Kwa jinsi nilivyo ona "P.O. Box 7439" na kuhusishwa na kampuni yenye miamala hapo juu, naanza kumuelewa Mzee JK alivyosema "sasa bora tusomeshe wanasayansi au wahandisi zaidi kuliko watu wa arts wanaokuja kuwa wanasheria.
Wanasheria wakikosa kazi wanajiingiza kwenye siasa na nchi haitawaliki."
Kwa busara zake na washauri wake wakaanzisha vipaumbele kwenye mikopo ya elimu ya juu.
Wanasayansi wakapewa hadi 100% na watu wa sayansi ya jamii, lugha na sanaa wakapata kiwango kidogo.
Sikumuelewa kwa ubaguzi wake, kumbe alikuwa na mengi ana yaona kwenye makabrasha yake ambayo mengine kamuachia mrithi wake,nae analalamika anakesha akiyasoma.