Pre GE2025 Eric Shigongo: Miaka mitatu ya Rais Samia Buchosa imeendelea sana

Pre GE2025 Eric Shigongo: Miaka mitatu ya Rais Samia Buchosa imeendelea sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
"Ninayo kila sababu ya kuishukuru serikali kwa namna inavyowatumikia wananchi wake. Ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan jimbo la Buchosa peke yake mimi kama mbunge nimepokea bilioni 63 za maendeleo, tumejenga barabara, tumejenga vituo vya afya vitano tumejenga sekondari mpya zaidi ya 8 tumejenga zahanati za kutosha karibu 21 imejenga madarasa ya kutosha kila kona. Wananchi wa Buchosa wanakuambia maisha yao yamekuwa bora kuliko yalivyokuwa zamani kwa sababu serikali ya Chama Cha Mapinduzi inafanya kazi."

"Haya yote yanafanyika katika taifa ambalo moja limefiwa na Rais wake, yote haya yanafanyika dunia ikiwa uchumi wake umetetereka kwa sababu ya Covid 19, kwa sababu ya vita vya Ukraine kwa sababu ya vita vya mashariki ya kati."

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Eric Shigongo Mbunge wa Jimbo la Buchosa akizungumza leo Februari 22 na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam.
20250222_194105.jpg
 
Sema mh Eric, kwenye kitabu chako kimoja ulitupiga kama eti mjukuu wa yule mmiliki wa magari ya Ford ya marekani alikupendaga.

Hiyo ilikua kamba mzee, yaani mahensam wooote ulaya na marekani walitoswa ukaja kupendwa wewe mbunge wa buchosa
 
Huyu Shigongo anatusemea ambavyo sivyo, hayo maendeleo mimi niliyekuwepo kwenye hii almashauri ya Buchosa wala siyaoni!
Wavuvi tunateseka mno, ushuru kila kona hata ukiwa na mboga ya kilo kumi kupeleka nyumbani wanakutoza ushuru mkubwa kwenye vyombo vya usafiri.
 
Kwahiyo awamu ya kwanza,ya pili ,ya tatu, ya nne,ya Tano zote hazikufanya kitu chochote sio?
 
Back
Top Bottom