Erdogan asema Uturuki inaweza kuzuia ombi la Uswidi la uanachama wa NATO

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
9a50ea1f-8fb5-425c-bdb2-046fb0b87896.jpg

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa Ankara inaweza kukubali Finland kujiunga na Nato, lakini si Sweden.

Alikosoa hatua ya Uswidi kukataa kuwarejesha makumi ya watu wanaodaiwa kufungwa kwa makundi ya wapiganaji wa Kikurdi na wakosoaji wengine wa serikali yake.

"Ikiwa unataka kabisa kujiunga na Nato, utaturudishia magaidi hawa," alisema Bw Erdogan. Maoni yake yanakuja siku chache baada ya Uturuki kusitisha mazungumzo ya kukubali mataifa hayo mawili ya Nordic kuwa wanachama.

Hatua hiyo ilichochewa na msururu wa maandamano yenye utata mjini Stockholm, likiwemo lile ambalo nakala ya Quran ilichomwa moto.

Maafisa wa Uswidi wamelaani maandamano hayo, lakini wametetea sheria za uhuru wa kujieleza nchini humo.

Kujibu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Uswidi na Ufini zilituma maombi ya kujiunga na Nato mwaka jana, na hivyo kumaliza miongo kadhaa ya kutojiunga na jeshi.

Ombi lao lazima liidhinishwe kwa kauli moja na wanachama wote wa sasa wa Nato, lakini Uturuki na Hungary zimeshindwa kuidhinisha.

Katika hotuba yake, Bw Erdogan alisema Uturuki sasa inaweza "kutoa jibu tofauti kuhusu Finland," akiongeza kuwa "Sweden itashtuka". "Tuliipa Uswidi orodha ya watu 120 na tukawaambia kuwarudisha magaidi hao nchini mwao," alisema Bw Erdogan. "Ikiwa hautawakabidhi, basi samahani kwa hilo." chanzo BBC.News
 
Yeye ndiye ataondoka NATO wavaa kobazi vichwa ni Kwa ajili ya kubebea nywele na ndevu tu.
Wangekuwa wanaweza kumtoa uturuki wangeshamtoa zamaniiiii sababu uturuki haburuzwi yy ana misimamo ya nchi yake kiuchumi kama sasa hv nato wenzake wanamuwekea vikwazo russia yy ndio anaanza ujenzi wa bomba la gesi,tatizo mnaichukulia turkey easy
 
Turkey Iko easy mkuu, Edorgan anajua hilo na hapo kwake hapaamini sana. Marufuku Turkey kujiunga EU
 
Katika hotuba yake, Bw Erdogan alisema Uturuki sasa inaweza "kutoa jibu tofauti kuhusu Finland," akiongeza kuwa "Sweden itashtuka". "Tuliipa Uswidi orodha ya watu 120 na tukawaambia kuwarudisha magaidi hao nchini mwao," alisema Bw Erdogan. "Ikiwa hautawakabidhi, basi samahani kwa hilo." chanzo BBC.News
Anajaribu tu kutingisha kiberiti huyu...hiyo ndio kete yake muhimu ya kushinda uchaguzi nchini mwake.
 
Sasa wewe ndio umeongea pointi kama msomi!!!!Lazima afanye kitu kwa sababu uchaguzi unakuja na waafidhina wa chama chake wanataka msimamo kutoka kwake kama mwenyekiti wa chama!!!!Huwezi kuwaita wakurdi magaidi kisa wanadai haki zao!!!!!!Swedeni itajiunga na NATO sababu wazungu wanajuana!!!Kama ambavyo uturuki inapigania kujiunga na umoja wa ulaya EU!!!
 
Kasome tena historia na jiografia , Kardinali wako kakuingiza choo cha kike na kukulisha tango pori
Sasa nyie mnatukanana hata mambo ya NATO hamjui tayari mshaingiza mambo ya udini!!!!!Mbona uturuki hakuna mambo ya kuvaa kobazi!!!!Pombe,brothel,casinos kama kawa mzee full kujiachia kwenye fukwe za kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo!!!!
 
