako, Frida ilikuwa aje Bagamoyo kwaajili ya usaidizi wa hilo andiko ili liwe andiko makini.

Basi ni maajabu, sijui kimetokea nini. Tumefika jana Dodoma, tunawashkuru serikali, tumeenda hospitali, tumefatilia ile nyaraka, wanasema hatujui ugonjwa, sasa kulikoni?

Mgonjwa alikuja ameshafariki, alikuwa wapi? Baadae habari zinasemekana alikuwa kazini, sisi hatukuelewa kabisa, tukaendelea kuchanyikiwa, kusema kweli ilituuma kweli lakini hata hivyo Binadamu njia yake ni moja.

PIA, SOMA=> Waziri Chamurilo: Familia(Mfugale) wameonyesha ombwe kwamba ilikuwa haifahamu, Mhandisi Mfugale alisema anajisikia vibaya kikaoni

 
Umeandika haya ukiwa unalenga nini? Hujaeleweka kabisa
Nadhani wanasema kifo cha ndugu yao Mfugale kina utata. Alikuwa haumwi, lakini pia kafikishwa hospitali akiwa ameshakufa. Wakauliza alifia wapi? Wakaambiwa alifia kazini. Hospitali nao wakasema hawajui ugonjwa uliomuuwa.

Hapo sasa labda ripoti ya “postmortem” itawapatia picha kamili kujuwa chanzo cha kifo cha Engineer Mfugale.
 
Kufariki kwa mwanadamu si lazima hadi aumwe.

Wapo watu wanaofariki kwa amani kabisa bila mateso wala ugonjwa.

Muda unafika moyo unafeli tu wenyewe na mtu anaenda zake.

Vijijini huko, kuna wazee muda wao wa kuondoka ukifika unapata anawaita watu wake wa karibu na kuwaaga kabisa.

Kuna wengine utakuta wanafanya usafi nyumba zao, wanakusanya nguo zao na kuweka mahali pazuri, muda ukifika analala zake na anapotelea huko.
 
Back
Top Bottom