Se Busca
Member
- Dec 11, 2023
- 69
- 260
Pichani ni Eric Mandala Kizenga, raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Fally Ipupa alitunga wimbo maarufu kumsifia mkewe, Maria Piron Mandala (PM). Wimbo huu ulizua gumzo sana, na kuonyesha namna alivyokuwa akimpenda mkewe.
Hata hivyo, kuanzia juzi, habari kuhusu Eric Mandala zimekuwa tofauti kabisa. Mtu huyu ambaye alikuwa akitajwa kuwa na utajiri mkubwa nchini Kongo sasa amekumbwa na kashfa kubwa. Juzi, akiwa nchini Colombia, Eric Mandala alikamatwa akiwa na kilo 200 za cocaine ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa kwenye moja ya malls maarufu nchini humo.
Cocaine hiyo inadaiwa ilitoka Ecuador na ilikuwa inaelekea Morocco kupitia bandari ya Algeciras, Hispania.
Mandala alikamatwa pamoja na mwanamke wa Kikolombia, na walikamatwa wakiwa na kiasi cha dola 50,000 za kimarekani taslimu. Polisi waligundua kuwa Eric Mandala alikuwa akifuatiliwa na maafisa wa kudhibiti dawa za kulevya tangu Agosti mwaka jana, na hatimaye alikamatwa juzi kwenye mtego wao.
Zaidi ya hayo, mwaka 2020, Eric Mandala alijivunia kununua nyumba ya kifahari katika jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, jijini Dubai, kwa kiasi cha Euro milioni 1.85 cash, jambo ambalo lilishangaza wengi na kuacha vinywa wazi.
Wakati Eric Mandala akisota kwenye mikono ya polisi, maswali yanajitokeza kuhusu kama Adolphe Muteba Tshilamwina ataungana na mzozo huu au ataepuka mtego huu. Hali inavyokuwa ni ngumu kusema, lakini ni wazi kuwa hadithi hii itazidi kutoa makala nyingi.