Mbona umenijia mimi hukumwona yule aliyeandika ?? mimi si nimejibu tu ??
 
Sasa wewe ndio umeongea pointi kama msomi!!!!Lazima afanye kitu kwa sababu uchaguzi unakuja na waafidhina wa chama chake wanataka msimamo kutoka kwake kama mwenyekiti wa chama!!!!Huwezi kuwaita wakurdi magaidi kisa wanadai haki zao!!!!!!Swedeni itajiunga na NATO sababu wazungu wanajuana!!!Kama ambavyo uturuki inapigania kujiunga na umoja wa ulaya EU!!!

Kasome tena siasa za Sweden , Kuingia Nato si rahisi kwani upinzani mkubwa uko ndani wa kujiunga na Nato na ndio wakaja hao waliochoma Quran kuongeza petroli kwenye moto
 
Udini umekujaa kichwani mpaka umekuwa mpuuzi hivi unaujua umuhimu wa Uturuki ndani ya NATO au unaropoka tu?
Uturuki ni nchi ya pili kwa kuchangia wanajeshi NATO baada ya marekani!!!Afu mbona uturuki hakuna mambo ya kuvaa kobazi!!!!!Ni nchi poa sana kila kitu unapata mpaka ganja na kuna club's,kuna brothel,s and business connection,s zipo sana Antiokia city na kuna unique bata za kufa mtu kuliko hata Dubai!!!!Na mademu wa kituruki waelewa sana ukikutana nao!!!Sema Uturuki imeshindwa kujiunga na umoja wa ulaya kwa sababu moja tu nayo ni dini!!!!!Majority ya waturuki ni waislamu na umoja wa ulaya japo hawasemi wazi ila dini ni kigezo kikuu kujiunga!!!!Pamoja na yote Swedeni itajiunga na NATO sababu wazungu wa ulaya waga wanajuana it's matter of time!!!!
 
Sasa nyie mnatukanana hata mambo ya NATO hamjui tayari mshaingiza mambo ya udini!!!!!Mbona uturuki hakuna mambo ya kuvaa kobazi!!!!Pombe,brothel,casinos kama kawa mzee full kujiachia kwenye fukwe za kaskazini na mashariki mwa nchi hiyo!!!!

Wazungu hawana kujuana kuna maslahi , kasome waswedish waliwafanyia nini Wadenmark na wa Norway wakati wa vita vya 2 vya dunia , sio siri hiyo
 
Uturuki ni nchi ya pili kwa kuchangia wanajeshi NATO baada ya marekani!!!Afu mbona uturuki hakuna mambo ya kuvaa kobazi!!!!!Ni nchi poa sana kila kitu unapata mpaka ganja na kuna club's,kuna brothel,s and business connection,s zipo sana Antiokia city na kuna unique bata za kufa mtu kuliko hata Dubai!!!!Na mademu wa kituruki waelewa sana ukikutana nao!!!Sema Uturuki imeshindwa kujiunga na umoja wa ulaya kwa sababu moja tu nayo ni dini!!!!!Majority ya waturuki ni waislamu na umoja wa ulaya japo hawasemi wazi ila dini ni kigezo kikuu kujiunga!!!!Pamoja na yote Swedeni itajiunga na NATO sababu wazungu wa ulaya waga wanajuana it's matter of time!!!!

Umeandika vizuri kuhusu Uturuki ila hapo kwenye Sweden kuna kasoro
 
Kasome tena siasa za Sweden , Kuingia Nato si rahisi kwani upinzani mkubwa uko ndani wa kujiunga na Nato na ndio wakaja hao wanaliochoma Quran kuongeza petroli kwenye moto
Watajiunga tu na NATO!!!Kaka sio nisome siasa za swedeni bali nimeishi huko kaka!!!Wanaochoma Quran ni wanasiasa wenye mrengo wa kulia wanaopinga wahamiaji!!!Hakuna tofauti na kesi ya Indonesia pale serikali ya jimbo moja ilipoamua kuchoma dozeni za biblia!!!!Ni masuala ya siasa za ndani
 
Back
Top Bottom