Eric Garcetti: Ni jambo la kufurahisha kuona Demokrasia kubwa zaidi duniani ikifanya kupitia uchaguzi wa India

Eric Garcetti: Ni jambo la kufurahisha kuona Demokrasia kubwa zaidi duniani ikifanya kupitia uchaguzi wa India

Joined
Feb 22, 2024
Posts
10
Reaction score
10
Mumbai (Maharashtra) [India], Mei 22 (ANI):
Wakati uchaguzi wa Lok Sabha unafanyika nchini India katika awamu ya saba, Balozi wa Marekani nchini India, Eric Garcetti amesema kuwa Dunia imeshangazwa na inashuhudia demokrasia kubwa zaidi ikitendeka kupitia Uchaguzi huo.

Akiwa mwangalizi kwa mara ya kwanza, Garcetti alisema kuwa alivutiwa na kampeni zenye nguvu, na mikutano iliyokuwa ikiendelea kote nchini, na akaongeza kuwa ilisisimua kushuhudia yote hayo.

Akizungumza na chombo cha Habari cha ANI, Balozi huyo alisema "Ni jambo la kushangaza kuona demokrasia kubwa zaidi duniani ikifanya Kupitia uchaguzi mkubwa zaidi duniani na tumeona kampeni zenye nguvu ajabu, tumeona vyama, tumeona mikutano, na ni kitu kimenitia moyo kama mwangalizi wa mara ya kwanza nimefurahishwa kuona jambo hili na ninawatakia wananchi wa India mafankio mema.

Uchaguzi wa Lok Sabha unafanyika nchini India katika awamu saba na Kuhesabu kura kutafanyika Juni 4.

Wakati Chama cha Bharatiya Janata kinachoongozwa na Waziri Mkuu Narendra Modi kinatafuta muhula wa tatu mfululizo madarakani, Muungano wa upinzani wa INDIA unalenga kunyakua madaraka kutoka kwa BJP inayoshikilia madaraka kwa sasa.

Waziri Mkuu Narendra Modi, anatafuta muhula wake wa tatu kutoka kwa Mshindani wake Varanasi.Kwenye Uchaguzi wa 2014-2019 Modi alimshinda mpinzani wake huyo kwa kura nyingi

Akisifu ukuaji wa India, Garcetti alisema mataifa hayo mawili ni "washirika wa asili". "India ni nchi yenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi katika ulimwengu unaoendelea na Marekani ni nchi ya uchumi unaokua kwa kasi zaidi katika ulimwengu ulioendelea," alisema.

"Sisi ni washirika wa asili na sisi ni marafiki na ikiwa Marekani na India zinaweza kuendelea kupanua uchumi wetu pamoja, tunaweza kufanya mambo mazuri sio tu kwa nchi zetu wenyewe, ajira, na ustawi wa kiuchumi, bali tunaweza kusaidia dunia kwa kupanua mnyororo wa usambazaji, kwenda maeneo kama Afrika, Asia ya Kusini-Mashariki, nchi za visiwa vya Pasifiki..." alisema balozi huyo.

Alibainisha kuwa India na Marekani daima zimekuwa na ushirikiano thabiti wa pande mbili.Pia alizungumzia uhusiano uliopo kati ya India na Marekani katika sekta ya anga za juu.

"Unajua, uhusiano wetu katika anga za juu ni kama uhusiano wetu Duniani. Ni imara zaidi kuliko ilivyowahi kuwa katika historia yetu. Tuna uwezo huu wa kuhakikisha kwamba Marekani na India sio tu zinaongeza uhusiano, bali ni uhusiano unaozidisha. Tutawaweka Wahindi angani mwaka huu kwenye misheni ya Marekani," Garcetti aliambia ANI.

Alibainisha kuwa nchi zote mbili pia zitakuwa na setilaiti pamoja, ambayo itazinduliwa mwaka huu.

"Tutakuwa na setilaiti tuliyoijenga pamoja. Inaweza kusaidia kuokoa sayari yetu, kuzinduliwa mwaka huu.

Nadhani hatungeota haya miaka mitano iliyopita... ndio maana mada hii ilikuwa muhimu sana kwetu. Mara nyingi tunasema uhusiano wetu ni kutoka kwenye kina cha bahari hadi nyota. Sasa ni hivyo," Garcetti alisema. (ANI)

BB1mSa86.jpeg
 
Back
Top Bottom