#COVID19 Eric Kabendera: Magufuli alifariki kwa COVID-19 mwaka 2021

#COVID19 Eric Kabendera: Magufuli alifariki kwa COVID-19 mwaka 2021

View attachment 3192824
Katika kitabu chake cha In the Name of the President, Ndugu Eric Kabendera ameonyesha kuwa Hayati Magufuli alifariki kwa COVID-19.

Ikumbukwe kuwa katika utawala wa Magufuli masharti ya watalaam wa afya kutaka watu kujikinga na maambukizi kama kuvaa barakoa yalikuwa hayazingatiwi hasa katika maeneo ya umma.

Kimya cha serikali ya Tanzania kiliendelea kuzua wasiwasi hasa miongoni mwa wananchi, watalaam wa afya na wanaharakati wa haki za binadamu, ambao walizuiwa kuzungumzia maambukizi hayo hasa kupitia mitandao ya kijamii.
Kwahyo Corona iliisha au imeishaje!?
 
haujanielewa, ninachomaanisha vifo vya viongozi waandamizi vilikua na clear pattern ambayo ukifanya analysis utagundua kuna kitu nyuma zaidi ya maelezo mepesi ya kusingizia 'covid'. There is a clear pattern juu ya timing na mfuatano wa vifo (mahiga, kijazi, mfugale, mkapa, kwandikwa, magufuli et al). Pattern ambayo hatujaiona tena ikiendelea kwa viongozi baada ya kifo cha JPM. Swali, covid sasa hivi imeenda wapi? mbona viongozi hawafululizi kufa kwa kupishana wiki moja au mbili tena?
Covid-19 imeenda wapi,ina maana haikuwepo au toka huko china na duniani ilikua maigizo!?.. kuhusu mkapa hata jakaya alilalamika kwamba 'jana nilikua nae, alikua mzima,mara naambiwa kafa'..hapa tumuulize yule dikteta wako aliyedaiwa kutaka kutawala milele,lakini mpango alipona na mkapa hakuwa na covid-19,mahiga,mfugale,kijazi,wauawe Ili iweje?.. yaani mhandisi wa madaraja mfugale auawe Ili iweje!?.. duniani kote covid-19 haipo kwa sasa
 
Kuisafisha huchafuki, ila ukitaka kuchafua ndipo unachafuka...
Crude oil ni chafu na husafishwa kuwa mafuta ya kila aina ikiwemo grease safi, petrol, oil, diesel, oaraffin nk. Tatizo oil chafu huwezi tena kuipurify iweze kuwa safi elewa hapo 😀 Magu hakuwa msafi na anayetaka kimsafisha ataishia kuchafuka yeye tu.
 
We dogo una mtindio wa ubongo si bure...
Achana na reply zangu, huwezi kuzielewa.
Kuniita dogo haiwezi kusaidia.

Fafanua, iweje mtu kaandika kitabu tu unataka auawe?

Tukitaka kila mwny maoni tofauti na upendavyo wewe auawe, na wewe si itabidi uuawe kwa kuwa una maoni tofauti na mimi?

Wewe na huyo jiwe mwendazake, nani aliwapa mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu wengine kisa tu wanaandika au kusema vitu msivyopenda?
 
Fatilia comments zangu za nyuma kuhusu Eriki kaflag.
Tatizo lako una mihemko sana.
Na fatilia pia comments na reply za wenzio kwenye hiyo comment yangu ndo ujue ni kwa namna gani una mihemko.
 
View attachment 3192824
Katika kitabu chake cha In the Name of the President, Ndugu Eric Kabendera ameonyesha kuwa Hayati Magufuli alifariki kwa COVID-19.

Ikumbukwe kuwa katika utawala wa Magufuli masharti ya watalaam wa afya kutaka watu kujikinga na maambukizi kama kuvaa barakoa yalikuwa hayazingatiwi hasa katika maeneo ya umma.

Kimya cha serikali ya Tanzania kiliendelea kuzua wasiwasi hasa miongoni mwa wananchi, watalaam wa afya na wanaharakati wa haki za binadamu, ambao walizuiwa kuzungumzia maambukizi hayo hasa kupitia mitandao ya kijamii.
Pumbavu sana.Sasa hii ni habari? kufa kwa COVID siyo habari .Tanzania walikufa wengi na duniani kwa ujumla.Kwa hiyo Magufuli kufa kwa Covid siyo habari.Ni maradhi miongongoni mwa maradhi .Angekufa kwa kupigwa amefumaniwa hiyo ndiyo ingekuwa habari.
Yaani hiki Kibendera na Kitabu chake anachemka kwelikweli.
 
Fatilia comments zangu za nyuma kuhusu Eriki kaflag.
Tatizo lako una mihemko sana.
Na fatilia pia comments na reply za wenzio kwenye hiyo comment yangu ndo ujue ni kwa namna gani una mihemko.
Hakuna hoja yeyote uliyojibu hapa.

Ni watanzania msiojitambua, huna hoja.

Lakini mimi nakuambia, ipo siku mtawaeleza watanzania, mamlaka ya kuteka na kuua mliyatoa wapi, mark my words.
 
Wakitaka kumjua aliempa COVID ni dogo mmoja katika walinzi wake, alipokuwa sokoni Morogoro waangalie kwa makini video.

Kuna dogo alikuwa anaisambaza

Shida pia ni utaahira wake alikataa chanjo, ni kujitakia (uwezi shindana na bwana godi).

Worst unataka kuwapangia na wengine wasipate chanjo ushajiona mungu mtu (hakukuwa na namna he had to be eliminated, sad). Ndio uhalisia mambo mengine sio ya kuvumilia sad but justified on the token of greater utility,

Mambo mengine hayataki emotional, ningeamuru same thing hata ningekuwa mimi japo nilimkubali sana jamaa (uwezi zuia chanjo kwa wengine kisa imani zako) that’s just stupid and unacceptable.
The positive aspect is that he passed away while fearlessly defending his beliefs, standing firm in the face of intimidation, and refusing to bow to the imperialists, making him a true hero.
 
Magufuli bado anaishi kwenye mioyo ya watanzania walio wengi , yaani kama hawaamini wamshindanishe aliyekuwepo na hayati watapata majibu..

Japo binafsi sikuwa na mkubali ila kumchafua Magufuli kutabakia mitandaoni mtaani unaweza kuchapwa viboko hawawezi kukuelewa na itachukua miaka mingi kulifuta jina lake kwenye Mioyo ya Watanzania walio wengi.
 
M
Anyway twendeni taratibu kimsingi COVID 19 ni ugonjwa wa virusi unaoenea haraka sana kwa njia ya hewa, majimaji kutoka kwa muathirika kupitia kugusana, kukaribiana etc
Kipindi late President yupo hospital alikuwa kazungukwa na viongozi wakuu wa nchi na vyombo vya usalama ambao walikuja kukubali kuwa waliongea nae mambo kadhaa hata kuwaomba wamrudishe kwao Chato.
Kwa namna coyote kama ingethibitika ni COVID 19 hill lisingewezekana maana angewekwa totally quarantine bila kukaribiana na watu wengine kuzuia maambukizi zaidi.
Kimazingira Inaonesha haikuwa Covid 19 na ndiomaana walikuja na hoja ya ugonjwa na moyo sasa wameturn to covid. Twende tu taratibu ukweli utajulikana tu.
mmh !
 
Back
Top Bottom